HOJA Mimi ni mwajiriwa Serikalini. Nilikopa, ila nimefeli malengo nahisi ninaenda kupotea

HOJA Mimi ni mwajiriwa Serikalini. Nilikopa, ila nimefeli malengo nahisi ninaenda kupotea

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Nina experience na mikopo mkuu Hizi biashara zetu bila kuziboost kwa mikopo haziinuki leo wala kesho. Inshort nilichojifunza katika mikopo. Bank zenyewe ni wanyonyaji wakubwa riba ni kubwa kupita maelezo. Elimu ya mikopo watu hawana kabisa Mkopo ukiingia mtu anamega kiasi kidogo akale kwanza bata hiyo nyingine ndio ijizungushe iongezeke, hakuna mistake mbaya kama hiyo UMAKINI ndio Kila Kitu Unatakiwa Uwe Mchumi kwelikweli na walivyo washenzi ukirudisha hela yao bila shida wanakubembeleza uchukue mwingine na offer juu! Sasa Jichanganye Utaimba Halleluya
Na jamaa yangu aliwarudishia million 1 CRDB wakaanza kumzungusha kulipia
 
hakuna mtu anaependa kuishi kwa mshahara wa halmashaur maana ni mdogo sana na hakuna posho. shda ni kuwa hatuna connections za kuhamia huko kwny taasisi. kama una connection pls tusaidie.

je ukimkopesha huyo mtumishi afu akakugeuka na kukataa kulipa utafanyaje? mana huna kibali cha kukopesha huezi mshtaki popote. na mshahara ukiingia yeye anatoa kwa simu.

watumishi wengi wanapenda biashara kwa sababu kwny biashara there is leverage yaan biashara inaweza kuendelea ww ukiwa kazn kwako ( in bussiness you can use other people's time). sasa kwny ufundi ni lazma wewe uwepo hapo vinginevyo wale ulowaajiri watakuibia afu wanaenda fungua ofisi kama yako hapo hapo pembeni yako na wanaondoka na wateja wako. haya ukisema ufanye kilimo hyo ardhi unaipata wapi hapa dar?
Tupeni connection na sisi tukale hela za taasisi
 
Mkuu hio pombe itakupoteza mazima... hasa ukizingatia haupo kwenye stable cash flow.

1. Hivyo nakushauri itumie pombe ukishajipata, kwasasa waachie waliojipata.

2. Usivamie/fungue biashara usiyoijua/ usiokuwa na uzoefu nayo kwa kipindi kisichopungua mwaka, hasa kwa pesa ya mkopo ni Hatari yaani dangerous...

Usifungue biashara kwa pesa ya mkopo kwa kuhamasika na motivations za mitandaoni kwani motivation ni hamasa tu ambazo zimekosa uhalisia katika utekelezaji wake on the ground(Changamoto), na hizi changamoto ndio siri yamafanikio yenyewe.

Kwa kumalizia Pesa ya mkopo huwa inatumika kukuza na kupanua biashara iliyokwisha kusimama kwa uhakika... Na sio kuazisha biashara.
Kaka changamoto sisi watumishi saving kwa hii mikopo Inatusaidia maana kupata million 2 au 3 ya haraka haraka ni ngumu sana
 
Nisamehe nitakuwa mkali wala sitakupa maneno ya pole na huruma. Sio kila mtu ni mfanyabiashara wakati mwingine mkubali hatma ya maisha. Ungeishi kwa hiyo laki7 bila kujiingiza kwenye biashara. Unakubali hatma ya maisha unaishi kulingana na mshahara wako. Kwa huo mshahara haupaswi kuwa na watoto 2 ni huyo mmoja anatosha. Na kuna materials hupaswi kutumia wala kutamani kumiliki. Ndio kanuni ya ulimwengu upo kwenye kifungo cha waliokupangia uishi vipi hapa duniani. Wala sio Mungu anayepanga bali wanadamu wenzetu ndio wameweka huo wigo.
Hili swala huwa linanitafakarisha sana hivi yawezekana tunaishi kwenye matrix?
 
Usianze kunyooshea watu vidole! Utafeli zaidi na zaidi!

Katika milioni 12 ulimfungulia mkeo biashara, sidhani kama ulimfungulia biashara ya milioni 12, jiulize ulimfungulia biashara ya shilingi ngapi. Iliyobaki ulifanya wewe biashara na umefeli pia sasa kwann unamsema mkeo.

Tulia usilaumu watu, chukua tu hiyo milioni 8 ujilipue tena, uzuri umeshapata somo utakuwa makini sasa. Tambua ukitafuna tena hiyo milioni 8 UMEKWISHA!
 
Kaka changamoto sisi watumishi saving kwa hii mikopo Inatusaidia maana kupata million 2 au 3 ya haraka haraka ni ngumu sana
Basi inatakiwa mara nyingine ukitaka kufanya biashara hakikisha unaifahamu vizuri hio biashara...

Katika biashara mara chache sana huwa inatokea mtu ana anajiripua/anabet na kufanikiwa na mara nyingi mtu akivamia biashara hua hachukui muda anaifunga.

Biashara inahitaji ufanye utafiti, ule utafiti wa direct observation(unazama kwenye biashara ili upate uhalisia wa changamoto zilizopo).

Jambo la kuzingatia ni hili;
Kwa kumalizia Pesa ya mkopo huwa inatumika kukuza na kupanua biashara iliyokwisha kusimama kwa uhakika... Na sio kuazisha biashara.
 
Ulevi nilikuwa nakunywa nikaacha mimi nina pombe sijaiendekeza ila kwa sasa ndo nimezidisha japo kuacha ninaweza ninashukuru Mungu ananipa Hekima ya kuweza kuacha addicted yoyote ila kinachoniumiza kichwa mke wangu ni mpuuzi sana amekuwa kama mzigo

Kwann unasema mke wako ni mpuuzi mkuu?

Give out 3 Valid causes 😏
 
Makubwa akivuliwa nguo hasimami huchutama Dunia imekupa unachostahili kwa sasa karibu kutulia kabla hujachukua maamuzi ya kukopa.

Usihadaike na stori za waliofanikiwa kama umeshauchukua mkopo uweke kwenye lakini ya voda na uuwekeze kwa mwezi utapata faida hata kidogo huku unafanya research ya biashara pmj na fursa nyengine.
 
As a business consultant wakujitegemea
Nakushauri usikope mtaji kwa sasa na ukiweza ishi kwa kiasi hicho hicho cha 400k yaani usifosi maisha ya kuzidi hicho kiasi

My driver namlipa 500k ana mke na watoto watatu na wala sijawahi sikia ana Kausha damu,

Ntarudi baadae for way forward
 
As a business consultant wakujitegemea
Nakushauri usikope mtaji kwa sasa na ukiweza ishi kwa kiasi hicho hicho cha 400k yaani usifosi maisha ya kuzidi hicho kiasi

My driver namlipa 500k ana mke na watoto watatu na wala sijawahi sikia ana Kausha damu,

Ntarudi baadae for way forward
Sasa kama dereva unamlipa 500k wewe income inasomaje! Buzznes gani mkuu hebu tumegee tonge nasisi
 
Back
Top Bottom