Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Dunia imekengeuka.., wafuatiliaji wa Historia hili sio jipya Mercantilism used to be a thing hapo zamani (lakini matokeo hayakuwa mazuri) kama kweli wana-excess ya mazao, wana hoja ya kupunguza uagizaji ila comparative advantage itakuonyesha kwamba kila mtu kununua kile ambacho mwingine anaweza kuzalisha kwa gharama nafuu na ubora ndio akili (zaidi ya hapo unatesa mpaka watu wako mwenyewe)

 
Tupo nyakati tofauti kabisa. Ni nyakati za Ubaya Ubwela tu. Ameanza Marekani ikaja China sasa ni Malawi na Tanzania.
 
Bashe kazia hapo hapo baba mpaka watoe mlio, we ungekuwa unauza mazao malawi ungemuelewa waziri wa kilimo
 
Bashe kazia hapo hapo baba mpaka watoe mlio, we ungekuwa unauza mazao malawi ungemuelewa waziri wa kilimo
Ngoja tuiweke hii katika scale ndogo labda itawasaidia kuelewa enyi wenye changamoto za kuelewa mambo.

Wewe una genge, jirani yako ana duka. Kwa hiyo ukiwa na jirani yako unamuuzia nyanya na wewe unanunua soda kwake, siku akisema anaacha kununua nyanya kwako ni ugomvi? NI akili kumlazimisha kununua nyanya kwako ikiwa amesema anataka kulima nyanya zake wenyewe? Na ndio utamwambia kwa kuwa mimi nina gari hata lift yangu hupandi tena hadi ukubali kuendelea kununua nyanya kwangu?

Na unasema tena sitaki tena kukuruhusu kukodisha gari yangu kuleta bidhaa zako dukani kwako, hadi uendelee kununua nyanya kwangu.

Kumbuka, hakuna makubaliano yoyote rasmi kwamba atanunua nyanya kwako ili wewe ununue soda kwake.

Sasa sema, katika scale hii, unaona wewe ni muungwana?
 
Naunga mkono maamuzi ya Bashe. Malawi haiwezi ghafla kuwa self sustained, kuna kila possibly wanapokea bidhaa hizo kutoka kwenye other sources ie- Zimbabwe, South Africa. Juzijuzi walipata mafuriko wakawa hawana chakula tukawapelekea misaada including chakula. Leo hii wamelima wapi to the point of being self sustained? Kuna harufu ya corruption na desperation ya SA kutafuta masoko ya bidhaa zake nje ya nchi baada ya kupigwa spana na Trump
 
Malawi hawahitaji kuweka sera hii kama hizi ndio sababu, kwa sababu market forces zingefanya wanunuzi wa Malawi wageukie SA kwenye bidhaa rahisi zaidi, kama kweli SA wanazo za ziada na Malawi anaziona kama alternative source. Serikali ya Malawi haiwezi kuwalazimisha wafanya biashara wake kununua mchele Tanzania kama upo wa bei poa SA. After all, SA haina mchele wala tangawizi ya kuwauzia Malawi, wala Zimbabwe. Malawi wana ardhi yao inayofaa kwa kulima mpunga.

Kwa hiyo point yako haina mshiko

Hatuna mkataba rasmi wa kuwauzia Malawi tangawizi mchele nk kiasi kwamba tuwalaumu kwa kukiuka mkataba
 
Tupo nyakati tofauti kabisa. Ni nyakati za Ubaya Ubwela tu. Ameanza Marekani ikaja China sasa ni Malawi na Tanzania.

2 Timotheo 3:1-5 SRUV​

Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wakaidi, wenye kujivuna
 
Unataka watu wa Mbeya wakauze wapi mchele wao ? Naichukia ccmu ila Malawi kweny hili sipo nao , Malawi wawekeze kweny kilimo na kuboresha miundo mbinu yao ila kuzuia watu kufanya biashara haiez kuza kilimo chao
 
Kweli usisikilize tatizo kwa upande mmoja, kwa jinsi alivyo announce bashe kwa watanzania ni as if kuna booooonge la msala na katoa kauli za kimakakamavu sana, tutakuja kususi hilo libandari, watu watumie huduma sehemu nyingine
 
Unataka watu wa Mbeya wakauze wap mchele wao ? Hv una maslai gan na Malawi , imagine jirani yako anazuia watu wake kuja kununua vitu dukani kwako utakubali bidhaa zikuharibikie kisa unataka uonekane mwema ?

CCM ni mbovu ilq tusijitoe akili , sehem kama hz ndo ccmu hutumia kuwafanya wapinzan wakose sapoti kwa wananchi

Tujifunze kuchanga karata vzr , kwa hili Bashe yupo sahihi , lzm uhakikishe kwako wanakula iwe kila namna na sio kujifanya mwema wkt kwako wanaenda umia
Bashe anataka kujifanya Trump wa Tanzania, lakini kama akili ya serikali ya Raisi Samia ndio hii na ndio inayotoa maamuzi kama mikataba ya bandari, basi Tanzania ni nchi ya kuhurumiwa sana
 
Kweli usisikilize tatizo kwa upande mmoja, kwa jinsi alivyo announce bashe kwa watanzania ni as if kuna booooonge la msala na katoa kauli za kimakakamavu sana, tutakuja kususi hilo libandari, watu watumie huduma sehemu nyingine
Watumie wapi kwingine ? Hv raman ya Malawi huijui? Msumbiji kaskazin kunq vita na ndo njia fupi kwa Malawi

Pia kenya atazunguka sana , so Malawi hana namna labda aanze tumia ndege

Namuunga mikono Bashe kwenye hili , hakuna kucheka na Kima
 
Hapo juu umesema wewe ni mtanzania lakini kadiri mjadala unavyoendelea unaonyesha uhalisia wako.
Vitu vingi hapa unavieleza kwa hisia, kwamba uamuzi wa mh Hussein Bashe umekuumiza mno.
Hujaumizwa na usitishwaji bidhaa za kilimo kutoka Tanzania kuingizwa Malawi.

Kwamba watarudisha mgogoro wa Ziwa Nyasa, waambie waurudishe, tutakabiliana nao kwa namna watavyokuja.
 
Kuwaiondoa lebels unadhani ni suala rahisi?
 
Ahsante Kwa maoni yako! Endelea kufanya upembuzi zaidi, inawezekana wewe ni mzalendo haswa lkn bado ninamashaka na misimamo yako!
 
Nilitegemea hilo suala kwa kuwa linagusa wizara tofauti tofauti basi lizungumzwe na wazir mkuu.
 
Usikute safari ina karibia kufika mwisho, watu wana mzoom tu 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…