Ahsante kwa nyongeza KAKA, mi nilichoona jamaa bado ana ule mtazamo wa kishamba wa wanafunzi wa kibongo ambao baadhi yetu tuliwahi kuupitia tulipokuwa 5 & 6 baada ya trojan wa organic chemistry, quantum mechanics, taxonomy na microbiology kufanya yakeNimeipenda comment yako hasa kwa hichi kipande, umenikumbusha kitu kikubwa sana yaani. Tena inajulikana kabisa kuwa, mtu aliyesoma kidogo sayansi ndio yupo rahisi zaidi kumkataa Mungu, lakini akisoma deep zaidi akabobea ana uwezekano mkubwa zaidi wa kumkubali Mungu. Sheikh mmoja aliwahi kusema kila kilichoumbwa unachokiona ni aya, ni kama mafunuo ya Muumba kwetu. Ukilisoma jani au mbuzi vizuri utamtambua Mungu, hata ukiisoma cosmos vizuri utamshuhudia Mungu. Sayansi haipingani na Mungu sema tu elimu nusu, ujuzi nusu huwa una mtindo wa kuwa haribifu kwa mwenye kuupata. Tumuombee huyu jamaa elimu yake iboreke aelimike zaidi, aujue ukweli.
Sasa masdinero masproblemas kama tukipropose nadharia ya kwamba; Kwa kuwa imagination na imani inaonekana kwa binadamu zaidi, na kwa kuwa tunatambua kuwa inaashiria uwepo wa ufikiri wa hali ya juu ndiyo unaowezesha imagination. Basi wale wanaoshindwa kuwa na imani basi ni walemavu. Yaani wana upungufu wa uwezo fulani wa kiakili wa kuwa na imani maana imagination zao sio powerful kivile[emoji2955]?
Au tukitaka kuwa na huruma kwao tusiwadogoshe kuwafanya subnormal. Tuchukulie kwamba imagination kali iwe ni kwa wale ambao wapo na uwezo mkubwa zaidi kiakili yaani 'gifted' halafu hawa wasioimagine wawe normal people. Either way wale wanaoimagine kiakili wapo juu ya wasiotaka kuimagime. Tusisahau historia inaonesha gunduzi mbalimbali [za kisayansi na kijumla tu] tu zilipelekea kuhusianisha watu na wachawi au wanawasiliana na miungu kutokana na 'watu wa kawaida' kushindwa kun'gamua inawezekanaje mtu wa kawaida kuja na majibu/teknolojia/elimu tata namna hiyo.
Kama unakumbuka tulijazana ujinga kwamba wanasayansi wote hawaamini uwepo wa Mungu, jambo ambalo si kweli. Sayansi haikupori haki ya kuamini uwepo wa Mungu kwa hoja ya kutothibitishika kwa majaribio ya kisayansi - huu ni ufahamu mbovu na ndo sumu tulizokuwa tunanyweshana bila antidotes. Uhalisia ni kwamba, si kila mwanasayansi ni atheists, wapo wanasayansi wengi tu wakubwa ambao ni theists, naposema wengi namaanisha wengi wakiwemo Kepler, Newton, Mendel, Einstein, Korpenicus na wengineo
Na hili haliishi kwa wanasayansi tu, hata wanafalsafa wote siyo atheists, wapo wana filosofi wakongwe tena walioanzisha na kusimika misingi mingi ya falsafa na logic na kuipa nguvu misimamo yao ambao wanaamini au waliamini uwepo wa Mungu akiwemo Galileo, Campbell, Aquinas, Aristotle, Anthony Flew na wengineo
Sasa ndugu yetu bado anaishi na huyo trojan kwamba ukishakuwa mwanasayansi eti huwezi kuamini uwepo wa Mungu sababu ni mambo yaliyo kwenye misingi tofauti. Yaonyesha hajui kwamba katika fani ambayo ni rahisi zaidi kukufanya ukaamini uwepo wa Mungu ni sayansi, sayansi asili na sayansi ya mazingira kama jiografia: concept kama cosmology kama ulivyodokeza na nyinginezo. Yatosha mtu kumsoma na kumuelewa kiumbe duni mno kama mdudu chungu 'sisimizi' au jani la mmea kama ulivyodokeza na akapata utambuzi wa kufahamu uwepo wa Mungu
Jamaa yetu anafikiri kuamini Mungu kwa mwanasayansi kunamlazimu achukue DNA yake aingie nayo maabara au achukue telescope/microscope amchungulie amuone, yikes!
Sijawahi jadiliana na atheists wa karne hii mwenye hoja dhaifu kama hizo, na sijui nani aliyemwambia kwamba kuona ndo kuamini, au ndo positivism philosophy of knowing? Na kama umemuelewa kwenye maelezo yake alipokuwa akiponda imani, anadai kwamba hata akithibitikiwa na ukweli kuhusu uwepo wa Mungu hataamini wala kuabudu, eti ni ujinga, inasikitisha sana!
Katika misingi yangu niliyojiwekea huwa sijadiliani na mtu mwenye misimamo ya kizushi hivyo, yaani hata kama amesimamishiwa hoja za haki/kweli yeye aendelee kupinga tu! Hiyo ni sifa ya mtu mwenye kibri na upumbavu, aende mashariki na magharibi, akusanye wanasayansi wote wa sasa na waliokuwepo tangia enzi na enzi hamna atakayeweza kutibu hayo maradhi, asituchoshe