HOJA Mimi ni mwajiriwa Serikalini. Nilikopa, ila nimefeli malengo nahisi ninaenda kupotea

HOJA Mimi ni mwajiriwa Serikalini. Nilikopa, ila nimefeli malengo nahisi ninaenda kupotea

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kama serekari karibu zote duniani zinakopa, wewe nani usikope?

Kama bado kiwango chako cha kukopesheka ni himilivu, kopa tu, muhimu usirudie makosa uliyofanya katika mkopo wa kwanza.
Ashakwambia kawa mtu wa tungi Sasa Kuna nn hapo.
Mishahara wa laki 4 haitoshi fikiria wale wapiganaji wa huku mitaani wanaishije?
Watumishi wa serikali mmelala sana nyie. Business as usually
 
Acha uzembe na kuishi maisha ambayo sio yako, ulipokopesheka huenda 50% ya huo mkopo imelika kuonyesha wana una ajira na unalipwa vizuri one mistake one goal ila unaweza fanya comeback ya maana na maisha yakaendelea kama umeshajifunza na akili ikakomaa
% kubwa ya hio ela ya mikopo Alinunua nguo na vitu vya ndani
 
Haujasema upo mkoa gani mkuu ni biashara gani unataka kufanya biashara ya mwanzo iliyokuferisha ilikua ni ipi au ndugu yangu unafungua grocery na wewe mlevi inakuaje hapo...
Usikope kwa muda mrefu pambana kulipa hayo madeni ukiwa huru tafuta wazo la biashara harafu ndio ukope sio ukiambiwa tu unaweza kukopesheka hata usipokua na wazo sahihi la biashara unawaza kufanya biashara kwa mazingira yako tatua changamoto zinazokuzunguka ili uwe huru usipokua huru na madeni mengi hakuna kitu utafanya maana mzunguko pia wa biashara upo chini..
 
Kama na wewe biashara yako ilikufa kwanini uone mkeo ni mzigo. Inawezekana unampa biashara hapo hapo unamwachia na masuala yote ya jikoni. Lazima biashara itakufa.

Mke anaweza kuwa kibiashara hayupo vizuri lakini kama ana utii unaweza mfundisha na mwisho wa siku mkawa na mtazamo ambao unakaribiana.
Kabla ya kuchukua huo mkopo hakikisha umejiridhisha na hiyo biashara. Usichukue then ndo unaendelea kutafuta nini cha kufanya. Utakula yote.

Pia biashara haitaki ulevi. Acha ulevi kwanza then ndo uanze biashara.
 
Mimi ni muajiriwa serikali nina mwaka wa 3 sasa.

Nimefeli maisha ila sijakata tamaa.

Niliajiriwa na Take Home ya Laki 7 kwa Msukumo wa maisha maana nilikaa muda mwingi mtaani mara baada ya kuthibitishwa nilikopa bank million 12 kwa miaka 5 nikitarajia nitafanya biashara na kiuhalisia nilifanya biashara na kilimo ila zimefeli zote japo kwa kufanya self evaluation ni uzembe wangu binafsi nimeona.

Nimebaki na Take Home ya Laki 4 nina familia ya mke na mtoto 1 ninapambana kibishi japo kibayq zaidi nimepata mwanamke asiye mpambanaji japo ili sio la kulaumu hapo uzembe ni wangu pia.

Kwanini nimekuja kwenu.

Mimi nimeshafanya self evaluation nimeona kabisa nimefeli maisha na nisipokuwa makini naenda kupotea.

Nimeanza kuwa mlevi mtu nisiyejijali kibaya zaidi nimeingia kwenye madeni hadi haya ya kausha damu.
Ninapoongea hapa mwezi huu mshahara napata laki 2 maana nalipa madeni.

Sasa wakuu naomba kwa ukali au hekima karibuni kunishauri.
Nimemtoa mke wangu maana naona kama mzigo sio mtu anayependa kujishughulisha hapa nilishamfungulia biashara pia kwenye huo mkopo na aliua.

Leo nimekaa nimeona nikope kama million 8 nijilipue tena kwenye biashara.

Nitabaki na take home ya laki 3 ndani ya miaka 4 iliyobaki kadi ni muachie yeye adili na chakula.

Mimi huu mkopo wa million 8 nife nao kama nitafeli nifeli tu.

Kiuhalisia sina option yoyote kwa sasa hata mkinishauri ni save nipate mtaji mtakuwa mnanionea bure.

Karibuni kwa ushauri wakuu.
Ungeeleza hiyo mil12 umeifanyia nn
 
Pole sana Mkuu.

Kwanza una mshahara mkubwa wa take home ya laki 4 na umesema bado una posho pia. Niwahi kufanya kazi sehemu, kuna mtu alikuwa anapokea 290k hadi 315k take home na alikuwa na mke na mtoto na maisha yakawa yanaenda.

Pili, ondoa mindset ya kuwa una mshahara mdogo. Kuna watu wanapokea mshahara kama huo na wengine wengi chini ya hapo na wanafurahia maisha.

Tatu, badili mzunguko wako wa watu wa karibu au mazingira unayokaa mara kwa mara baada ya kazi. Marafiki, sehemu za starehe nk utakutana na watu wanatumia pesa hasa. Pia angalia mazingira uishiyo, kama umepanga sehemu ambayo watu wana maisha mazuri zaidi kuliko wewe, usishindano nao, ukiona huwezi ondoka.

Nne, mkeo ana akili ya kubana matumizi? Ikiwa ndio, zungumza nae kisha mrudishe, huyu atakusaidia eneo hilo lakini pia kujenga future nzuri unayoitaka wewe mzazi kwa damu yako.

Hizo starehe za pombe zitakuja kukuingiza pia ktk umalaya. Utakuwa kila siku unaingiza kipande kinachoweza kuharibu maisha yako.

Kila la heri.
 
Kama na wewe biashara yako ilikufa kwanini uone mkeo ni mzigo. Inawezekana unampa biashara hapo hapo unamwachia na masuala yote ya jikoni. Lazima biashara itakufa.

Mke anaweza kuwa kibiashara hayupo vizuri lakini kama ana utii unaweza mfundisha na mwisho wa siku mkawa na mtazamo ambao unakaribiana.
Kabla ya kuchukua huo mkopo hakikisha umejiridhisha na hiyo biashara. Usichukue then ndo unaendelea kutafuta nini cha kufanya. Utakula yote.

Pia biashara haitaki ulevi. Acha ulevi kwanza then ndo uanze biashara.
Anamlaumu mkewe biashara kufa wakati hata yeye pia mwenye mtaji mkubwa biashara ilikufa.
 
Utaniwia radhi mkuu.
Adui yako wa kwanza ni kutaka kuishi maisha yasio yako(nje ya kipato chako)

Pili ni mke wako(huyo anaweza kuwa kirusi na nguzo ya kukushusha chini usipojipambanua kama mwanaume)

Tatu ni anasa(pombe) hii ushawishi wake mkubwa upo kwa watu unaokuwa nao, nayo hupelekea pia kuishi nje ya kipato chako kwenye mambo ya kununuliana na kuchafua meza ilihali una mambo chungumzima hujayakamilisha.

Ziada, chunga sana tena chunga zaidi huyo mkeo anaweza kuwa chanzo cha anguko lako( kwa maelezo yako anaonekana ni mtu wa kutrend kila toleo la kitu anataka awe nalo ilihali kipato chenu hakiruhusu kuishi kwa trend).

#Hallelujah!!!
Hapa nimejifunza kitu
 
Yah hapa sikupingi kaka..ila nimeshafanya self evaluation nimeona mahali nilipokosea hela nilipoipokea niliona kubwa so karibia million5 ikaishia kununua vitu vya ndani na nguo na kiasi kidogo nikapeleka kwa biashara ila sikuwa seriously japo
Kamwe usianzishe malengo mapya tofauti na yale ya awali mara baada ya kukopa.Hii kanuni imenisaidia mno.
 
Mimi ni muajiriwa serikali nina mwaka wa 3 sasa.

Nimefeli maisha ila sijakata tamaa.

Niliajiriwa na Take Home ya Laki 7 kwa Msukumo wa maisha maana nilikaa muda mwingi mtaani mara baada ya kuthibitishwa nilikopa bank million 12 kwa miaka 5 nikitarajia nitafanya biashara na kiuhalisia nilifanya biashara na kilimo ila zimefeli zote japo kwa kufanya self evaluation ni uzembe wangu binafsi nimeona.

Nimebaki na Take Home ya Laki 4 nina familia ya mke na mtoto 1 ninapambana kibishi japo kibayq zaidi nimepata mwanamke asiye mpambanaji japo ili sio la kulaumu hapo uzembe ni wangu pia.

Kwanini nimekuja kwenu.

Mimi nimeshafanya self evaluation nimeona kabisa nimefeli maisha na nisipokuwa makini naenda kupotea.

Nimeanza kuwa mlevi mtu nisiyejijali kibaya zaidi nimeingia kwenye madeni hadi haya ya kausha damu.
Ninapoongea hapa mwezi huu mshahara napata laki 2 maana nalipa madeni.

Sasa wakuu naomba kwa ukali au hekima karibuni kunishauri.
Nimemtoa mke wangu maana naona kama mzigo sio mtu anayependa kujishughulisha hapa nilishamfungulia biashara pia kwenye huo mkopo na aliua.

Leo nimekaa nimeona nikope kama million 8 nijilipue tena kwenye biashara.

Nitabaki na take home ya laki 3 ndani ya miaka 4 iliyobaki kadi ni muachie yeye adili na chakula.

Mimi huu mkopo wa million 8 nife nao kama nitafeli nifeli tu.

Kiuhalisia sina option yoyote kwa sasa hata mkinishauri ni save nipate mtaji mtakuwa mnanionea bure.

Karibuni kwa ushauri wakuu.
Siku shauri ukope ukiwa kwenye hali hiyo. Kwasasa jitahidi kurudisha amani kati yako na mwenzako.

Sifahamu kama una amini mambo ya kiroho, ila kwa upande wangu nina uzoefu wa hela kupotea kila wakati kunapokuwa na ugomvi nyumbani. Amini usiamini hata ulevi uliopindukia mara nyingi ni matokeo ya nyumba kutokuwa na amani.

Anza kwa kumueleza ukweli wa hali halisi mwenzako, wekeni mkakati wa pamoja wa kupunguza matumizi. Halafu anzeni safari ya pamoja kwa kipato mlichonacho. Mkifaulu huo mtihani ndio mjadiliane kuhusu kukopa.
 
Wote walioshauri wapo vzr, kimsingi hebu tumia utashi wako kulingana na vipaumbele vyako, ujue ili upokee ushauri ni lazima uwe umejiandaa kwa majibu ambayo tayari ulisha tolea maamuzi.
 
Back
Top Bottom