Mimi ni Mkristo mlokole, nimeanza kukosa Imani na ukristo nahisi Uislam ndiyo dini ya kweli

Uko sahihi kabisa baada ya miaka 10 ukristo utakuwa sawa na fiesta.
Ona ibada za siku hizi za akina amsanja vijana wanapenda vitu rahisi rahisi.
Manabii sasa ndio usiseme.
Ukristo unajifia
Upo sahihi sana
 
Huko Vatican walijifungia siku 26 na mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini duniani
Wamekuja na mkakati gani siku zote hizo

Mkakati ni ule ule haujawahi badilika,

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Marko 16:15-16
 
Ulikua mkristo wa kanisa yani wa kujiandikisha namaanisha. Uliwakuta wazazi ni wakristo tu na wewe ukaingia wala hukupata nafasi ya kumtafuta wewe binafsi niseme haukuwa wa kristo wewe. Huyu kristo ukimjua hakuna namna unayodhani unaweza kuachana nae.
 
Tatizo unakwenda kanisani kuangalia watu na vitu hujaenda kumtafuta Mungu na nguvu zake...
Kwani biblia inaposema ninyi ni chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu inamaanisha nini?
 
Ulikua mkristo wa kanisa yani wa kujiandikisha namaanisha. Uliwakuta wazazi ni wakristo tu na wewe ukaingia wala hukupata nafasi ya kumtafuta wewe binafsi niseme haukuwa wa kristo wewe. Huyu kristo ukimjua hakuna namna unayodhani unaweza kuachana nae.
Nimependa comment hii...

Ukimjua Kristo huwezi kuachana nae...
 
Yesu Hana kanisa ,kanisa linaongozwa na mchungaji Kila muumini ana mchungaji wake ,mchungaji akipotoka kanisa lote linapotoka !
Sio mara zote aisee. Kumbuka alimwambiaje Elia baada ya Elia kukata tamaa na kulalamika Mungu amchukue tu maana Yezebel anaitafuta roho yake? Alimwambia nimejisaazia watu 7000 wasiopiga goti kwa baali. Na walikua kati ya Israel wachafu mno. Kuanzia ndani ya nyumba ya Kifalme.
 
Napenda sana ibada ,naamini kupitia ibada mambo mengi yanaweza kuwa sawa! Napata shida kidogo na Imani yangu ya ukristo ,miaka ya 1980 ---1990 ibada ilikuwa nzuri sana kokote utakakoenda kusali na kanisa lolote utakaloingia Ibada zilikuwa na nguvu halisi ya mungu ,hapakuwa na makorombwezo Wala mbwembwe kama Sasa! Huwa navurugwa sana nikiingia kanisani mambo mengi yamebadilika! Kanisa la Sasa imekuwa sehemu ya disco ,dance na mitindo ya hovyo ya mavazi,wanawake wanavaa nguo ambazo hata kwenye baadhi ya bar hawavai na wachungaji wako busy na mapato na matumizi, mahubiri asilimia tisini ni fedha na mipasho ! Nimechoka na miujiza ya zana kama uganga ,kanisa la Leo mchungaji anaamini lazima abebe zana ndio apande madhabahuni ,ukristo unabadilika Kila mwaka ,sura ya kanisa sio Ile ya 1990 ,2000,Kila mwaka kanisa linavaa sura nyingine,wachungaji wetu wanavita kubwa ya kugombea waumini kiasi hawana ushirikiano Tena ! Ni maadui na hawana maombi ya pamoja Tena kama zamani ,Kila mchungaji yaonekana kama ana mbingu ya kwake ,Kuna kundi wanajiita mitume na manabii na Kuna kundi la maaskofu na wachungaji ,maaskofu na wachungaji wanahisi wao nao wanambingu Yao ambayo mitume na manabii hawataenda ! Na mitume na manabii pia wanaona wachungaji na maaskofu hawana nguvu ya mungu Tena! Hizi ni dalili mbaya sana kwa miaka 20 ijayo ya ukristo, mpaka Sasa asilimia 70 waislam wako sawa na unaweza kuwaelewa ! Lakini wakristo wamefeli kabisa , naikubali sana ibada ya hija na Ile ya kuchinja waislamu wanaungana Duniani kote kwa ajili ya Allah! Lugha Yao inakuwa Moja na kauli Yao ni thabiti kabisa ,wanavaa vizuri sana wanapokuwa kwenye ibada na hata ,huwezi kuyaona mapaja ya mwanamke msikitini yakiwa nje sijui kama nitaweza kuuvumilia ukristo kwa miaka michache ijayo mungu aturehemu !
Sasa unasubiri nini? Si uende?
 
Kweli umevurugwa! Maana umeshindwa hata kuweka maelezo yako kwenye aya!!

Anyway, kwa niaba ya rafiki yangu wa damu FaizaFoxy, nakushauri utembelee msikiti uliopo karibu haraka iwezekanavyo ili usilimishwe.

Kulia lia na kulalamika tu hapa jukwaani, hakutakusaidia chochote.
 
Back
Top Bottom