Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Na kwa sababu ya yote haya kuwaambia msipitishe vitu vyenu kwenye bandari yetu mkitaka kuvipeleka nje unaona ni sahihi? Tumetangaza vita na Malawi?

Hebu niambie unaona ni jambo la akili kumwambia Malawi umekataa kununua mchele wetu basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe Tanzania?
Ni sahihi sana tu mkuu, tena ilitakiwa hata balozi awe ameshatimuliwa kufika muda huu,....hawa watu wamekuwa wakiwaonea sana hata madereva wa malori ya Tanzania,...muda si mrefu walizuia bodaboda wa bongo kugusa kwao ilihari wao wanafika huku bila wasiwasi wowote,....hao mbwa sio wa kuwahurumia mkuu,....ni WASHENZI sana
 
Mnawajua Wamalawi na Wazambia au mnawasikia Bashe upo sahihi sana ndio vita ya kiuchumi inavyopigana hivyo Hao wamalawi wamesumbua sana kutoa karanga na mahindi kutoka kwao miaka nenda rudi Kuja Tanzania na Kenya ila kupeleka SA hakuna tatizo wala vibali vingi
 
Ikiwa kuna walionielewa katika point kwamba sikatai Bashe kuchukua reciprocal measures kutoruhusu bidhaa za mazao toka Malawi kuingizwa Tanzania kwa ajili ya kuuzwa, basi ni vema sana. Lakini kwa wale ambao mnaona Bashe yuko sahihi kutumia bandari yetu kama fimbo ya kuwachapia Malawi ili kuwalazimisha wanunue mchele na viazi vya Mbeya, natamani ningejua uweo wa elimu zenu. Nachelea nabishana na watu wa vijiweni ambao hawana kazi zaidi ya kubishana kutwa nzima nani zaidi kati ya Yanga na Simba, au Zuchu ni moto zaidi ya Zari. Sina muda wa kupoteza na nyie. Mwenye kunielewa na anielewe
 
nimeishi mpakani na MALAWI kwa miaka mingi sana,....ni watu WAJINGA, WASHENZI, na WAPUMBAVU mnooo,....hao washenzi sio wa kuwahurumia hata kidogo,....pamoja na TANZANIA kutoa msaada mkubwa sana wa chakula Malawi lakini bado wamekuwa watu wenye visirani sana na watanzania bila sababu za msingi,......hao acha wapigwe pini tu 📌📍📍
Acha uongo. Tanzania lini imekuwa ikitoa msaada wa chakula kwa Malawi? Wewe ukienda kununua mchele dukani mwenye duka anakuwa ametoa msaada wa chakula kwa mkeo na watoto wako? Hivi nyie watu mna akili za shule zipi, chekechea?
 
Mkuu anakosea kwa mfano Malawi anapitisha Mahindi na Mchele Tanzania yaende Kenya na Somali kwanini uwazuie?
Sasa Malawi wana bomba lao la Mafuta je napo anawazui wasilete mafuta yao nchini?
Mkuu siku zote ukibip lazima utapigiwa tu
Amefanya hivyo ili waachie/waruhusu mara1
 
Ipo,lakini ni katika kuwavutia watumie bandari yetu. Kumbuk sio lazima watumie bandari yetu. Malawi wanahitaji mkakati mdogo sana kujitoa kutumia bandari ya Dar es Salaam. Wanaweza hata kuamua mradi wa kimkakati wa kujenga barabara kuu kutoka Blantyre hadi Beira Mozambique, ambapo ni karibu sana ukilinganisha na kuja Dar. Wanasema tatizo ni rebels eneo hili. Wanaweza hata kuwa na joint military operation na Mozambique ili kuwasafisha rebels eneo hili.

Kama tuliweka mkakati wa TAZARA ili kuwapa Zambia access ya bandari ya Dar, unafikiri Malawi watashindwa mradi wa kimkakati wa kujipa access ya bandari za Mozambique? Infact wanaweza kumshukuru Bashe kwa kuwaamsha. Angalia ramani hapo chini

View attachment 3307414
Hamna nchi ya kututisha hapa si malawi, zambia, msumbiji wala SA


Tuna kila kitu
 
Ndio nasema, ni watu wasioona mbali ndio wana mawazo kama hayo, ya ki-Trump. Kwa nini uwazuie katika mikakati yao ya kujitegemea kwa chakula? Mbona tunamshangilia Traole anaposema anataka Burkina Faso ijitegemee kwa chakula, na tunalaani Malawi wakichukua hatua hizo na kuwanyima access ya bandari yetu ili waendelee kututegemea kwa chakula? Sisi ni wanafiki sana basi. Traole safi sana, Malawi hapana, na tunaimba nyimbo za kujitegemea kwa chakula, eeeh!
Tumsifu Bashe anaposema na sii tusiruhusu rasilimali zetu zichezewe na malawi
 
Binafsi Mimi naona Bashe Yuko sawa
Haiwezekani Malawi anufaike na rasimali zetu kama bandari, miundo mbinu na soko halafu sisi atunyime soko la bidhaa na njia za kusafirisha bidhaa za TANZANIA kwenda kusaini mwa Africa
Huyo tunakufa nae kila mtu abakinna chake
Angezuia nao kuuza bidhaa Tanzania. Bandari hawaitumii bure... Tanzania inahitaji nchi kibao zitumie bandari yetu. Sasa tukianza itumie kama fimbo watu watatafuta alternative.
Mimi sioni sababu ya kuitumia bandari katika hili ukizingatia kwanza hizo tariff hazikuilemga Tanzania peke yake tuseme wanatukomoa, ni zuia la nchi zote. Hivyo nasi angezuia bidhaa zao kuuzwa kwetu.
 
Mnawajua Wamalawi na Wazambia au mnawasikia Bashe upo sahihi sana ndio vita ya kiuchumi inavyopigana hivyo Hao wamalawi wamesumbua sana kutoa karanga na mahindi kutoka kwao miaka nenda rudi Kuja Tanzania na Kenya ila kupeleka SA hakuna tatizo wala vibali vingi
a) Malawi buys $48 million Grain from UAE per year. Tanzania next door produces Grain

b) Angola buys $57 million Fish from Argentina per year. Namibia next door is largest fish producer

We can have $32 billion rotating SADC economies per year. But we don’t trust each other !!!
 
a) Malawi buys $48 million Grain from UAE per year. Tanzania next door produces Grain

b) Angola buys $57 million Fish from Argentina per year. Namibia next door is largest fish producer


We can have $32 billion rotating SADC economies per year. But we don’t trust each other !!!
Kasome pia kuwa mwaka 2023 Tanzania iliimport mchele wenye thamni ys usd 83 milioni. Huu ni zaidi ya malawi. Sasa kama wazalishaji tuna import kwanini ushangae malawi kuimport?
Unaweza kuwa unazalisha aina hii ukaimport mchele wa aina nyingine ambao huzalishi. Labda hata hizo grain walizoimport si zile tunazozalisha mfano basmat.
 
Mihemko tu inamsumbua Bashe.
SHIFTA kisha haribu mabilioni ya shilingi kwenye mashamba ya vijana alioanzisha bila upembuzi yakinifu, sasa anatafuta njia ya kutokea ili asiwajibike. Hizo hela walizozichoma Samia alikwenda kukopa African Development Bank na ni Sehemu ya deni letu la nje.
 
Tanzania inaonekana hatuna sera ya mambo ya nje, tupo tupo tu. Lakini hata hivyo, kauli za Bashe kwa Malawi juu ya Malawi kuzuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio ya kiungwana, na haiakisi -Utanzania tulio nao.

Tukio liko hivi, katika kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni na kukuza kilimo ndani ya nchi, Malawi imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kuzalishwa Malawi. Bidhaa hizi ni pamoja na mchele, unga, tangawizi, maji ya kunywa ya chupa, nk, ambavyo vingi vinatoka Tanzania.

Bashe, waziri wa Kilimo, amewajibu Malawi kwamba kwa kuwa wamefanya hivyo basi na Tanzania inazuia bidhaa zote za kilimo toka Malawi kuingia Tanzania.

Sasa kama Bashe angeishia hapo isingekuwa Tatizo, kwa kuwa angeweza kusema ni reciprocal arrangement, na sie tunalinda bidhaa za ndani na kukuza kilimo ndani ya nchi. Hata hivo lazima utumie busara, ili usiumize wananchi kwa mihemuko ya kulipiza kisasi

Lakini Bashe kaenda mbali zaidi, akasema,

2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.

3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.

Sasa najiuliza
  1. Suala la Malawi kupitisha Mazao yake bandari ya Dar es Salaam kwenda nje linahusiana nini na wao kusema wanazuia kuagiza bidhaa za kilimo toka nje? Huku si kukomoana tu kwa makusudi?
  2. Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, kwa nini? Mbolea inasafirishwa kwenda Malawi kama wanavyosafirisha bidhaa nyingine kwa kutumia bandari ya Tanzania, ambayo sisi tunataka waitumie kwa sababu ni huduma wanalipia. Sasa leo tunawakomoa Malawi kuwanyima matumizi ya bandari kwa sababu tu wanataka ku-promote uzalishaji wa kilimo ndani ya nchi yao?
Ikumbukwe kwamba, Malawi imezuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio tu toka Tanzania, bali kwa nchi zote kutia ndani South Afrika, Zimbabwe nk. Sasa kwa nini tunawaingilia? Kwa mfano, sisi Tanzania tunaruhusu uingizaji wa maji ya kunywa ya chupa? Kama hapana, kwa nini?

Sasa unafanyaje uamuzi kwa Malawi, kwamba kama hununui mchele wetu wa Mbeya, basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe kwenye bandari yetu. Ni akili hiyo ya kiwango cha waziri?

Tunaposema Tanzania ina sera ya Ujamaa na Kujitegemea -japo sijui kama bado ipo - kujitegemea tuna maanisha nini? Tunawaadhibu Malawi kutimia bandari yetu kwa sababu wanataka kujitegemea katika bidhaa za kilimo? Mbona hata sisi Tanzania kuna wakati, ili kukuza sekta fulani fulani, tunadhibiti uingizaji wa bidhaa fulani toka nje, kwa iwe nongwa kwa Wamalawi?

Kwanza haya matamshi ya Bashe sio mambo ya wizara yake; wanaohusika ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Mambo ya Nje, sasa kimbelembele cha nini, kumshawishi Raisi Samia kwamba yeye ni tough guy?

Mimi naona katika hili Bashe amekosa busara kabisa - ame-overreact. Raisi Samia awaombe msamaha Malawi kwa kauli hizi za Bashe. Labda pia maamuzi haya ya Bashe yatakuwa na baraka za Raisi Samia. Kama ni hivyo, hivi tuseme Tanzania tumekaa tukatafakari tukaona msimamo kama huu ni wa hekima kweli? Niiteni mhaini, lakini kuna maamuzi mengine mnafanya kama viongozi yatatutia aibu.
Bashe yuko sahihi...hio ndio vita ya kiuchumi. Win win situation. Hawezekqni wewe ufaidikee kwangu...alafu wewe utaki mimi nifaidikee. Bashe ongeza moto wale jamaa ni landlocked country. Mbaka wasema maji ni mmaaa
 
Inasikitisha Waafrika tunafarakana huku Wachina tunawaachia kila kitu na kila mahali.
 
Bashe huwa anajitahidi sana kwenye wizara yake ila kwahili sina hakika maana wao ndowalioenda shule lakini mimi nangumbaru yangu niliyopata kwa walimu waupe nafikiri kama taifa tungeangalia faida tunapopata wanatumia bandari yetu ushuru wabarabara madereva wanaotumia barabara wanatuungisha bidhaa mbalimbali humo barabarani mama lishe nk wangetumia takwimu yapesa tunayotoa na kuingiza toka huko napia tz tujifunze kulinda bidha zetu tuagize tusivokuwa navyo
 
Watumie wapi kwingine ? Hv raman ya Malawi huijui? Msumbiji kaskazin kunq vita na ndo njia fupi kwa Malawi

Pia kenya atazunguka sana , so Malawi hana namna labda aanze tumia ndege

Namuunga mikono Bashe kwenye hili , hakuna kucheka na Kima
Kuna mizigo inatoka south africa inakuja tanzania kupitia tunduma, kua malawi ashindwe kutumia south africa!!? Si maamuzi tu na kuamua!!?
 
1744964732617.png


Niko tayari kuwa Mtanzania pekee anaepingana na serikali, na hata kuitwa mhaini, kupinga kitendo cha Tanzania kutumia bandari kama fimbo dhidi ya Malawi. Kutoa msimamo kwamba hata Malawi wakitaka kusafirisha bidhaa zao za kilimo kwanda nchi za nje, au kuingiza mbolea toka nje, hawataruhusiwa kutumia bandari yetu hadi waruhusu Wanyakyusa wa Mbeya wawauzie mchele, ni jambo la kijinga sijapata kuona katika geopolitics. Na mbaya zaidi kwamba hawaruhusiwi kununua mbolea Tanzania au kuipitisha Tanzania wakiinunua nje.

Na kwa nini Tanzania inataka kuji-limit kwenye soko moja tu la Malawi? Viongozi wanashindwa kuwatafutia masoko wakulima Watanzania kwa hiyo sasa wanawadanganya mbaya wao ni Malawi. Hiyo ni saikoloji ya watu wasio na uwezo wa kuongoza. Kuna masoko mengi na makubwa ya mchele na tangawizi vya Tanzania kuliko Malawi. Kwanza Malawi hapa wanatusaidia indirectly. Why do you want to put all your eggs in one market basket called Malawi? Bashe asiwe mvivu, atafute masoko mbadala, achana na Malawi. Alijisahau sana juu ya hili na haya ndio matokeo. Mbaya wa wakulima hapa ni Bashe na serikali, sio Malawi.

Kama sera ya malawi juu ya jambo hili ingekuwa imelengwa Tanzania peke yake, hapo ningemwelewa Bashe. Lakini kama Malawi amechukua hatua hizi kwa nchi zote, kwa nini Tanzania ndio tuwe mstari wa mbele kumwadhibu Malawi? Na kama anachofanya Malawi kinaathiri nchi za SADC ka South Africa, Zambia, Zimbabwe nk, basi Tanzania ilipaswa kulipeleka suala hili kwenye mkutano husika wa SADC, badala ya kulifanya ni vita binafsi kati ya Tanzania na Malawi, na hasa ukizingatia suala hili linahusu wizara ya biashara na viwanda na mambo ya nje. Huo ni upofu na kukosa busara kwa viongozi wetu.

Kwa nini jambo hili linakuwa gumu kuelewa kwa wengi wenu? Wote mna akili kama za Bashe?
 
Acha uongo. Tanzania lini imekuwa ikitoa msaada wa chakula kwa Malawi? Wewe ukienda kununua mchele dukani mwenye duka anakuwa ametoa msaada wa chakula kwa kwa mkeo na watoto wako? Hivi nyie watu mna akili za shule zipi, chekechea?
MALAWI ilipokumbwa na dhoruba na kimbunga mwaka juzi ni nani alitoa msaada mkubwa wa chakula kuliko Tanzania, kwa nchi zinazoizunguka?.......kama wewe ni mmalawi tuliza matako,...pitishine mbolea kwenye bandari yenu,...bado mafuta nayo tutawapiga stop mbwa nyinyi,...
 
Mnawajua Wamalawi na Wazambia au mnawasikia Bashe upo sahihi sana ndio vita ya kiuchumi inavyopigana hivyo Hao wamalawi wamesumbua sana kutoa karanga na mahindi kutoka kwao miaka nenda rudi Kuja Tanzania na Kenya ila kupeleka SA hakuna tatizo wala vibali vingi
wa Malawi na Zambia hawafikirii kwa kutumia ubongo, nadhani kuna kiungo kingine wanachotumia kufikiri,......hawa watu ni watu wa shari shari tu ,..ni wavivu na wajinga ajabu,...spana waliyopigwa haiwatoshi mbwa hao....
 
Back
Top Bottom