HOJA Mimi ni mwajiriwa Serikalini. Nilikopa, ila nimefeli malengo nahisi ninaenda kupotea

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Usikope tena mkuu, komaa na hiyo laki nne mpaka mtaji unapatikana.
 
watu wapewe elimu ya mikopo
au watafute ilmu hio kwenye internet wajue outcome yake kabla hawajaingia kwenye trap
Nina experience na mikopo mkuu Hizi biashara zetu bila kuziboost kwa mikopo haziinuki leo wala kesho. Inshort nilichojifunza katika mikopo. Bank zenyewe ni wanyonyaji wakubwa riba ni kubwa kupita maelezo. Elimu ya mikopo watu hawana kabisa Mkopo ukiingia mtu anamega kiasi kidogo akale kwanza bata hiyo nyingine ndio ijizungushe iongezeke, hakuna mistake mbaya kama hiyo UMAKINI ndio Kila Kitu Unatakiwa Uwe Mchumi kwelikweli na walivyo washenzi ukirudisha hela yao bila shida wanakubembeleza uchukue mwingine na offer juu! Sasa Jichanganye Utaimba Halleluya
 
Jamaa asome hapa aelewe
 
Inategrmeana unaishia wapi hiyo Laki tatu inayobaki kwa Mke na Mtoto mmoja inawatosha kwa matumizi ya Chakula, Bill za maji na umeme.

Jambo Lingine ktk hizo 8M chukua Bodaboda itakusadia kwenye biashara zako utakoa gharama pia usiwe na wasi wasi ukiwa na muda wa ziada gonga Vichwa vya bodaboda
 
Usijinene mabaya

Hakuna mtu ambaye hana Mkopo, usiogope kukopa.

Kunywa pombe kupindukia huko do utafeli achana na masuala ya Pombe.

Lima yanapofika Masika, huwezi kufeli kila mwaka, kuna mwaka utafaulu tu.

Hela yote ya mkopo haiwekwi kwenye Biashara moja.

Karibu mtaani
 
Utaniwia radhi mkuu.
Adui yako wa kwanza ni kutaka kuishi maisha yasio yako(nje ya kipato chako)

Pili ni mke wako(huyo anaweza kuwa kirusi na nguzo ya kukushusha chini usipojipambanua kama mwanaume)

Tatu ni anasa(pombe) hii ushawishi wake mkubwa upo kwa watu unaokuwa nao, nayo hupelekea pia kuishi nje ya kipato chako kwenye mambo ya kununuliana na kuchafua meza ilihali una mambo chungumzima hujayakamilisha.

Ziada, chunga sana tena chunga zaidi huyo mkeo anaweza kuwa chanzo cha anguko lako( kwa maelezo yako anaonekana ni mtu wa kutrend kila toleo la kitu anataka awe nalo ilihali kipato chenu hakiruhusu kuishi kwa trend).

#Hallelujah!!!
 
Kama umeshajitambua kuwa ulevi utakupoteza badilika

Ingekuwa hujajitambua ndio kungekuwa tatizo na tungekushauri...maamuzi ni yako

Wacha Pombe,pambania familia
Alikopa Pesa nyingi akiwa hanywi, ikapotea. Sasa anakunywa lakini hajasema kama hicho kidogo kilichobaki kinamalizwa na pombe.

Huyu shida yake sio pombe. Bali ni kutojipanga vema.. Mkopo si hela ya kuanzishia biashara, ni ya kutanulia biashara.
 
Mtumishi wa umma ukipata check no emb usibweteke jitahid utoke huko halmashauri kwa namna yeyote ile, kuna taasisi nyingi tu wanavuta noti za kutosha sana yaan kwa mwez mtu hakos allowance more than 800K hapo bado mshahara. Tokeni kwenye TGS mtakufa njaa
 
Yah hapa sikupingi kaka..ila nimeshafanya self evaluation nimeona mahali nilipokosea hela nilipoipokea niliona kubwa so karibia million5 ikaishia kununua vitu vya ndani na nguo na kiasi kidogo nikapeleka kwa biashara ila sikuwa seriously japo
Hapo do ulipozingua.

Vitu vya ndani ungelitumia mshahara wako au posho zako za wiki.

Hujachelewa, tuliza kichwa.
 
Nisamehe nitakuwa mkali wala sitakupa maneno ya pole na huruma. Sio kila mtu ni mfanyabiashara wakati mwingine mkubali hatma ya maisha. Ungeishi kwa hiyo laki7 bila kujiingiza kwenye biashara. Unakubali hatma ya maisha unaishi kulingana na mshahara wako. Kwa huo mshahara haupaswi kuwa na watoto 2 ni huyo mmoja anatosha. Na kuna materials hupaswi kutumia wala kutamani kumiliki. Ndio kanuni ya ulimwengu upo kwenye kifungo cha waliokupangia uishi vipi hapa duniani. Wala sio Mungu anayepanga bali wanadamu wenzetu ndio wameweka huo wigo.
 
Mkuu hio pombe itakupoteza mazima... hasa ukizingatia haupo kwenye stable cash flow.

1. Hivyo nakushauri itumie pombe ukishajipata, kwasasa waachie waliojipata.

2. Usivamie/fungue biashara usiyoijua/ usiokuwa na uzoefu nayo kwa kipindi kisichopungua mwaka, hasa kwa pesa ya mkopo ni Hatari yaani dangerous...

Usifungue biashara kwa pesa ya mkopo kwa kuhamasika na motivations za mitandaoni kwani motivation ni hamasa tu ambazo zimekosa uhalisia katika utekelezaji wake on the ground(Changamoto), na hizi changamoto ndio siri yamafanikio yenyewe.

Kwa kumalizia Pesa ya mkopo huwa inatumika kukuza na kupanua biashara iliyokwisha kusimama kwa uhakika... Na sio kuazisha biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…