Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Unataka kusema kua na sisi ni wajomba zao watumie tu bandari yetu huku mazao yetu yasiende kwao,.Kwenye vita ya kiuchumi kila mbinu lazima itumike ili tukubaliane, Trump si unaona matishio yake kwa China?? Na unaona China anavyojibu mapigo?? Malawi lazima tumdhibiti kwa kila mbinu maana tunawaheshimu sana hadi tumewapa sehemu wakawa na "Malawi Cargo". Mheshimiwa Bashe akamatie hapo hapo hadi waje mezani. Yanaongeleka.
Hivi mkuu tujiulze tuu kwamb ikitokea budhaa zetu kadhaa zikazuiliwa RDC, Rwanda na uganda kwasabab zao ila zisizo za shari just kuimarisha masoko yao ya ndani hivi tunaweza wazuia na wao bidhaa zao zisipite mzizima port? Kama tulivyofanya huko Kwa Kamuzu Banda??
 
Wadau naomba kuelimishwa.
Hivi kama tz tunategemea(import) zao flani labda mahind na ngano kutoka kenya.
Halaf ikatokea kenya ikapiga marufuku watu wake kuuza mahindi na ngano nje ya nchi je, hilo linaweza kuwa na madhara sawa na ambavyo nasis tunaweza kuzuiwa bidhaa zetu kuuzwa nje ya nchi kama hii isue ya malawi na tanzania??
 
Hawa waseng3 malawi si ndo walisema ziwa nyasa ni lao 100%? Safi Bashe wabane pumb.u hao hadi watoke damu.
 
Kwamba mazao yao wakipitisha kwenye Bandari yao hawatulipi ?!!!!!

Ni sawasawa mke wako anakunyima chakula wewe unataka kumyima unyumba to whose benefit ?!!!!

Dunia hii ishakuwa ya kipuuzi, As a Globalist speaking, its very Sad...
 
Hivi mkuu tujiulze tuu kwamb ikitokea budhaa zetu kadhaa zikazuiliwa RDC, Rwanda na uganda kwasabab zao ila zisizo za shari just kuimarisha masoko yao ya ndani hivi tunaweza wazuia na wao bidhaa zao zisipite mzizima port? Kama tulivyofanya huko Kwa Kamuzu Banda??
Kuzuia exports ni tofauti kidogo na kuzuia imports. Kenya wakipiga marufuku bidhaa zao kuuzwa Tanzania huwa haina shari kama kupiga marufuku bidhaa za Tanzania kuingia Kenya.

Kuna wakati Kenya walipiga marufuku mahindi ya Tanzania kwenda Kenya, tulikuja juu sana, lakini tulichofanya ni kupiga marufuku maziwa ya Kenya kuja Tanzania, hadi ikabidi tukae mezani.

Angalia kwamba kujibizana kunatakiwa kuwe katika eneo moja, sio Kenya wapige marufuku mahindi ya Uganda kuingia Kenya halafu Uganda wapige marufuku gari za kutoka Kenya kwenda Rwanda kupitia Uganda kwa sababu Kenya hawataki kununua mahindi yao. Hapo sio haki.
 
Kuzuia exports ni tofauti kidogo na kuzuia imports. Kenya wakipiga marufuku bidhaa zao kuuzwa Tanzania huwa haina shari kama kupiga marufuku bidhaa za Tanzania kuingia Kenya.

Kuna wakati Kenya walipiga marufuku mahindi ya Tanzania kwenda Kenya, tulikuja juu sana, lakini tulichofanya ni kupiga marufuku maziwa ya Kenya kuja Tanzania, hadi ikabidi tuake mezani.

Angalia kwamba kujibizana kunatakiwa kuwe katika eneo moja, sio Kenya wapige marufuku mahindi ya Uganda kuingia Kenya halafu Uganda wapige marufuku gari za kutoka Kenya kwenda Rwanda kupitia Uganda kwa sababu Kenya hawataki kununua mahindi yao. Hapo sio haki.
Hapo mkuu nmekuoata barabara.
 
Tanzania inaonekana hatuna sera ya mambo ya nje, tupo tupo tu. Lakini hata hivyo, kauli za Bashe kwa Malawi juu ya Malawi kuzuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio ya kiungwana, na haiakisi -Utanzania tulio nao.

Tukio liko hivi, katika kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni na kukuza kilimo ndani ya nchi, Malawi imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kuzalishwa Malawi. Bidhaa hizi ni pamoja na mchele, unga, tangawizi, maji ya kunywa ya chupa, nk, ambavyo vingi vinatoka Tanzania.

Bashe, waziri wa Kilimo, amewajibu Malawi kwamba kwa kuwa wamefanya hivyo basi na Tanzania inazuia bidhaa zote za kilimo toka Malawi kuingia Tanzania.

Sasa kama Bashe angeishia hapo isingekuwa Tatizo, kwa kuwa angeweza kusema ni reciprocal arrangement, na sie tunalinda bidhaa za ndani na kukuza kilimo ndani ya nchi. Hata hivo lazima utumie busara, ili usiumize wananchi kwa mihemuko ya kulipiza kisasi

Lakini Bashe kaenda mbali zaidi, akasema,

2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.

3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.

Sasa najiuliza
  1. Suala la Malawi kupitisha Mazao yake bandari ya Dar es Salaam kwenda nje linahusiana nini na wao kusema wanazuia kuagiza bidhaa za kilimo toka nje? Huku si kukomoana tu kwa makusudi?
  2. Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, kwa nini? Mbolea inasafirishwa kwenda Malawi kama wanavyosafirisha bidhaa nyingine kwa kutumia bandari ya Tanzania, ambayo sisi tunataka waitumie kwa sababu ni huduma wanalipia. Sasa leo tunawakomoa Malawi kuwanyima matumizi ya bandari kwa sababu tu wanataka ku-promote uzalishaji wa kilimo ndani ya nchi yao?
Ikumbukwe kwamba, Malawi imezuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio tu toka Tanzania, bali kwa nchi zote kutia ndani South Afrika, Zimbabwe nk. Sasa kwa nini tunawaingilia? Kwa mfano, sisi Tanzania tunaruhusu uingizaji wa maji ya kunywa ya chupa? Kama hapana, kwa nini?

Sasa unafanyaje uamuzi kwa Malawi, kwamba kama hununui mchele wetu wa Mbeya, basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe kwenye bandari yetu. Ni akili hiyo ya kiwango cha waziri?

Tunaposema Tanzania ina sera ya Ujamaa na Kujitegemea -japo sijui kama bado ipo - kujitegemea tuna maanisha nini? Tunawaadhibu Malawi kutimia bandari yetu kwa sababu wanataka kujitegemea katika bidhaa za kilimo? Mbona hata sisi Tanzania kuna wakati, ili kukuza sekta fulani fulani, tunadhibiti uingizaji wa bidhaa fulani toka nje, kwa iwe nongwa kwa Wamalawi?

Kwanza haya matamshi ya Bashe sio mambo ya wizara yake; wanaohusika ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Mambo ya Nje, sasa kimbelembele cha nini, kumshawishi Raisi Samia kwamba yeye ni tough guy?

Mimi naona katika hili Bashe amekosa busara kabisa - ame-overreact. Raisi Samia awaombe msamaha Malawi kwa kauli hizi za Bashe. Labda pia maamuzi haya ya Bashe yatakuwa na baraka za Raisi Samia. Kama ni hivyo, hivi tuseme Tanzania tumekaa tukatafakari tukaona msimamo kama huu ni wa hekima kweli? Niiteni mhaini, lakini kuna maamuzi mengine mnafanya kama viongozi yatatutia aibu.
Hii itaathiri Imani katika nchi za jirani kutegemea babdari na Barbara zetu kuputishia bidhaa zao.
 
Ikiwa kuna walionielewa katika point kwamba sikatai Bashe kuchukua reciprocal measures kutoruhusu bidhaa za mazao toka Malawi kuingizwa Tanzania kwa ajili ya kuuzwa, basi ni vema sana. Lakini kwa wale ambao mnaona Bashe yuko sahihi kutumia bandari yetu kama fimbo ya kuwachapia Malawi ili kuwalazimisha wanunue mchele na viazi vya Mbeya, natamani ningejua uweo wa elimu zenu. Nachelea nabishana na watu wa vijiweni ambao hawana kazi zaidi ya kubishana kutwa nzima nani zaidi kati ya Yanga na Simba, au Zuchu ni moto zaidi ya Zari. Sina muda wa kupoteza na nyie. Mwenye kunielewa na anielewe
Ukisoma hii utagundua kuwa uwezo wako ndio mdogo. Soma uone wamalawi wenyewe wanasema je
Screenshot_20250418-231346.jpg
 
Jana nimeona akihojiwa alietoa tamko huko Lilongwe na Waandishi wa habari hakuna cha maana alichokua anaongea zaidi ya kulalamika tu Bashe wapige spana hao washazoea kutunyanyasa bila sababu za msingi.
 
Ukisoma hii utagundua kuwa uwezo wako ndio mdogo. Soma uone wamalawi wenyewe wanasema je
Nikisoma hapo nagundua wewe ndio uwezo wako ni mdogo sana. Hakuna sehemu nimesema Tanzania haipaswi kuchukua hatua reciprocal katika suala la kuzuia mazao ya Malawi kuuzwa nchini Tanzania. Nimelaani kuwazuia access ya bandari kwa ajili ya hili suala. Umesoma shule gani wewe mzito kusoma na kuelewa kiasi hiki?

Na pia hiyo cutting uliyoweka hapo ni maoni ya mtu, sio response ya serikali ya Malawi. Mie naongelea hatua za Bashe kama mwakilishi wa serikali. Nipe response ya serikali ya Malawi, sio mwandishi wa gazeti la Times la Malawi.

Ni sawa na CCM kusema kama Chadema hawataki ku-sign kanuni za uchaguzi ili washiriki uchaguzi basi wakatieni umeme na maji wenye ofisi zao hadi wakubali kutia sahihi, halafu malofa kama wewe mshangilie amri kama hiyo toka kwa Samia.
 
Hii itaathiri Imani katika nchi za jirani kutegemea babdari na Barbara zetu kuputishia bidhaa zao.
Wewe umenielewa sana! Hata kama Tanzania atafanikisha lengo lake katika hili, kovu la hiki kidonda halitasahaulika kamwe na hizo nchi. Bashe amekosea sana, na kama ni Samia kamuagiza ameharibu sana.
 
Nikisoma hapo nagundua wewe ndio uwezo wako ni mdogo sana. Hakuna sehemu nimesema Tanzania haipaswi kuchukua hatua reciprocal katika suala la kuzuia mazao ya Malawi kuuzwa nchini Tanzania. Nimelaani kuwazuia access ya bandari kwa ajili ya hili suala. Umesoma shule gani wewe mzito kusoma na kuelewa kiasi hiki?

Na pia hiyo cutting uliyoweka hapo ni maoni ya mtu, sio response ya serikali ya Malawi. Mie naongelea hatua za Bashe kama mwakilishi wa serikali. Nipe response ya serikali ya Malawi, sio mwandishi wa gazeti la Times la Malawi.

Ni sawa na CCM kusema kama Chadema hawataki ku-sign kanuni za uchaguzi ili washiriki uchaguzi basi wakatieni umeme na maji wenye ofisi zao hadi wakubali kutia sahihi, halafu malofa kama wewe mshangilie amri kama hiyo toka kwa Samia.
Hukuangalia athari hasi za wakulima wetu na wafanyabiashara wetu walizopata juu ya msimamo wa Malawi?

Kwa sababu hili ni suala la kulinda maslahi ya kiichumi...
 
Hukuangalia athari hasi za wakulima wetu na wafanyabiashara wetu walizopata juu ya msimamo wa Malawi?

Kwa sababu hili ni suala la kulinda maslahi ya kiichumi...
Bado haujaelewa thread. Umeisoma au umesoma title tu? Hizo athari nazielewa na kuzikubali.

Kuna mahali nimetoa mfano, kwamba ni sawa na CCM kusema kama Chadema hawataki ku-sign kanuni za uchaguzi ili washiriki uchaguzi basi wakatieni umeme na maji wenye ofisi zao hadi wakubali kutia sahihi

Tanzania hatupaswi kutumia blackmail katika negotiations, only primitive and uncultured people will resort to that. Tunatakiwa tutumie reciprocation.
 
Uelewa wake ndio mdogo kwenye haya mambo
Kama wewe ni msomi mwenye uelewa zaidi yangu, tafakali juu ya hii kauli yangu hapa, "Tanzania hatupaswi kutumia blackmail katika negotiations, only primitive and uncultured people will resort to that. Tunatakiwa tutumie reciprocation"

La sivyo wewe na hao ninaowasema ni primitive and uncultured.
 
Baraza la Mawaziri lilitakiwa likae kujadili sakata la Malawi.
Waziri amekurupuka.
Rais anyooshe ashike kalamu yake haraka kubadili hali hii
 
Wamalawi wanadai wao wanafaidika zaidi na Tanzania kuliko Tanzania pana kipindi walikamata karanga iliyokua inatoka mpakani Isongole bila sababu zilichukua muda kuachiwa hawa jamaa sijui ability zao wanafikiri nini?
sa hivi wanalia tu
 
Nikisoma hapo nagundua wewe ndio uwezo wako ni mdogo sana. Hakuna sehemu nimesema Tanzania haipaswi kuchukua hatua reciprocal katika suala la kuzuia mazao ya Malawi kuuzwa nchini Tanzania. Nimelaani kuwazuia access ya bandari kwa ajili ya hili suala. Umesoma shule gani wewe mzito kusoma na kuelewa kiasi hiki?

Na pia hiyo cutting uliyoweka hapo ni maoni ya mtu, sio response ya serikali ya Malawi. Mie naongelea hatua za Bashe kama mwakilishi wa serikali. Nipe response ya serikali ya Malawi, sio mwandishi wa gazeti la Times la Malawi.

Ni sawa na CCM kusema kama Chadema hawataki ku-sign kanuni za uchaguzi ili washiriki uchaguzi basi wakatieni umeme na maji wenye ofisi zao hadi wakubali kutia sahihi, halafu malofa kama wewe mshangilie amri kama hiyo toka kwa Samia.
Kubishana na wajinga kama wewe kwenye mabo yanayokudi nitakuwa najichosha. FYI Malawi wanataka kukaa mezani kuyamaliza na waziri wao wabishara kaisha sema hilo.
 
Back
Top Bottom