Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Unataka kusema kua na sisi ni wajomba zao watumie tu bandari yetu huku mazao yetu yasiende kwao,.Kwenye vita ya kiuchumi kila mbinu lazima itumike ili tukubaliane, Trump si unaona matishio yake kwa China?? Na unaona China anavyojibu mapigo?? Malawi lazima tumdhibiti kwa kila mbinu maana tunawaheshimu sana hadi tumewapa sehemu wakawa na "Malawi Cargo". Mheshimiwa Bashe akamatie hapo hapo hadi waje mezani. Yanaongeleka.
 
Sisi ndo tutaathirika kwasababu tutapoteza soko la bidhaa zetu za viwandani, bandari pamoja na malori yetu
Malawi hawawezi vita vya jino kwa jino na Tanzania.
Wanategemea Tanzania kuendesha mambo yao mengi tu.
Nachojua kuna watanzania wengi wamewekeza maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, kuwaondoa wote hao mara moja kutawaletea usumbufu.
Hata hivyo wana hiyari, wakiona inawezekana wawaondoe ili kila mmoja apambane kwake.
 
Kama Malawi wana akili, hivi sasa watakuwa wanajadili mkakati wa kupitisha bidhaa zao zote Beira Mozambique au Durban South Africa, mbaki na bandari yenu mliyotoa kwa Waarabu.

Kumbuka kwa mfano, kinachowazuia Malawi kupitisha magari yao South Africa ni kwa sababu Tanzania tunawaruhusu kutatoa kwa kuyaendesha, na South Africa wanataka yabebwe kama mzigo. Haina maana hawawezi kutumia malori ya kubebeba magari ili yapitie Durban.

Na pia watakuwa na mkakati wa kulianzisha tena sula la mpaka katika ziwa Nyasa, liende Mahakama za Kimataifa
 
Nyie ondokeni mkajifungie ,sisi tutawapelekea wamalawi mizigo yao tena kwa kuzirusha angani...KQCargo!
 
Kajamaa kajinga sana, yeye angebaki kuzungumzia mambo ya wizara yake isitoshe maamuzi kama hayo yanafanywa na rais au baada ya baraza la mawaziri kukutana .
Sasa ameingilia wizara ya mawasiliano, fedha na mambo ya nje.
 
Nime reflect back kwa kilichotutokea tukiwa watoto na hatua alizochukua Bashe dhidi ya Malawi.
Kwa hiyo conclusion ni nini? Mie nahisi Malawi watatafuta njia mbadala, na hata kama itawagharimu zaidi. Watakuwa tayari kuchukua mkopo wa World Bank ili wajenge barabara ndani ya Mozambiqque kupata access ya bandari za Msumbiji. Nakwambia hapa Bashe amekosea sana. Ni sawa angewekwa vikwazo reciprocal kwenye mazao tu, lakini kutumia bandari kama fimbo amefanya jambo la kitoto sana. Na nahisi hata Zambia, DRC wanaweza kujoin forces na Malawi kupata access ya bandari za Mozambique. Kumbuka hadi sasa tunawabembeleza Zambia watumie bandari ya Dar, wao sio lazima, ndio maana hata reli ya TAZARA hawaijali. Usifikiri Bashe anapopiga kelele kama hizi Zambia na DRC hawasikilizi
 
Hakuna urafiki wa hivo
Malawi akubali kuishi na jirani zake vizuri
Tanzania tunanufaika na soko la mazao yetu huko Malawi, Sasa kama ameamua kutaka wakulima wetu zaidi ya 80% wafe, yaani Malawi amejali maslahi yake akaona sisi hatufai
Sasa na sisi tunamnyima nafuu tulizokuwa tunampa za bandari, kutumia barabara zetu Bure, ushuru na kumhakikishia ulinzi na usalama n.k
Akiona vip apite huko Msumbiji mbali na risk ya usalama iliyoko huko atakuwa mwenyewe
Akiona tunafaa atakuja tukae mezani

Haiwezekani uzuie gasi na mafuta ya Russia ambao ndo anategemea kukuza uchumi halafu akuchekee eti kwakuwa wewe ni mteja wa ngano yake, hilo haliwezekani atakufukuza haraka sana
 
Kwa nini unaongea kama vile Malawi kaweka huu mkakatiwa kujitegemea kwa chakula dhidi ya Tanzania peke yake? Kwa mfano, amesema hataki toothpick zitoke nje ya nchi. Badala ya kumsifia na kumuiga sie tupo bize tunaagiza toothpick na pini na sindano toka China!
 
Yaani ni rahisi sana kuona watu wanaobisha wakati hawana exposure ya kutosha kuelewa hivi vitu. Uandishi wako unaakisi hilo.

Kwa hiyo unaona ni sawa kwa wakulima wetu zaidi ya 80% kutegemea soko la Malawi, ni akili hiyo? Na hao wakulima wetu 80% wanaotegemea soko la Malawi, wanatoka wapi hasa, Mbeya, Iringa hadi Musoma?
 
No reforms no election
 
Kwa hili Bashe namsupport 💯
 
Vita Ya Uchumi Ni Mbaya Sana
na kati ya kitu serikali ilitakia kuajiri/kuassign maafisa TISS bora na wengi ni kwenye eneo la uchumi pamoja na ulinzi. ukiona mtandaoni namna watanzania wanavyopata shida kusafirisha malori zambia, inaumiza sana, achana na hiyo malawi tu. tunatakiwa kuwachunguza na kuwawekea mikakati.
 
Kwa hili Bashe namsupport 💯
Sawa, wewe kusupport haibadilishi uamuzi wake kuwa wa busara. Katika dunia ya watu wengi, hata ufanye uamuzi wa kipumbavu namna gani kuna watu watau support kwa nguvu tu - ndio maana kina Idd Amin waliweza kutawala
 
Una tatizo kichwani wewe
Kilimo ndo uti wa mgongo wa Tanzania
Mtu akigusa maslahi ya kilimo na mazao anauwa Watanzania
Hii inakuwa vita kubwa
Nenda Uarabuni uguse Mafuta uone
Nenda Russia uguse gesi na mafuta uone.
Nenda China uguse viwanda uone

Malawi ametukosea sana kuzuia soko na njia ya kupeleka mazao kusini mwa Africa

Na sisi tuna mfungia anachonufaikq nacho cha kwetu hadi aone umuhimu wetu arejee mezani Kwa adabu tuyamalize

laZima tuwafundishe majirani kuheshimu maslahi yetu, hili liwe funzo Kwa majirani wengine kama Rwanda, Zambia, Kenya, DRC, Uganda, Mozambique na wengine

Wajue Tanzania hatuna masiala mjinga akigusa maslahi ya wakulima wetu, tunapambana nae
 
Halaf umekurupuka kusema huu ni msimamo wa Bashe..Je una uhakika Gani kama huu msimamo haujapitishwa na Serikali (cabinet)..na Bashe ni mtoa tamko tu..!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…