Napenda sana ibada, naamini kupitia ibada mambo mengi yanaweza kuwa sawa! Napata shida kidogo na Imani yangu ya ukristo, miaka ya 1980 -1990 ibada ilikuwa nzuri sana kokote utakakoenda kusali na kanisa lolote utakaloingia Ibada zilikuwa na nguvu halisi ya Mungu.
Hapakuwa na makorombwezo Wala mbwembwe kama Sasa! Huwa navurugwa sana nikiingia kanisani mambo mengi yamebadilika! Kanisa la Sasa imekuwa sehemu ya disco,dance na mitindo ya hovyo ya mavazi, wanawake wanavaa nguo ambazo hata kwenye baadhi ya bar hawavai na wachungaji wako busy na mapato na matumizi. Mahubiri asilimia tisini ni fedha na mipasho! Nimechoka na miujiza ya zana kama uganga, kanisa la Leo mchungaji anaamini lazima abebe zana ndio apande madhabahuni ,ukristo unabadilika Kila mwaka ,sura ya kanisa sio Ile ya 1990 ,2000.
Kila mwaka kanisa linavaa sura nyingine, wachungaji wetu wanavita kubwa ya kugombea waumini kiasi hawana ushirikiano Tena ! Ni maadui na hawana maombi ya pamoja Tena kama zamani. Kila mchungaji yaonekana kama ana mbingu ya kwake. Kuna kundi wanajiita mitume na manabii na Kuna kundi la maaskofu na wachungaji ,maaskofu na wachungaji wanahisi wao nao wanambingu Yao ambayo mitume na manabii hawataenda ! Na mitume na manabii pia wanaona wachungaji na maaskofu hawana nguvu ya mungu Tena!
Hizi ni dalili mbaya sana kwa miaka 20 ijayo ya ukristo, mpaka Sasa asilimia 70 waislam wako sawa na unaweza kuwaelewa! Lakini wakristo wamefeli kabisa , naikubali sana ibada ya hija na Ile ya kuchinja waislamu wanaungana Duniani kote kwa ajili ya Allah!
Lugha Yao inakuwa Moja na kauli Yao ni thabiti kabisa ,wanavaa vizuri sana wanapokuwa kwenye ibada na hata ,huwezi kuyaona mapaja ya mwanamke msikitini yakiwa nje sijui kama nitaweza kuuvumilia ukristo kwa miaka michache ijayo mungu aturehemu !
UISLAMU NI NINI?
Maana ya Neno Uislamu Kilugha
Kilugha, Uislamu unamaanisha kujisalimisha, kunyenyekea na kutii. Dini hii ndio inaitwa Uislamu kwa sababu ni dini yenye msingi wa kusalimu amri za Allah na kuzitii.
Maana Yake Kiistilahi
Ni njia ya maisha, mfumo wenye misingi ya imani na matendo ya kuwafanya watu wapate furaha kamili duniani na ahera, iliyotumwa na Allah na kufikishiwa watu kupitia kwa mitume. Uislamu ni sheria ya kiungu inayowaongoza watu wenye akili kuelekea mambo mazuri kulingana na hiari zao.
Yaliyomo katika Uislamu
Maana ya Uislamu ni kujisalimisha: kujisalimsha kwenye amri na makatazo ya Allah. Uislamu hautakuwepo bila ya kujisalimisha kwenye hukumu za Allah.
(Angalia al-An'am, 162 na an-Nisa, 65) Mwanadamu ni mja aliyeumbwa na Allah.
Kwa kuwa Allah amekizingira kila kitu kwa elimu Yake na kwa kuwa Yeye ana hekima, sharti la utumwa ni kujisalimisha Kwake. Sheria za uhai humshurutisha mwanadamu kujisalimisha kwa Allah kwa sababu Allah ndiye anayezijua zaidi sheria hizo na anamjua zaidi mwanadamu.
Ulimwengu na kila kilichomo ndani mwake hutii sheria za Muumbaji huyo. Kwa hivyo, dini ya ulimwengu wote ni Uislamu. Jua, mwezi na nyota, vyote hivyo vinafuata Uislamu. Kwa kuwa Uislamu unamaanisha kumtii Allah na kujisalimisha Kwake, tunaona kwamba viumbe vyote hivyo vinamtii Allah bila ya kuasi. Yaani, tunashuhudia kwamba vinajisalimisha na kwamba vyote vinafuata Uislamu.
“Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumtii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa?" (Aal-i Imran, 3/83)
Katika aya hiyo hapo juu, kujisalimisha kwa viumbe angani na ardhini kumetolewa kama mfano na mwanadamu ameambiwa yafuatayo:
"Ewe Mwanadamu! Jisalimishe kama wao." Kama Ali (ra) anavyosema,
"Uislamu ni utii na kujisalimisha." Mtu asiyejisalimisha kwa Allah hazingatiwi kuwa ni Muislamu. Mtu huzingatiwa kuwa ni mtumwa wa yule anayejisalimisha kwake. Uislamu ni alama na taswira ya imani. Je kujisalimisha bila ya imani, yaani, Uislamu bila ya imani unawezekana? Hata ikiwezekana, haikubaliki. Munafikuna (wanafiki) ni watu wanaojisalimisha bila ya imani. Leo, watu wanaojitambulisha kuwa ni Waislamu huku hawaamini kuwa ni lazima, hao hawajapokea hukumu za Allah kwa moyo na wanafuata itikadi (dini) zingine wanaingia katika kundi hili. Uislamu (kujisalimisha) thabiti, ni lazima kujisalimisha katika Sharia'ah ya Allah bila kusita, kikamilifu na bila ya masharti yoyote.
Kama mtu atajisalimisha kwa Allah kwa hiari yake mwenyewe, na akaishi kama Muislamu kwa kuuchagua Uislamu, ataishi kwa amani na kwa kutangamana na ulimwengu tangu alipojisalimisha kwa yule yule ambaye ulimwengu umejisalimisha kwake. Basi, mtu wa namna hiyo anakuwa mwakilishi wa Allah juu ya ardhi.
UISLAMU NI NINI?
Haiwezekani kufafanua maana ya dini ya Uislamu kwa kifupi bali kwa urefu. Maana yake pana inaweza kufanyika tu kwa ufafanuzi wa Quran na Sunnah kwa sababu yaliyo katika Uislamu na mipaka yake yanabainishwa na Quran na Sunnah. Uislamu unaweza kufundishwa kutoka katika Quran na Sunnah. Allah ameifanya dini hii kuwa kamilifu na pana kwenye vipengele vyote. Hakuna jambo lisilokuwa na ufafanuzi katika Uislamu. Imebainishwa iwapo jambo ni halali, haramu, makruh (lenye kuchukiwa), sunnah, au wajibu; hukumu ya kila tendo au imani imebainishwa. Katka Uislamu kuna hukumu mahususi kuhusu imani, ibada, siasa, masuala ya kijamii, uchumi, vita, amani, sheria na yote yenye kumhusu mwanadamu; au, msingi wa mujtahid kufanya hukumu ni Quran na Sunnah. Allah anaeleza rasilimali hii ya Quran kama ifuatavyo:
“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu." (an-Nahl, 16/89 na pia angalia Yusuf, 111)
Wanazuoni ambao ni Mujtahid huwa wanahukumu masuala ambayo hukumu zake hazikufafanuliwa waziwazi katika Quran na Sunnah kwa kuegemeza maamuzi yao juu ya Quran na Sunnah.
Mtume (s.a.w) aliufafanua Uislamu kwa njia nyingi. Mmojawapo ni huu ufuatao:
"Uislamu umejengwa juu ya kanuni tano: Kushuhudia kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah na kwamba Muhammad (s.a.w) ni Mjumbe Wake, kuswali, kulip zaka, kufanya Hajj na kufunga katika Mwezi wa Ramadhani." (Bukhari, Iman 1; Muislamu, Iman 22; Nasai, Iman 13; Tirmidhi Iman 3)
Hadithi hiyo hapo juu inaeleza kuwa Uislamu una misingi mitano. Tunachotakiwa kuzingatia ni ukweli kuwa misingi hiyo mitano ndiyo nguzo za Uislamu isipokuwa zenyewe peke yake haziundi Uislamu wote. Hatuwezi kusema kuwa nyumba huwa na msingi tu; halikadhalika, si sahihi kusema kuwa Uislamu una kanuni tano tu. Mwenye kusoma Quran ataona kuwa maadili, uchumu, masuala ya kijamii, amani, vita, wema, uovu n.k. ni mambo yaliyotajwa pamoja na kanuni hizo tano katika Quran. Uislamu una msingi na jengo. Msingi una kanuni hizo tano. Jengo lina hukumu zingine za Uislamu zinazohusu maisha ya kibinadamu. Wajibu wa Muislamu ni kuujua Uislamu wote kwa ujumla na kuutekeleza wote kwa ujumla.
Chini ya nuru ya hadithi maarufu hapo juu, tunaweza kugawanya misingi ya Uislamu katika makundi mawili: imani, iliyoelezwa kifupi kwa maneno ya shahada na amali njema, zilizotajwa kama amali nne kutokana na umuhimu. Uislamu ni imani inayoanzia katika kalima ash-shahada (maneno ya shahada) na kanuni za imani. Uislamu ni ibada inayojitokeza pamoja na swala, zakah, saumu na hajj. Hizo zinaitwa kanuni au misingi ya Uislamu. Sehemu zilizosalia za Uislamu ni jengo lililowekwa juu ya misingi hiyo. Mambo yanayounda jengo hilo ni mifumo ya kimaisha ya Uislamu: mfumo wa kisiasa, mfumo wa kiuchumi, mfumo wa kijeshi, mfumo wa kijamii,mfumo wa elimu, n.k. Uislamu pia una vibali ili kuhakikisha mamlaka yake. (Vibali vinamaanisha kwamba ni nguvu ya kuhakikisha kuwa sheria na amri za kimaadili zinatekelezwa; inamaanisha desturi zinazohusu ushurutishaji). Vibali hivyo ni jihad, kuamrisha wema na kukataza uovu, adhabu asilia na adhabu za kiungu anazotoa Allah duniani na ahera. Hivyo, Uislamu ni imani, ibada, mifumo ya kimaisha na vibali.