Mimi ni Mkristo mlokole, nimeanza kukosa Imani na ukristo nahisi Uislam ndiyo dini ya kweli

Uko sahihi kabisa baada ya miaka 10 ukristo utakuwa sawa na fiesta.
Ona ibada za siku hizi za akina amsanja vijana wanapenda vitu rahisi rahisi.
Manabii sasa ndio usiseme.
Ukristo unajifia
Upo sahihi sana
 
Huko Vatican walijifungia siku 26 na mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini duniani
Wamekuja na mkakati gani siku zote hizo

Mkakati ni ule ule haujawahi badilika,

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Marko 16:15-16
 
Ulikua mkristo wa kanisa yani wa kujiandikisha namaanisha. Uliwakuta wazazi ni wakristo tu na wewe ukaingia wala hukupata nafasi ya kumtafuta wewe binafsi niseme haukuwa wa kristo wewe. Huyu kristo ukimjua hakuna namna unayodhani unaweza kuachana nae.
 
Tatizo unakwenda kanisani kuangalia watu na vitu hujaenda kumtafuta Mungu na nguvu zake...
Kwani biblia inaposema ninyi ni chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu inamaanisha nini?
 
Nimependa comment hii...

Ukimjua Kristo huwezi kuachana nae...
 
Yesu Hana kanisa ,kanisa linaongozwa na mchungaji Kila muumini ana mchungaji wake ,mchungaji akipotoka kanisa lote linapotoka !
Sio mara zote aisee. Kumbuka alimwambiaje Elia baada ya Elia kukata tamaa na kulalamika Mungu amchukue tu maana Yezebel anaitafuta roho yake? Alimwambia nimejisaazia watu 7000 wasiopiga goti kwa baali. Na walikua kati ya Israel wachafu mno. Kuanzia ndani ya nyumba ya Kifalme.
 
Sasa unasubiri nini? Si uende?
 
Kweli umevurugwa! Maana umeshindwa hata kuweka maelezo yako kwenye aya!!

Anyway, kwa niaba ya rafiki yangu wa damu FaizaFoxy, nakushauri utembelee msikiti uliopo karibu haraka iwezekanavyo ili usilimishwe.

Kulia lia na kulalamika tu hapa jukwaani, hakutakusaidia chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…