Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

Ahsante kwa nyongeza KAKA, mi nilichoona jamaa bado ana ule mtazamo wa kishamba wa wanafunzi wa kibongo ambao baadhi yetu tuliwahi kuupitia tulipokuwa 5 & 6 baada ya trojan wa organic chemistry, quantum mechanics, taxonomy na microbiology kufanya yake

Kama unakumbuka tulijazana ujinga kwamba wanasayansi wote hawaamini uwepo wa Mungu, jambo ambalo si kweli. Sayansi haikupori haki ya kuamini uwepo wa Mungu kwa hoja ya kutothibitishika kwa majaribio ya kisayansi - huu ni ufahamu mbovu na ndo sumu tulizokuwa tunanyweshana bila antidotes. Uhalisia ni kwamba, si kila mwanasayansi ni atheists, wapo wanasayansi wengi tu wakubwa ambao ni theists, naposema wengi namaanisha wengi wakiwemo Kepler, Newton, Mendel, Einstein, Korpenicus na wengineo

Na hili haliishi kwa wanasayansi tu, hata wanafalsafa wote siyo atheists, wapo wana filosofi wakongwe tena walioanzisha na kusimika misingi mingi ya falsafa na logic na kuipa nguvu misimamo yao ambao wanaamini au waliamini uwepo wa Mungu akiwemo Galileo, Campbell, Aquinas, Aristotle, Anthony Flew na wengineo

Sasa ndugu yetu bado anaishi na huyo trojan kwamba ukishakuwa mwanasayansi eti huwezi kuamini uwepo wa Mungu sababu ni mambo yaliyo kwenye misingi tofauti. Yaonyesha hajui kwamba katika fani ambayo ni rahisi zaidi kukufanya ukaamini uwepo wa Mungu ni sayansi, sayansi asili na sayansi ya mazingira kama jiografia: concept kama cosmology kama ulivyodokeza na nyinginezo. Yatosha mtu kumsoma na kumuelewa kiumbe duni mno kama mdudu chungu 'sisimizi' au jani la mmea kama ulivyodokeza na akapata utambuzi wa kufahamu uwepo wa Mungu

Jamaa yetu anafikiri kuamini Mungu kwa mwanasayansi kunamlazimu achukue DNA yake aingie nayo maabara au achukue telescope/microscope amchungulie amuone, yikes!

Sijawahi jadiliana na atheists wa karne hii mwenye hoja dhaifu kama hizo, na sijui nani aliyemwambia kwamba kuona ndo kuamini, au ndo positivism philosophy of knowing? Na kama umemuelewa kwenye maelezo yake alipokuwa akiponda imani, anadai kwamba hata akithibitikiwa na ukweli kuhusu uwepo wa Mungu hataamini wala kuabudu, eti ni ujinga, inasikitisha sana!

Katika misingi yangu niliyojiwekea huwa sijadiliani na mtu mwenye misimamo ya kizushi hivyo, yaani hata kama amesimamishiwa hoja za haki/kweli yeye aendelee kupinga tu! Hiyo ni sifa ya mtu mwenye kibri na upumbavu, aende mashariki na magharibi, akusanye wanasayansi wote wa sasa na waliokuwepo tangia enzi na enzi hamna atakayeweza kutibu hayo maradhi, asituchoshe
 
Tumuombee huyu jamaa elimu yake iboreke aelimike zaidi, aujue ukweli.

Kwa kweli, labda kwa maombi, lakini kama ni hoja tumeshachemka, we fikiri mtu timamu anafikia kuandika "hata akijua kweli Mungu yupo hawezi abudu ni ujinga"

Tuna kazi pevu mno, ila walau tutakuwa tumefaulu kumfanya aamini hata kama kimatendo atakuwa mkaidi
 


Chimbuko la tafakuri ni wazo, na zao la tafakuri ni ubunifu au ugunduzi 'uvumbuzi'
 

"Science without religion is lame, religion without science is blind" - ALBERT EINSTEN
 

EINSTEIN ni mwanasayansi 'mdadisi' mkubwa kuliko wote katika karne ya 20 na alikuwa akiamini uwepo wa Mungu 'mtu wa imani'

Sasa mwenzangu na mimi kutoka Bonyokwa Nangulukuru sijui hoja zako huwa unaziokotea kwenye jalala gani

Ni kana kwamba huwezi kueleza jambo bila kudhihirisha ufahamu wako mbovu wa mambo au udhaifu wa upeo wako
 
Nimejua mpangilio wa mawazo na masomo ya kiroho kwa kufatilia miaka mingi. Kuna mambo kimsingi yapo kwenye masuala ya imani lakini sio kwenye taaluma za sayansi. Mfano tafsiri na uelewaji wa mambo mengi yanategemea utashi wa mtu na mipaka atakayojiwekea. Hakuna hicho kitu kwenye vipimo vya kisayansi. Hatuwezi kupata maana tofauti kwenye seti moja ya data halafu wote tukawa sawa. Kitu ili kikubalike na kila mmoja lazima kipitie chujio la upinzani na matokeo yawe sawa kwa kila anayepima na kuona majibu. Hali ni tofauti kwenye uzushi na usanii wa mambo ya kiroho. Tutazunguka sana lakini ukweli uko wazi kabisa. Ufunuo ni kitu cha uongo. Cha kutunga. Wengne wameiga. Hiyo deduction ya kuona kitu kama mti na kukadiria tu kuna mungu kaumba ndio uzushi wenyewe. Very wrong and far from scientific thought process.

Essence ya kuamini na kuabudu iko na sababu. Tamaduni zina mchango mkubwa sana lakini pia baiolojia ya miili yetu. Chanzo mwilini kiko kwenye bongo zetu. Kuna kitabu kimeelezea vizuri na kwa urahisi hii pointi kinaitwa "human brain " cha dr. Rita Carter. Simple explanations za kuanzia. So utakuta kwa vile bongo zetu sote zimeundwa kuhitaji kuabudu vitu vya kuongoza maisha yetu kila sehemu duniani kuna hizi imani. Tofauti zinaibuka kulingana na mazingira au muingiliano wa tamaduni.

In any way, imani zote pamoja na kazi zote na hasara zake hazina ukweli ndani yake! Ubunifu una kikomo. Kikomo ni sayansi. U can imagine flying cars au interstellar travel but only scientific and technological advances have the last say. There are multiple times the number of ideas than applicable inventions. However I do agree it is very useful in keeping technicians on there toes to do better each passing day and make improvements. [emoji106]
 
Kuhusu sharti la kutochanganya taaluma na imani nahisi hujanielewa. Kuna wataalamu wengi tu wenye kufuga hizo imani za mungu kichwani. Nilichojaribu kuelezea ni kwamba mtu huyo mwenye hizo imani hawezi kuziingiza kwenye taaluma. Kufanya hivyo anakuwa ameshindwa kutimiza wajibu kitaaam. Imani na taaluma haviendi pamoja hata nukta moja ya muda. Ukichanganya tu umeharibu. Ukiwa kwenye meza ya sayansi Fata taratibu mungu weka mbali. Ukirudi kwako piga goti utakavyo au kwenye muda wako wa ziada tembelea hekalu ujumuike na wenzio wa imani sawa na yako. Sijasema haiwezekani kwa injinia au tabibu kuwa na imani. Uzi huu umeanzishwa na mtu anadai ni mwanabaiolojia. Kimantiki inashangaza lakin ndio uhalisia wa kibinadamu. Usinizushie uongo.

Nilikujbu madhaifu ya sayansi ni kama ya fani zingine zisizo za kiimani. Sayansi sio jambo la kiimani lenye udhaifu kuanzia mwanzo ndani yake plus na watu wanaojihusisha nayo. Inabeba tu madhaifu yote ya watu wanaojihusisha nayo pasipo yenyewe kulazimu makosa, madhaifu yote ya binadamu yanatokea kwenye kazi. Huwezi kuuliza muziki una udhaifu gani? Jibu ni rahisi. Kama fani hakuna udhaifu wa kulaumu fani yenyewe. Ila mambo ya wanamuziki ndio yanajenga au kubomoa fani yao.

Kuhusu uchawi ni kweli haupo kiuhalisia. Naandika kiuhalisia nikimaanisha nacho ni kitu ambacho hakina athari kama inavyodhaniwa. Hakuna namna ya uchawi kufanya kazi. Mfano mtu apasue nazi kama kutaka kitu fulani kitokee kama kutoa kitu kingine kisichoelezeka kama mkosi au jini n.k n.k.... wengi wametoa na wanaendelea kutoa ushuhuda kuona uchawi na wachawi. Shida hapa hatuwezi kuamini na kuchukulia rasmi upo kwa ushuhuda pekee. What if huyo mtu alikuwa anapitia hallucination? Kuna illusions nyingi sana kama kuona vitu kwenye giza, vivuli kuhisi ni vitu hai... utapokea vipi kitu bila uhakika nacho? Bila shaka huwezi pasipo uhakika. Maisha yote kwanini sijarogwa au kuona uchawi? Basi tuseme tusioamini huo ujinga wachawi hutuacha salama hawatuchezei au kututoa misukule. Siku ushahidi wa uchawi utakuwa wazi kila mtu atapokea hayo mambo bila ubishi na kufatilia namna yatasaidia maisha yake. Sayansi haiwezi kukataa mambo ya uchawi kwa vile sio kazi yake kukataa au kukubali bali kuchunguza ukweli wake. Kama hamna ushahidi hakuna la kuongeza zaidi ya kusema hamna uthibitisho wa kitu uchawi unaoongelewa. Usilazimishe kitu kisicho na ushahidi wa moja kwa moja kikubalike tu ili kiendane na kinachodaiwa kwenye jamii. Kukosa ushahidi ni hoja tosha kusema hakuna uchawi.

Kwenye fani za neuroscience bado consciousness ni suala mtambuka. Ni hivi karibuni tu kumeanza kuwa na vifaa kama mashine ya nuclear magnetic resonance imaging, PET scan vya kuusoma na kuupima ubongo moja kwa moja ili kuuelewazaidi. So hata ukimuuliza mtaalamu consciousness iko sehemu gani hutopata jibu. Hasa atasema bado haijulikani eneo hilo. Sayansi sio dini. Haisemi inajua kila kitu na uiamini tu. Inaelewa na kuweka wazi kikomo cha uelewa kilichofikiwa. Kinasogea kila siku, ni suala la muda tu. Consciousness itaeleweka zaidi ya sasa. Kuna vingi vilikuwa havijulikani siku za nyuma.

Kuhusu Darwin mtu atakeweza kuelewa dhana alizoanza kuzigundua ni mwenye akili wazi inayoweza kupokea mambo yasiyo dhahiri kwa haraka. Kama una akili iliyojifungafunga kiasi kwamba ukiambiwa viumbe vyote vinamauhisiano unashindwa kuelewa lazima akupe shida. Ukisikia sokwe, tumbiri, sisi, binadamu wa kale na primates wote tuna chanzo kimoja lazima ukimbilie kutoelewa na kudhani tulizaliwa na viumbe waliopo hivi sasa!
 
Kama sio kitu ni nini sasa🥱
 
"Science without religion is lame, religion without science is blind" - ALBERT EINSTEN
Nakubali. Kuna motivation fulani hivi ya ziada inasukuma kufatilia zaidi haya mambo asilia ili kukimbia upuuzi wa imani potofu kama mambo hayo ya mungu!
 
Unaelewa aina ya mungu aliyedhaniwa kuwepo na Einstein au unaanza kuropoka?
 

[emoji848]

Unajaribu kukimbia kivuli chako, ukifanikiwa nifahamishe nikutunze, maelezo yako ya awali yapo wazi, na hilo umelionyesha mara nyingi zaidi ulipokuwa ukijadiliana Uhakika Bro kuliko hata mimi "ulikuwa wamshangaa na kumuona mtu duni sana kuwa muumini na pia kuwa mwanabaiolojia", na kwenye maelezo yako ulijikita kadri uwezevyo kumthibitishia kwamba anachoamini haimpasi kuamini sababu eti ni mwanasayansi, sasa unachojaribu kukana ni nini? Kujua kugeuzageuza maana ya sentensi na maneno siyo kujua kujenga hoja
 

Hey, hatupo kwenye siasa, jibu unachoulizwa 'taja', hili si darasa la siasa! hivi we jamaa una shida gani? yaani uulizwe ni yapi mapungufu ya fani ya takwimu, udai takwimu kama fani haina mapungufu bali watakwimu na wanaojihusisha na fani ya takwimu kama wanadamu ndo wana mapungufu, hii akili ndo huwa unaitumia kuvuka barabara?

Takwimu kama fani ina madhaifu au mapungufu yafuatayo:
  • Haielezi phenomenom ambazo ni qualitative
  • Haielezi stori nzima "takwimu hueleza mambo kwa muhtasari"
  • Takwimu ni fani isiyodili na figure moja kwa mfano: uzito wa mtu X
Kinachokushinda kueleza kama hivyo ni nini? Eti sayansi siyo jambo la kiimani, mara sijui muziki kama fani hauna madhaifu! Nani kakwambia hauna? Tuhamie kwenye music?

Najua fika kinachokufanya ukwepe kutaja udhaifu wa fani ya sayansi, endelea kuzunguka mbuyu hivyohovyo, la sivyo utaivua fani nguo na baadhi ya angle zitabaki tupu, kukwepakwepa hivyo ni salama kwa misingi yako batili
 

Nijibu kwa kifupi tu kwamba, una shida kubwa mno ya uelewa, maelezo yako ya mwanzo yanakiri na kusadikisha ushahidi unaotolewa na watu wengi kuhusu uchawi halafu mwisho unakama kwa hoja inayopingana na hiyo ya mwanzo ya kukosekana kwa ushahidi, ulikuwa unatengeneza statement of the problems e? What if huyo mtu! Siyo wewe uliyesema "watu wengi", au ulisa

Eti uchawi haupo kwa sababu hauna athari kama unavyodhaniwa! Hili si suala la kudhani, Ebo! Wala siyo suala la kukosekana kwa athari, ni hali ambayo kwa 100% ipo na hatuhitaji sayansi ituthibitishie kuwepo au kutokuwepo kwake, sayansi haina uwezo huo, sayansi ina udhaifu mkubwa katika kushindwa kuyatambua/kuyaeleza/kuyakubali/kuyabaini baadhi ya mambo ambayo ni halisi 'reality' na kukimbilia kwenye hutimisho la kutokuwepo kwa hayo mambo! Na nilijua ni lazima utajificha humo ndo maana kwenye maelezo yangu ya mwanzo sikusita kueleza

Eti utapokeaji kitu bila uhakika nacho, unahitaji uhakika gani? Mambo mangapi kwenye sayansi tumefundishwa na tumeyapokea na hatuna uhakika nayo? Na siyo kuwa na uhakika nayo tu bali mengi hayapo kabisa, au yapo kama idea tu lakini hayatahibitishiki kwa kutumia milango ya fahamu wala majaribio, au hatuna uhakika nayo wala hatuna uhakika juu ya uwepo wa hayo. Ulishawahi kuhakiki uwepo wa Moles au Atoms? Ulihakikije? Wapi ulishawahi kuhakiki uwepo wa hewa au upepo? Ulihakikije? Ulishawahi kuiona hewa au una-experience tu? Wapi ulishawahi kuhakiki uwepo wa latitude na longitude? Uache unafiki, mambo kibao tumemezeshwa tu pasina uhakiki wowote na tumeyapokea kwa upofu pasina hata kuthubutu kufanya uchunguzi. Ushauri: Unapokuwa unajenga hoja yoyote kumbuka kuanzia kwenye sayansi, weka hilo akilini, kama zipo lakini

Eti huo ujinga! Ita hiyo phonemena vyovyote utakavyo, hilo halibadilishi chochote wala haliondoshi chochote
 

Nijibu kwa kifupi kwamba: si kila phenomenon ambayo ni halisi "reality" sayansi inaweza kuichunguza, kuielezea na kuitolea hitimisho la kweli
 

Hongera, hili umejibu vizuri kiasi. Sayansi kushindwa kutambua akili ilipo hakuifanya akili iwepo au isiwepo, na hili linagutusha kwamba si kila ambacho sayansi inashindwa kulitolea ufafanuzi hitimisho ni kutokuwepo kwake

Na hilo linagutusha zaidi kwamba kuna phenomenon ambazo ni superior kwa sayansi na akili ni moja wapo, kama sayansi imeweza kuelezea unobservable mystical phenomenon kama atoms na subatoms, inashindwaje kueleza akili ambayo ni innate unobservable qualitative phenomenon?

Ahsante sana, kwa mara ya kwanza umedhihirisha udhaifu wa sayansi hapo ulipoandika "Sayansi haisemi inajua kila kitu", ama kusuhu dini kujua kila kitu hilo sijui umelipatia wapi? Hamna dini inayofundisha hivyo, acha kulisha imani za watu maneno ya uongo

Sasa huo udhaifu wa sayansi ulioutaja hapo ndo phenomena kama JUJU "Uchawi" zinaingia ndani yake. Najua fika kwamba unajua udhaifu wa sayansi japo unajifanya kujificha chini ya kivuli cha dole gumba lako. Sayansi kushindwa kujua kila kitu hakuyafanyi mambo yasiyojulikana na sayansi yawepo au yasiwepo [emoji4]. Nachokupendea huwa unarukaruka wee halafu baadaye unajifunga mwenyewe

Niweke wazi katika maelezo yako yote uliyowahi kuandika, hichi kipengele umeonyesha ukomavu wa ufahamu, umekitendea haki kwa kiasi chake, doa chafu: kuchanganya maelezo kwa kutuhumu dini kujua kila kitu
 

Achilia tusiojua kusoma wala kuandika ambao kwa wewe unatuona hatuna akili, ni wanasayansi wangapi wakubwa kwa wadogo, wasasa na wakale wamezikosoa vibaya mno nadharia zake za evolution? Hao wanasayansi hawana akili? Wewe ndo una akili sana e? Unachojaribu kufunikafunika na kupakapaka mafuta hapo ni nini?

Huu utahira wa Darwin endelea kujadiliana na wanafunzi wa darasa la kwanza D, tena wale wasio na mtaala wa Montessori, japo hata wao watakuona dishi limeyumba
 
Mungu yupo na ataendelea kuwepona anaepiga uwepo wa Mungu anamattzo ila Yesu na Mohammad hao hawapo na hao ndo utapeli unapoanzia na apo ndo ugomvi huanzia
 
Nakubali. Kuna motivation fulani hivi ya ziada inasukuma kufatilia zaidi haya mambo asilia ili kukimbia upuuzi wa imani potofu kama mambo hayo ya mungu!
?

Ukubali ukatae sisi haituhusu, wewe kuona jambo fulani ni upuuzi hakulifanyi hilo jambo kuwa ni upuuzi. Na huo ufahamu ulioupata kwenye quote ya Einstein ni wewe na akili zako za kukodisha tu, kwa sisi ambao tunamsoma na kumuelewa Einstein tunajua amemaanisha nini alipohusisha hayo mambo mawili 'uhusiano'
 
Unaelewa aina ya mungu aliyedhaniwa kuwepo na Einstein au unaanza kuropoka?
Hilo halijalishi! Eti "dhana", unataka kuthibitisha nini? Iwe ni dhana au ni yakini sisi hilo halituhusu, hayo ni mambo yanayoishi kwenye moyo na fikra za mtu sisi hatuwezi kuyajua, hoja ni kwamba "ALBERT EINSTEIN NI MWANASAYANSI NA ALIAMINI MUNGU YUPO". Sasa je ni Mungu yupi na mwenye sifa zipi? Mjadala wetu haukuwa sifa za Mungu, mada ilikuwa "kuamini au kutoamini uwepo wa Mungu kwa wanasayansi". Kwa kifupi tu ni kwamba mjadala wetu wa awali umeishia hapo na imejitosheleza, yafuatayo ni nyongeza tu

Najua umeuliza hivyo kwa sababu umesoma maelezo machache ambayo Einstein alinukuliwa aliposema anaamini Mungu wa mwanafalsafa Spinoza. Kwa upeo wako finyu utakuwa umesoma sifa chache za huyo Mungu kama makala nyingi zilivyonukuu na umebweteka badala ya kutafuta marejeo halisi ya Spinoza alipojaribu kueleza sifa za Mungu wake. Nikufumbue macho kwamba sifa za Mungu wa Spinoza zinazolandana mno na sifa za Mungu wa Abrahamic Religions kuliko kutofautiana kwake, yaani karibu 65% - 85% ya sifa za Mungu wake alizoeleza zinamsadifu Mungu wa Abrahamu au Mungu wa wengi katika wanadamu

Halafu pia, hivi kuna sehemu au siku uliwahi kuniuliza Mungu wangu ana sifa zipi au ni Mungu gani? Kilichokufanya usiniulize ni nini? Mbona uliendelea tu kujadili uwepo au kutokuwepo kwake? Ni wazi kwamba una utambuzi usiohitajia kuniuliza kujua Mungu wangu ni wa aina gani na ana sifa gani? Ulipoandika "baada ya kuabudu uchukue telescope/microscope umchungulie umuone Mungu" ulikusudia Mungu gani? Ng'ombe au Mwamba? Kwani Miungu hivyo haionekani kwa macho ya nyama hadi utumie hadubini? Ni wazi kwamba ulijua mimi kama theist ni Mungu gani ninayemkusudia na ana sifa zipi kuu

Kwa upeo wako unaona ni jambo linalowezekana wanasayansi/wanafalsafa wote ambao ni theists wakaamini Mungu mwenye sifa zinazofanana kwa 100%? Sasa tunaposema wanasayansi 'theists' wanaamini uwepo wa Mungu huwa tunamaanisha nini? Huwa tunazingatia kufanana kwa 100% kwa sifa za Uungu kwa kila mmoja wao? Au huwa tunakusudia Mungu wa aina gani? Hoja nyingine hata siyo za kuibua, ungekausha tu

Na huenda hujanielewa, ngoja nikukokoteze tena!

Kwani sifa za Mungu aliyeaminiwa kuwepo au kuzungumziwa na Plato au Socrates ndo sifa za Mungu wa Eliyya au Zakaria ?

Je, sifa za Mungu aliyeaminiwa na kuzungumziwa na Faraday au Pasteur ndo sifa za Mungu wa Yesu au Muhammad?

Kwani hata Abrahamic Religions kila dini inayounda hilo kundi inapoelezea sifa za Mungu wao huwa zinafanana kwa 100%?

Ingia ndani kidogo, yaani katika ngazi ya madhehebu ya kila dini, je kila dhehebu linavyoeleza sifa za Mungu wao ndivyo mapote mengine ya dini hiyo yanavyoeleza pasina kutofautiana kukubwa au kudogo?

Shuka katika ngazi ya waumini wa dhehebu moja la kila dini, je kila muumini anayejiegemeza katika dhehebu A au B sifa za Mungu anayemuamini anavyozieleza zinafanana zote na sifa za Mungu wa muumini mwenzake wa dhehebu hilohilo?

Katika kujiuliza hayo maswali bila shaka kuna mambo utakuwa umejifunza ikiwemo hili: ufahamu hutofautiana hata kwa watoto waliotoka kwenye mfuko mmoja wa uzazi, ni mambo ya kawaida watu kutofautiana uelewa kutokana na kutofautiana upeo na daraja la ubobezi wa fani yeyote

Na haswa kwenye hilo kinachozingatiwa ni dhamira ya mlengwa kwa Mungu kwa kubainisha japo sifa zake kuu chache, kukosea au kupatia kumuelezea ni matokeo ya ufahamu tu, na wala hilo haliondoshi kusudi la Mungu wala uwepo wake. Hivi kwani Einstein hata katika sayansi ni vingapi amepatia na vingapi amekosea? Sasa kama yapo hayo kinachokushangaza kwenye hili ni nini na ukizingatia filosofia wala thiolojia si fani zake. Nanukuu maelezo yako "Tafsiri na uelewaji wa mambo mengi yanategemea utashi wa mtu na mipaka atakayojiwekea"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…