GE2025 Mimi nataka mabadiliko Tanzania ila siungi mkono maandamano au mapinduzi ya kijeshi

GE2025 Mimi nataka mabadiliko Tanzania ila siungi mkono maandamano au mapinduzi ya kijeshi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
KAMA SIAMINI MABADILIKO KWENYE MAANDAMANO NTATUMIA NJIA GANI HILI MABADILIKO YATOKEE NDO SWALI AMBALO MTU YEYOTE ATANIULIZA AU ATATAKA KUJUA

JIBU NI-MAOMBI
Vijana au watu wengi sana wanaogopa kusema kwamba ntatumia njia ya maombi kufanikisha jambo langu-wengi wanaogopa kwamba wataitwa vichaa, hawana akili na kejeli nyingine

Mimi nampenda Yesu na kupitia yeye naamini kama nchi tutavuka salama tarehe 29 na sio tu kuvuka salama kwa amani bali na mbadiliko yatafuata mfano wa hayo niliyoyataja hapo juu

Nina siku 12 za kujinyenyekeza kwa Mungu na kumlilia ili aiponye nchi ambayo ipo kwenye uncertainty

Naheshimu wale ambao mnaamini kwenye njia nyingine za kudai haki ila sizi-ungi mkono
Mkuu umeandika vizuri ila hapa kwenye kusema maombi kupitia Yesu ndo yataleta mabadiliko umeharibu kabisa hoja zako. Inaonyesha hujui kabisa ufanyeje kupata mabadiliko unayoyataka ukaamua kujificha kwenye kichaka cha dini na kumtaja Yesu. Jenga hoja za kisomi badala ya kuwa kama wafuasi wa Mwamposa.
 
Tunashukuru kwa maoni ila tulipofika bora jeshi lichukue nchi
Acha kujidanganya. Jeshi kushika nchi ndo kujichimbia kaburi kabisa kimaendeleo. Dunia ya leo inahitaji democracy na diplomasia ya hali ya juu ili kwenda sawa. Wanajeshi wao kila kitu amri hawataweza kwenda sawa na kasi ya dunia.
 
Ujinga huu, sasa unataka mabadiriko yapi ya msimu wa mvua?

Tawala za ki fascist haziondoki bila mapinduzi.

Sema hutaki mabadiriko kabisa, landa una nufaika na yanayoendelea.
 
Miezi ya hivi karibuni kuna mtanzania anaishi marekani anaitwa mange kimambi na ameitisha maandamano na mpaka sahivi anayapigia debe kwa njia mbalimbali kupitia mtandao wa instagram
  1. Wako watakaopiga kura
  2. Wako wanaosupport maandamano
  3. Wako wanaopinga
  4. Wako ambao hawajajua wako upande upi wanasubiria siku hiyo waone upepo
  5. Wako wanaombea mapinduzi ya kijeshi
MIMI DENNIS ROBERT SHUGHURU SISUPORT MAANDAMANO AU UHASI WOWOTE ILI KUFIKIA MABADILIKO NI UKWELI KAMA NCHI TUNAHITAJI MABADILIKO ILA KWA MTIZAMO WANGU SISUPPORT MAANDAMANO

HASARA ZA KUTEGEMEA MAANDAMANO IN LONG RUN
  1. Kuwa na jamii inayopenda shortcut hasa linapokuja swala la kutatua changamoto mfano Madagascar mwaka 2009 waliandamana na jeshi likamtoa Marc Ravalomanana na walimuweka Andry Nirina Rajoelina kupitia maandamano, mwaka 2025 wamentoa Andry nirina rajoelina kupitia maandamano kwa hiyo unaweza ona hiyo pattern
  2. Maandamano yanaweza yakazaa mambo mengine mfano uasi na vikundi vya waasi n.k mfano mwaka 1977 Mengistu Haile Mariam afisa wa ngazi za chini jeshini alifanya mapinduzi akawa waziri mkuu wa Ethiopia matokeo yake yakazaliwa vikundi vya waasi eneo la ahmara na tingranya mpaka utawala wa abiy Ahmed unaipitia hii changamoto kwa hiyo unaweza ona hio pattern
NI UKWELI MIMI BINAFSI NATAKA MABADILIKO KAMA ILA SIO KUPITIA MAANDAMANO NA MAPINDUZI YA JESHI NA NI KAMA YAFUATAYO
  1. Msajili wa vyama vya siasa asichaguliwe moja kwa moja na Rais
  2. Mkuu wa tume ya uchaguzi, na wajumbe wa tume ya uchaguzi wasichaguliwe na Rais
  3. Mkuu wa Takukuru asichaguliwe na Rais
  4. Dpp asichaguliwe na Rais na DCI (Director of criminal investigation) asiwe chini ya polisi bali awe chini ya ofisi ya DPP
  5. Rais awe eligible kushitakiwa akiwa amestaafu kama kuna makosa alifanya
  6. Spika wa bunge asiwe affiliated na chama cha siasa
  7. Mshindi wa pili kwenye matokeo ya Urais atakuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni
KAMA SIAMINI MABADILIKO KWENYE MAANDAMANO NTATUMIA NJIA GANI HILI MABADILIKO YATOKEE NDO SWALI AMBALO MTU YEYOTE ATANIULIZA AU ATATAKA KUJUA

JIBU NI-MAOMBI
Vijana au watu wengi sana wanaogopa kusema kwamba ntatumia njia ya maombi kufanikisha jambo langu-wengi wanaogopa kwamba wataitwa vichaa, hawana akili na kejeli nyingine

Mimi nampenda Yesu na kupitia yeye naamini kama nchi tutavuka salama tarehe 29 na sio tu kuvuka salama kwa amani bali na mbadiliko yatafuata mfano wa hayo niliyoyataja hapo juu

Nina siku 12 za kujinyenyekeza kwa Mungu na kumlilia ili aiponye nchi ambayo ipo kwenye uncertainty

Naheshimu wale ambao mnaamini kwenye njia nyingine za kudai haki ila sizi-ungi mkono
Maombi yanakupa nguvu halafu unazitumia hizo nguvu kutenda (act) ,kumbuka Imani bila matendo imekufa

Soma Joshua 1:9
 
huyu jamaa nishagundua ni mgonjwa wa akili(rejea upuuzi alokuwa akipost kipindi fulani hivi) asa unategemea nini kutoka kwa mtu kama huyu? Denis anaumwa na hataki matibabu!
Aaah!
Kumbe ni yule yule ambaye huwa sijisumbui kumsoma?
Nashukuru kwa kunistua. Sitahangaika naye tena hapa.
 
Kuna mtu kakutisha? Akutishe wewe kwa sababu zipi hasa!
Binafsi sina la ziada na wewe tena, maadam nishajuwa hali yako ilivyo.
Tumia jina lako halisi ndo urudi, mkuu unanifananisha na wewe ambaye unatumia jina fake alafu unajiona mjanja na mwerevu
Werevu wote wanajiamini
 
Tumia jina lako halisi ndo urudi, mkuu unanifananisha na wewe ambaye unatumia jina fake alafu unajiona mjanja na mwerevu
Werevu wote wanajiamini
Nimekwisha kueleza. Sina la ziada na wewe tena kwa kujuwa hali yako ilivyo. Hayo ya jina yatakusaidia kitu gani mtu duni kama wewe.

Sasa hadi unataka nikufafanulie maana ya kutumia jina ninalotumia? Hili nalo ni jambo la kung'ang'ania nalo kweli?

Wewe kama wewe, ukinijuwa itakusaidia kitu gani wewe?
 
Kama hutumii jina lako halisi means hujiamini na unasumbuliwa na uoga sasa mimi nimeshavuka hiyo level najiamini na niko real
Isije ikawa nabishana na robot
 
Kama hutumii jina lako halisi means hujiamini na unasumbuliwa na uoga sasa mimi nimeshavuka hiyo level najiamini na niko real
Isije ikawa nabishana na robot
Ni rahisi sana kwangu kuingia kwenye akili hizo hizo za kichizi ili tuelewane vizuri. Kwa hiyo kama unanihitaji kwa namna hiyo nitaacha mengine yooote ili tuendelee na huu uchizi unaotafuta kuuendeleza hapa..
 
Mkuu umeandika vizuri ila hapa kwenye kusema maombi kupitia Yesu ndo yataleta mabadiliko umeharibu kabisa hoja zako. Inaonyesha hujui kabisa ufanyeje kupata mabadiliko unayoyataka ukaamua kujificha kwenye kichaka cha dini na kumtaja Yesu. Jenga hoja za kisomi badala ya kuwa kama wafuasi wa Mwamposa.
Yesu ndo kila kitu yeye ndo anayetupa mbinu au mawazo ya kufanikiwa kwenye nyanja zote za maisha

Kama baadhi ya viongozi wanatembea na irizi, wanaenda kwa waganga unaonaje ajabu mimi kumuamini Yesu
 
Ni rahisi sana kwangu kuingia kwenye akili hizo hizo za kichizi ili tuelewane vizuri. Kwa hiyo kama unanihitaji kwa namna hiyo nitaacha mengine yooote ili tuendelee na huu uchizi unaotafuta kuuendeleza hapa..
Nikurahisishie wewe niite
  1. Chizi
  2. Mjinga
  3. Kichaa
  4. Na mengineyo
Hakuna hata jina moja utakaloniita litaanidhuru na kama ndo sehemu yako ya kujifurahisha endelea
Usidhani kuniita hivyo unanikera unapoteza nguvu zako
 
Sasa natenga muda rasmi tuendelee na mada yako hii.
Hayo yote uliyo orodhesha hapo ni sifa halisi zinazo akisi ulivyo. Unabisha?
 
Tanzania Itakua nchi ya Kwanza kupata mabadiriko kwa Maombi.

Hata Farao, Aliwaachia wana wa izraeli baada ya Mungu kumwaga damu za mtoto wa kwanza kwa kila Familia
 
Back
Top Bottom