Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

Nimeipenda comment yako hasa kwa hichi kipande, umenikumbusha kitu kikubwa sana yaani. Tena inajulikana kabisa kuwa, mtu aliyesoma kidogo sayansi ndio yupo rahisi zaidi kumkataa Mungu, lakini akisoma deep zaidi akabobea ana uwezekano mkubwa zaidi wa kumkubali Mungu. Sheikh mmoja aliwahi kusema kila kilichoumbwa unachokiona ni aya, ni kama mafunuo ya Muumba kwetu. Ukilisoma jani au mbuzi vizuri utamtambua Mungu, hata ukiisoma cosmos vizuri utamshuhudia Mungu. Sayansi haipingani na Mungu sema tu elimu nusu, ujuzi nusu huwa una mtindo wa kuwa haribifu kwa mwenye kuupata. Tumuombee huyu jamaa elimu yake iboreke aelimike zaidi, aujue ukweli.

Sasa masdinero masproblemas kama tukipropose nadharia ya kwamba; Kwa kuwa imagination na imani inaonekana kwa binadamu zaidi, na kwa kuwa tunatambua kuwa inaashiria uwepo wa ufikiri wa hali ya juu ndiyo unaowezesha imagination. Basi wale wanaoshindwa kuwa na imani basi ni walemavu. Yaani wana upungufu wa uwezo fulani wa kiakili wa kuwa na imani maana imagination zao sio powerful kivile[emoji2955]?

Au tukitaka kuwa na huruma kwao tusiwadogoshe kuwafanya subnormal. Tuchukulie kwamba imagination kali iwe ni kwa wale ambao wapo na uwezo mkubwa zaidi kiakili yaani 'gifted' halafu hawa wasioimagine wawe normal people. Either way wale wanaoimagine kiakili wapo juu ya wasiotaka kuimagime. Tusisahau historia inaonesha gunduzi mbalimbali [za kisayansi na kijumla tu] tu zilipelekea kuhusianisha watu na wachawi au wanawasiliana na miungu kutokana na 'watu wa kawaida' kushindwa kun'gamua inawezekanaje mtu wa kawaida kuja na majibu/teknolojia/elimu tata namna hiyo.
Ahsante kwa nyongeza KAKA, mi nilichoona jamaa bado ana ule mtazamo wa kishamba wa wanafunzi wa kibongo ambao baadhi yetu tuliwahi kuupitia tulipokuwa 5 & 6 baada ya trojan wa organic chemistry, quantum mechanics, taxonomy na microbiology kufanya yake

Kama unakumbuka tulijazana ujinga kwamba wanasayansi wote hawaamini uwepo wa Mungu, jambo ambalo si kweli. Sayansi haikupori haki ya kuamini uwepo wa Mungu kwa hoja ya kutothibitishika kwa majaribio ya kisayansi - huu ni ufahamu mbovu na ndo sumu tulizokuwa tunanyweshana bila antidotes. Uhalisia ni kwamba, si kila mwanasayansi ni atheists, wapo wanasayansi wengi tu wakubwa ambao ni theists, naposema wengi namaanisha wengi wakiwemo Kepler, Newton, Mendel, Einstein, Korpenicus na wengineo

Na hili haliishi kwa wanasayansi tu, hata wanafalsafa wote siyo atheists, wapo wana filosofi wakongwe tena walioanzisha na kusimika misingi mingi ya falsafa na logic na kuipa nguvu misimamo yao ambao wanaamini au waliamini uwepo wa Mungu akiwemo Galileo, Campbell, Aquinas, Aristotle, Anthony Flew na wengineo

Sasa ndugu yetu bado anaishi na huyo trojan kwamba ukishakuwa mwanasayansi eti huwezi kuamini uwepo wa Mungu sababu ni mambo yaliyo kwenye misingi tofauti. Yaonyesha hajui kwamba katika fani ambayo ni rahisi zaidi kukufanya ukaamini uwepo wa Mungu ni sayansi, sayansi asili na sayansi ya mazingira kama jiografia: concept kama cosmology kama ulivyodokeza na nyinginezo. Yatosha mtu kumsoma na kumuelewa kiumbe duni mno kama mdudu chungu 'sisimizi' au jani la mmea kama ulivyodokeza na akapata utambuzi wa kufahamu uwepo wa Mungu

Jamaa yetu anafikiri kuamini Mungu kwa mwanasayansi kunamlazimu achukue DNA yake aingie nayo maabara au achukue telescope/microscope amchungulie amuone, yikes!

Sijawahi jadiliana na atheists wa karne hii mwenye hoja dhaifu kama hizo, na sijui nani aliyemwambia kwamba kuona ndo kuamini, au ndo positivism philosophy of knowing? Na kama umemuelewa kwenye maelezo yake alipokuwa akiponda imani, anadai kwamba hata akithibitikiwa na ukweli kuhusu uwepo wa Mungu hataamini wala kuabudu, eti ni ujinga, inasikitisha sana!

Katika misingi yangu niliyojiwekea huwa sijadiliani na mtu mwenye misimamo ya kizushi hivyo, yaani hata kama amesimamishiwa hoja za haki/kweli yeye aendelee kupinga tu! Hiyo ni sifa ya mtu mwenye kibri na upumbavu, aende mashariki na magharibi, akusanye wanasayansi wote wa sasa na waliokuwepo tangia enzi na enzi hamna atakayeweza kutibu hayo maradhi, asituchoshe
 
Tumuombee huyu jamaa elimu yake iboreke aelimike zaidi, aujue ukweli.

Kwa kweli, labda kwa maombi, lakini kama ni hoja tumeshachemka, we fikiri mtu timamu anafikia kuandika "hata akijua kweli Mungu yupo hawezi abudu ni ujinga"

Tuna kazi pevu mno, ila walau tutakuwa tumefaulu kumfanya aamini hata kama kimatendo atakuwa mkaidi
 
Sasa masdinero masproblemas kama tukipropose nadharia ya kwamba; Kwa kuwa imagination na imani inaonekana kwa binadamu zaidi, na kwa kuwa tunatambua kuwa inaashiria uwepo wa ufikiri wa hali ya juu ndiyo unaowezesha imagination. Basi wale wanaoshindwa kuwa na imani basi ni walemavu. Yaani wana upungufu wa uwezo fulani wa kiakili wa kuwa na imani maana imagination zao sio powerful kivile[emoji2955]?

Au tukitaka kuwa na huruma kwao tusiwadogoshe kuwafanya subnormal. Tuchukulie kwamba imagination kali iwe ni kwa wale ambao wapo na uwezo mkubwa zaidi kiakili yaani 'gifted' halafu hawa wasioimagine wawe normal people. Either way wale wanaoimagine kiakili wapo juu ya wasiotaka kuimagime. Tusisahau historia inaonesha gunduzi mbalimbali [za kisayansi na kijumla tu] tu zilipelekea kuhusianisha watu na wachawi au wanawasiliana na miungu kutokana na 'watu wa kawaida' kushindwa kun'gamua inawezekanaje mtu wa kawaida kuja na majibu/teknolojia/elimu tata namna hiyo.

Chimbuko la tafakuri ni wazo, na zao la tafakuri ni ubunifu au ugunduzi 'uvumbuzi'
 
Parallel inawezekana. Kama njia tunazotumia hazikutani au kugusana sehemu yoyote, hizo ni parallels.

Misingi ya vipimo na imani huwa haikutani. Huwezi abudu halafu umalize uchungulie telescope au microscope kumtafuta huyo mungu. Mwisho wa siku either una amini au unajua. Huwezi kuunganisha vyote. Ukijua kitu huhitaji tena kuamini. Imani haina msaada kwenye taaluma au ujuzi wowote.

Mimi na wewe tuko parallel kwa msingi huo. Wewe mtu wa imani wakati mimi mdadisi. Nahoji kila kitu hadi uhalisia wa hizo imani. Sijajiwekea mpaka. Siwezi kuabudu kitu nisichoelewa. Hata iwapo moja ya aina nilizopata kuona kuhusu mungu ni kweli bado sitoabudu. Zote zimejaa ujinga. Mambo ya kale. Mimi sio mtu wa kale. Pamoja na kupitwa na wakati nahisi kuna watu walihoji hata kipindi hicho. Walikuwa imara kukataa ujinga. Kuabudu ni udhaifu ambao nitajionea aibu kufanya. Kuna wanaona ufahari kuabudu sio mimi. Utumwa, uvivu, ujinga, upotevu wa muda kwa zoezi lisilo na faida.... itoshe kusema bongo zetu ziko tofauti.

Unaonyesha viashiria vyote vya superstitious mentality kama unavyoweka jina la kitu unachoabudu kwa herufi kubwa. Kwanini usiweke herufi kubwa pale tu kuashiria unaanza sentensi mpya. Hiyo itakuwa sababu yenye maana zaidi. Nadhani utakuwa unajaribu kuonyesha heshima kwa hiko kitu. Heshima ya utani. Binafsi naona ni upuuzi.

Naweza nikakuheshimu kama mtu japo una mawazo nayojua ni imani potofu. Imani yako hiyo ni sehemu ndogo ya utu wako. Unaweza kuwa mtu mwema na hodari kwenye mambo mengine ya msingi. Kwani unadhani hakuna wataalamu wanaoamini hizo imani? Wanaheshimika kwenye field zao lakini inapokuja kwenye imani nao dhaifu. Kuheshimu imani zao itakuwa unafiki. Tunavumiliana tu sio kuheshimu imani yenyewe. Hata ikisemwa tunaheshimu imani, ukweli ni kwamba kauli hii ya "kisiasa" ina maana tunaheshimu watu wanaoamini ujinga fulani maana wao ni zaidi ya ujinga wao huo mmoja. Binafsi tunajua hatuwezi kufata ujinga wao ila mambo mengine ya msingi tutashirikiana.

Sijui umenielewa au tumeenda parallel tena? Nimejitahidi kuandika namna utakayoelewa Synonym.

"Science without religion is lame, religion without science is blind" - ALBERT EINSTEN
 
Misingi ya vipimo na imani huwa haikutani. Huwezi abudu halafu umalize uchungulie telescope au microscope kumtafuta huyo mungu. Mwisho wa siku either una amini au unajua. Huwezi kuunganisha vyote. Ukijua kitu huhitaji tena kuamini. Imani haina msaada kwenye taaluma au ujuzi wowote.

Mimi na wewe tuko parallel kwa msingi huo. Wewe mtu wa imani wakati mimi mdadisi. Nahoji kila kitu hadi uhalisia wa hizo imani. Sijajiwekea mpaka. Siwezi kuabudu kitu nisichoelewa. Hata iwapo moja ya aina nilizopata kuona kuhusu mungu ni kweli bado sitoabudu. Zote zimejaa ujinga. Mambo ya kale. Mimi sio mtu wa kale. Pamoja na kupitwa na wakati nahisi kuna watu walihoji hata kipindi hicho. Walikuwa imara kukataa ujinga. Kuabudu ni udhaifu ambao nitajionea aibu kufanya. Kuna wanaona ufahari kuabudu sio mimi. Utumwa, uvivu, ujinga, upotevu wa muda kwa zoezi lisilo na faida.... itoshe kusema bongo zetu ziko tofauti.

Naweza nikakuheshimu kama mtu japo una mawazo nayojua ni imani potofu. Imani yako hiyo ni sehemu ndogo ya utu wako. Unaweza kuwa mtu mwema na hodari kwenye mambo mengine ya msingi. Kwani unadhani hakuna wataalamu wanaoamini hizo imani? Wanaheshimika kwenye field zao lakini inapokuja kwenye imani nao dhaifu. Kuheshimu imani zao itakuwa unafiki. Tunavumiliana tu sio kuheshimu imani yenyewe. Hata ikisemwa tunaheshimu imani, ukweli ni kwamba kauli hii ya "kisiasa" ina maana tunaheshimu watu wanaoamini ujinga fulani maana wao ni zaidi ya ujinga wao huo mmoja. Binafsi tunajua hatuwezi kufata ujinga wao ila mambo mengine ya msingi tutashirikiana.

EINSTEIN ni mwanasayansi 'mdadisi' mkubwa kuliko wote katika karne ya 20 na alikuwa akiamini uwepo wa Mungu 'mtu wa imani'

Sasa mwenzangu na mimi kutoka Bonyokwa Nangulukuru sijui hoja zako huwa unaziokotea kwenye jalala gani

Ni kana kwamba huwezi kueleza jambo bila kudhihirisha ufahamu wako mbovu wa mambo au udhaifu wa upeo wako
 
Hakuna ambaye analipuka ghafla tu na liukweli fulani ambalo halina mashiko na kulifanya ndio mwisho mbona awe scientist au religionist. Kila mmoja anakuwa amemake observation halafu ndiyo anaanza ku make sense ya alichokiona, mwishowe anatengeneza nadharia zake halafu anazifanyia kazi na anafikia hitimisho kulingana na uwezo uliopo.

Wewe unajuaje kama watu wa kiroho hatujafikia hitimisho husika kwa njia ileile inayofuatwa na wanasayansi. Dini nyingi za asili mwanzo wake ulikuwa hivyo na ukadumu hivyo kwa miaka mingi hadi baadaye ufunuo ulipowasaidia kufikia viwango vya juu zaidi. Waliangalia miti, wanyama na wao na wakagundua hawakuvitengeneza wao wakadeduce atakuwepo mkubwa zaidi aliyevileta hivyo. Wakaishia kuhisi mawe makubwa, milima au miti itakuwa kama sio mungu basi ina uhusiano na Mungu. Walihitaji mafunuo ili kujua asili halisi ya Mungu ila haikubadilisha ile essense ya ukweli waliokuwa nao kwamba yupo Mwenyezi Muumbaji na Mjuzi.

Njia nyingine nayo inatumika 'armchair thinking' ni mtu anaimagine au anaambiwa ukweli fulani halafu anaanza kuutafutia observation. Hii kwenye dini tunaita ufunuo na kwenye mambo ya kiroho umetawala kwa sababu tunayemtumainia ni mkubwa kuliko sisi na mjuzi kuliko sisi. Na kwenye sayansi ni level ya majiniazi; unabisha? hebu niambie kama huyu jamaa aliongea madini au aliboronga?;

“The formulation of a problem is often more essential than its solution, which may be merely a matter of mathematical or experimental skill. To raise new questions, new possibilities, to regard old problems from a new angle requires creative imagination and marks real advances in science.”

Kitu cha kuzingatia ni kimoja uaminifu na ukweli. Njia ya kwanza mara nyingi inakuwa salama maana unapata fact unazichambua unazifuata ndio mwisho unajenga conclusion. Njia ya pili yenyewe you start with an end in mind. So ina risk hiyo end/conclusion yako ikawa right au wrong. Ukiwa sio muaminifu utaanza kuzitafuta fact ukakumbatia zinazosapoti ukareject zisizosapoti tunaita bias. Ukiwa muaminifu na mkweli utapata tu majibu, ya kweli utafurahia umegundua, ya uongo utafurahia umegundua kumbe ni uongo! Hii njia ya pili kwa kuwa ina risk, iko na raha sana maana ni real adventure!

Imagination advances science while observation perfects it[emoji109]. And both kinds of scientists are important, kind of check and balance.
Nimejua mpangilio wa mawazo na masomo ya kiroho kwa kufatilia miaka mingi. Kuna mambo kimsingi yapo kwenye masuala ya imani lakini sio kwenye taaluma za sayansi. Mfano tafsiri na uelewaji wa mambo mengi yanategemea utashi wa mtu na mipaka atakayojiwekea. Hakuna hicho kitu kwenye vipimo vya kisayansi. Hatuwezi kupata maana tofauti kwenye seti moja ya data halafu wote tukawa sawa. Kitu ili kikubalike na kila mmoja lazima kipitie chujio la upinzani na matokeo yawe sawa kwa kila anayepima na kuona majibu. Hali ni tofauti kwenye uzushi na usanii wa mambo ya kiroho. Tutazunguka sana lakini ukweli uko wazi kabisa. Ufunuo ni kitu cha uongo. Cha kutunga. Wengne wameiga. Hiyo deduction ya kuona kitu kama mti na kukadiria tu kuna mungu kaumba ndio uzushi wenyewe. Very wrong and far from scientific thought process.

Essence ya kuamini na kuabudu iko na sababu. Tamaduni zina mchango mkubwa sana lakini pia baiolojia ya miili yetu. Chanzo mwilini kiko kwenye bongo zetu. Kuna kitabu kimeelezea vizuri na kwa urahisi hii pointi kinaitwa "human brain " cha dr. Rita Carter. Simple explanations za kuanzia. So utakuta kwa vile bongo zetu sote zimeundwa kuhitaji kuabudu vitu vya kuongoza maisha yetu kila sehemu duniani kuna hizi imani. Tofauti zinaibuka kulingana na mazingira au muingiliano wa tamaduni.

In any way, imani zote pamoja na kazi zote na hasara zake hazina ukweli ndani yake! Ubunifu una kikomo. Kikomo ni sayansi. U can imagine flying cars au interstellar travel but only scientific and technological advances have the last say. There are multiple times the number of ideas than applicable inventions. However I do agree it is very useful in keeping technicians on there toes to do better each passing day and make improvements. [emoji106]
 
Ni nani aliyekukaririsha kwamba mtu akiwa mwanasayansi au mwanafalsafa ni lazima asiamini uwepo wa Divine Being kwa sababu ni fani zenye misingi tofauti? Eti huwezi kuunganisha vyote, yaani mtu kuwa mwanahistoria au mwanajiografia ndo kumpokonye haki ya kuamini? Nani kakufunza mambo haya, ni viashiria vya fikra limbukeni

Unayejadiliana naye humjui acha kunitengenezea nadharia tete, niweke mimi pembeni ambaye sijadhihirisha wazi wasifu wangu. Uhakika Bro ni mdadisi na pia ni muumini. Kuna jamaa ana username Mpare2 - rejea comments za juu amejidhihirisha wazi kwamba ni mwanasayansi na anaamini uwepo wa Mungu, sasa wewe sijui hilo sharti la kutokuwa mwanasayansi na muumini kwa wakati mmoja sijui umelipatia wapi!

Kwenye maelezo yako umediss ulivyotaka imani kwa ujumla wake, mara ni kale, upuuzi, kuabudu ni kupoteza muda, ni ujinga, upotofu na maneno ya kebehi kibao! Sawa ngoja hayo tuyapokee kwa mikono miwili japo hamna hoja ya msingi uliyojenga dhidi ya imani zaidi ya kuonyesha mitizamo yako hasi inayoishi kwenye kichwa chako. Kwa kuwa unajinadi wewe ni mwerevu sana kuliko watu takribani bilioni 7, mimi sitaidogosha sayansi kwa mitazamo hasi au maneno matupu kama wewe, badala yake nitaweka challenge ndogo sana kukufunza!

Niliwahi kukuuliza sayansi kama fani, unajua madhaifu yake? Ulichezacheza na maneno na hamna cha maana ulichojibu.

Hivi hata katika akili ya kawaida tu, mambo/hali/mienendo/tabia zote zilizopo ulimwenguni au vitu vyote vilivyomo/vinavyotuzunguka vinaweza kuelezwa kwa ufasaha/kweli na kuvielewa kwa kuegemea kwenye fani moja tu ambayo ni sayansi? Hivi kweli fani moja ndo itupe majibu ya mafumbo yote ulimwenguni?

Sayansi kama fani msingi wake mkuu umejijenga kwenye experimentation, sasa ngoja tuone implication ya hiyo approach na udhalili wake kwa mifano kwenye baadhi ya mambo (Challenge I): Uchawi upo au haupo? Unaweza kuthibitisha uwepo wa uchawi kisayansi? Sayansi kushindwa kuthibitisha uwepo wa uchawi ndo kunaufanya uchawi usiwepo?

Challenge II: Tusaidie kufanya utafiti wa kisayansi kuthibitisha uwepo wa akili tambuzi 'consciousness', kwamba ipo au haipo kwa muonekano na sifa zake! Eti uchukue telescope/microscope umchungulie Mungu! Kwa nini usichukue telescope/microscope uichungulie akili?

Tafakuri: Ni kwa nini sayansi ikishindwa kuthibitisha jambo hukimbilia kwenye hitimisho la kutokuwepo kwa hicho kitu! Wakati huohuo kwenye fani yetu yenyewe kuna mambo tunaitakidi yapo na hayathibitishiki lakini tunakomaa kutetea uwepo wake au tunajisahaulisha kama hayo mambo hayapo hivi kwa lengo la kuitakasa fani na madhaifu yake

Halikadhalika, kuna mambo yapo wazi lakini jinsi sayansi inavyoeleza ni kana kwamba imekuwa conflicted, au kuna deficit ya concepts, au concepts zake ni incomplete, hali inayopelekea kutoelewa jambo kwa kina au kupotosha kabisa, nimeona kwenye comment yako hapo chini umemtaja Darwin: sijui ni tahira gani wa karne hii unayeweza kumuelezea nadharia zake za evolution akakuelewa
Kuhusu sharti la kutochanganya taaluma na imani nahisi hujanielewa. Kuna wataalamu wengi tu wenye kufuga hizo imani za mungu kichwani. Nilichojaribu kuelezea ni kwamba mtu huyo mwenye hizo imani hawezi kuziingiza kwenye taaluma. Kufanya hivyo anakuwa ameshindwa kutimiza wajibu kitaaam. Imani na taaluma haviendi pamoja hata nukta moja ya muda. Ukichanganya tu umeharibu. Ukiwa kwenye meza ya sayansi Fata taratibu mungu weka mbali. Ukirudi kwako piga goti utakavyo au kwenye muda wako wa ziada tembelea hekalu ujumuike na wenzio wa imani sawa na yako. Sijasema haiwezekani kwa injinia au tabibu kuwa na imani. Uzi huu umeanzishwa na mtu anadai ni mwanabaiolojia. Kimantiki inashangaza lakin ndio uhalisia wa kibinadamu. Usinizushie uongo.

Nilikujbu madhaifu ya sayansi ni kama ya fani zingine zisizo za kiimani. Sayansi sio jambo la kiimani lenye udhaifu kuanzia mwanzo ndani yake plus na watu wanaojihusisha nayo. Inabeba tu madhaifu yote ya watu wanaojihusisha nayo pasipo yenyewe kulazimu makosa, madhaifu yote ya binadamu yanatokea kwenye kazi. Huwezi kuuliza muziki una udhaifu gani? Jibu ni rahisi. Kama fani hakuna udhaifu wa kulaumu fani yenyewe. Ila mambo ya wanamuziki ndio yanajenga au kubomoa fani yao.

Kuhusu uchawi ni kweli haupo kiuhalisia. Naandika kiuhalisia nikimaanisha nacho ni kitu ambacho hakina athari kama inavyodhaniwa. Hakuna namna ya uchawi kufanya kazi. Mfano mtu apasue nazi kama kutaka kitu fulani kitokee kama kutoa kitu kingine kisichoelezeka kama mkosi au jini n.k n.k.... wengi wametoa na wanaendelea kutoa ushuhuda kuona uchawi na wachawi. Shida hapa hatuwezi kuamini na kuchukulia rasmi upo kwa ushuhuda pekee. What if huyo mtu alikuwa anapitia hallucination? Kuna illusions nyingi sana kama kuona vitu kwenye giza, vivuli kuhisi ni vitu hai... utapokea vipi kitu bila uhakika nacho? Bila shaka huwezi pasipo uhakika. Maisha yote kwanini sijarogwa au kuona uchawi? Basi tuseme tusioamini huo ujinga wachawi hutuacha salama hawatuchezei au kututoa misukule. Siku ushahidi wa uchawi utakuwa wazi kila mtu atapokea hayo mambo bila ubishi na kufatilia namna yatasaidia maisha yake. Sayansi haiwezi kukataa mambo ya uchawi kwa vile sio kazi yake kukataa au kukubali bali kuchunguza ukweli wake. Kama hamna ushahidi hakuna la kuongeza zaidi ya kusema hamna uthibitisho wa kitu uchawi unaoongelewa. Usilazimishe kitu kisicho na ushahidi wa moja kwa moja kikubalike tu ili kiendane na kinachodaiwa kwenye jamii. Kukosa ushahidi ni hoja tosha kusema hakuna uchawi.

Kwenye fani za neuroscience bado consciousness ni suala mtambuka. Ni hivi karibuni tu kumeanza kuwa na vifaa kama mashine ya nuclear magnetic resonance imaging, PET scan vya kuusoma na kuupima ubongo moja kwa moja ili kuuelewazaidi. So hata ukimuuliza mtaalamu consciousness iko sehemu gani hutopata jibu. Hasa atasema bado haijulikani eneo hilo. Sayansi sio dini. Haisemi inajua kila kitu na uiamini tu. Inaelewa na kuweka wazi kikomo cha uelewa kilichofikiwa. Kinasogea kila siku, ni suala la muda tu. Consciousness itaeleweka zaidi ya sasa. Kuna vingi vilikuwa havijulikani siku za nyuma.

Kuhusu Darwin mtu atakeweza kuelewa dhana alizoanza kuzigundua ni mwenye akili wazi inayoweza kupokea mambo yasiyo dhahiri kwa haraka. Kama una akili iliyojifungafunga kiasi kwamba ukiambiwa viumbe vyote vinamauhisiano unashindwa kuelewa lazima akupe shida. Ukisikia sokwe, tumbiri, sisi, binadamu wa kale na primates wote tuna chanzo kimoja lazima ukimbilie kutoelewa na kudhani tulizaliwa na viumbe waliopo hivi sasa!
 
Wewe ni nani wa kunipangia mimi namna ya kuandika hicho kitu unachodai? Naonyesha - sionyeshi hili niachie mimi na nafsi yangu, huwezi kunijua, tosheka na hilo

Mbona mimi sijawa wa kwanza kuibuka na hoja kama hii isiyo na kwato wala ngozi? Uandishi wako wa herufi ndogo unanisaidia nini au unanipunguzia nini? Nimeona unaandika hivyo na nimeheshimu na sijatuhumu chochote, umekosa hoja za msingi za kujadili hadi uibuke na hili?

Eti hiko kitu! Kitu gani? Nukuu "Jina la kitu unachoabudu", Kumbe ulipokuwa unaandika kitu ulikuwa unakusudia MUNGU? Sasa tangu lini Mungu akawa Kitu? [emoji848]. Unapoelekea si pazuri "upuuzi" "utani" "kitu" "unachoabudu", ulichotaka kuandika hapo nimekielewa, kama umeshindwa kuheshimu imani za wengine basi jiheshimu mwenyewe

Sijapata kujadiliana na mtu wa mrongo wako mwenye ufahamu finyu kama wewe, yaani [emoji2960] - nipumzishe tu, endelea kujadiliana na wengine
Kama sio kitu ni nini sasa🥱
 
"Science without religion is lame, religion without science is blind" - ALBERT EINSTEN
Nakubali. Kuna motivation fulani hivi ya ziada inasukuma kufatilia zaidi haya mambo asilia ili kukimbia upuuzi wa imani potofu kama mambo hayo ya mungu!
 
EINSTEIN ni mwanasayansi 'mdadisi' mkubwa kuliko wote katika karne ya 20 na alikuwa akiamini uwepo wa Mungu 'mtu wa imani'

Sasa mwenzangu na mimi kutoka Bonyokwa Nangulukuru sijui hoja zako huwa unaziokotea kwenye jalala gani

Ni kana kwamba huwezi kueleza jambo bila kudhihirisha ufahamu wako mbovu wa mambo au udhaifu wa upeo wako
Unaelewa aina ya mungu aliyedhaniwa kuwepo na Einstein au unaanza kuropoka?
 
Kuhusu sharti la kutochanganya taaluma na imani nahisi hujanielewa. Kuna wataalamu wengi tu wenye kufuga hizo imani za mungu kichwani. Nilichojaribu kuelezea ni kwamba mtu huyo mwenye hizo imani hawezi kuziingiza kwenye taaluma. Kufanya hivyo anakuwa ameshindwa kutimiza wajibu kitaaam. Imani na taaluma haviendi pamoja hata nukta moja ya muda. Ukichanganya tu umeharibu. Ukiwa kwenye meza ya sayansi Fata taratibu mungu weka mbali. Ukirudi kwako piga goti utakavyo au kwenye muda wako wa ziada tembelea hekalu ujumuike na wenzio wa imani sawa na yako. Sijasema haiwezekani kwa injinia au tabibu kuwa na imani. Uzi huu umeanzishwa na mtu anadai ni mwanabaiolojia. Kimantiki inashangaza lakin ndio uhalisia wa kibinadamu. Usinizushie uongo.

[emoji848]

Unajaribu kukimbia kivuli chako, ukifanikiwa nifahamishe nikutunze, maelezo yako ya awali yapo wazi, na hilo umelionyesha mara nyingi zaidi ulipokuwa ukijadiliana Uhakika Bro kuliko hata mimi "ulikuwa wamshangaa na kumuona mtu duni sana kuwa muumini na pia kuwa mwanabaiolojia", na kwenye maelezo yako ulijikita kadri uwezevyo kumthibitishia kwamba anachoamini haimpasi kuamini sababu eti ni mwanasayansi, sasa unachojaribu kukana ni nini? Kujua kugeuzageuza maana ya sentensi na maneno siyo kujua kujenga hoja
 
Nilikujbu madhaifu ya sayansi ni kama ya fani zingine zisizo za kiimani. Sayansi sio jambo la kiimani lenye udhaifu kuanzia mwanzo ndani yake plus na watu wanaojihusisha nayo. Inabeba tu madhaifu yote ya watu wanaojihusisha nayo pasipo yenyewe kulazimu makosa, madhaifu yote ya binadamu yanatokea kwenye kazi. Huwezi kuuliza muziki una udhaifu gani? Jibu ni rahisi. Kama fani hakuna udhaifu wa kulaumu fani yenyewe. Ila mambo ya wanamuziki ndio yanajenga au kubomoa fani yao.

Hey, hatupo kwenye siasa, jibu unachoulizwa 'taja', hili si darasa la siasa! hivi we jamaa una shida gani? yaani uulizwe ni yapi mapungufu ya fani ya takwimu, udai takwimu kama fani haina mapungufu bali watakwimu na wanaojihusisha na fani ya takwimu kama wanadamu ndo wana mapungufu, hii akili ndo huwa unaitumia kuvuka barabara?

Takwimu kama fani ina madhaifu au mapungufu yafuatayo:
  • Haielezi phenomenom ambazo ni qualitative
  • Haielezi stori nzima "takwimu hueleza mambo kwa muhtasari"
  • Takwimu ni fani isiyodili na figure moja kwa mfano: uzito wa mtu X
Kinachokushinda kueleza kama hivyo ni nini? Eti sayansi siyo jambo la kiimani, mara sijui muziki kama fani hauna madhaifu! Nani kakwambia hauna? Tuhamie kwenye music?

Najua fika kinachokufanya ukwepe kutaja udhaifu wa fani ya sayansi, endelea kuzunguka mbuyu hivyohovyo, la sivyo utaivua fani nguo na baadhi ya angle zitabaki tupu, kukwepakwepa hivyo ni salama kwa misingi yako batili
 
Kuhusu uchawi ni kweli haupo kiuhalisia. Naandika kiuhalisia nikimaanisha nacho ni kitu ambacho hakina athari kama inavyodhaniwa. Hakuna namna ya uchawi kufanya kazi. Mfano mtu apasue nazi kama kutaka kitu fulani kitokee kama kutoa kitu kingine kisichoelezeka kama mkosi au jini n.k n.k.... wengi wametoa na wanaendelea kutoa ushuhuda kuona uchawi na wachawi. Shida hapa hatuwezi kuamini na kuchukulia rasmi upo kwa ushuhuda pekee. What if huyo mtu alikuwa anapitia hallucination? Kuna illusions nyingi sana kama kuona vitu kwenye giza, vivuli kuhisi ni vitu hai... utapokea vipi kitu bila uhakika nacho? Bila shaka huwezi pasipo uhakika. Maisha yote kwanini sijarogwa au kuona uchawi? Basi tuseme tusioamini huo ujinga wachawi hutuacha salama hawatuchezei au kututoa misukule. Siku ushahidi wa uchawi utakuwa wazi kila mtu atapokea hayo mambo bila ubishi na kufatilia namna yatasaidia maisha yake. Sayansi haiwezi kukataa mambo ya uchawi kwa vile sio kazi yake kukataa au kukubali bali kuchunguza ukweli wake. Kama hamna ushahidi hakuna la kuongeza zaidi ya kusema hamna uthibitisho wa kitu uchawi unaoongelewa. Usilazimishe kitu kisicho na ushahidi wa moja kwa moja kikubalike tu ili kiendane na kinachodaiwa kwenye jamii. Kukosa ushahidi ni hoja tosha kusema hakuna uchawi.

Nijibu kwa kifupi tu kwamba, una shida kubwa mno ya uelewa, maelezo yako ya mwanzo yanakiri na kusadikisha ushahidi unaotolewa na watu wengi kuhusu uchawi halafu mwisho unakama kwa hoja inayopingana na hiyo ya mwanzo ya kukosekana kwa ushahidi, ulikuwa unatengeneza statement of the problems e? What if huyo mtu! Siyo wewe uliyesema "watu wengi", au ulisa

Eti uchawi haupo kwa sababu hauna athari kama unavyodhaniwa! Hili si suala la kudhani, Ebo! Wala siyo suala la kukosekana kwa athari, ni hali ambayo kwa 100% ipo na hatuhitaji sayansi ituthibitishie kuwepo au kutokuwepo kwake, sayansi haina uwezo huo, sayansi ina udhaifu mkubwa katika kushindwa kuyatambua/kuyaeleza/kuyakubali/kuyabaini baadhi ya mambo ambayo ni halisi 'reality' na kukimbilia kwenye hutimisho la kutokuwepo kwa hayo mambo! Na nilijua ni lazima utajificha humo ndo maana kwenye maelezo yangu ya mwanzo sikusita kueleza

Eti utapokeaji kitu bila uhakika nacho, unahitaji uhakika gani? Mambo mangapi kwenye sayansi tumefundishwa na tumeyapokea na hatuna uhakika nayo? Na siyo kuwa na uhakika nayo tu bali mengi hayapo kabisa, au yapo kama idea tu lakini hayatahibitishiki kwa kutumia milango ya fahamu wala majaribio, au hatuna uhakika nayo wala hatuna uhakika juu ya uwepo wa hayo. Ulishawahi kuhakiki uwepo wa Moles au Atoms? Ulihakikije? Wapi ulishawahi kuhakiki uwepo wa hewa au upepo? Ulihakikije? Ulishawahi kuiona hewa au una-experience tu? Wapi ulishawahi kuhakiki uwepo wa latitude na longitude? Uache unafiki, mambo kibao tumemezeshwa tu pasina uhakiki wowote na tumeyapokea kwa upofu pasina hata kuthubutu kufanya uchunguzi. Ushauri: Unapokuwa unajenga hoja yoyote kumbuka kuanzia kwenye sayansi, weka hilo akilini, kama zipo lakini

Eti huo ujinga! Ita hiyo phonemena vyovyote utakavyo, hilo halibadilishi chochote wala haliondoshi chochote
 
Nilikujbu madhaifu ya sayansi ni kama ya fani zingine zisizo za kiimani. Sayansi sio jambo la kiimani lenye udhaifu kuanzia mwanzo ndani yake plus na watu wanaojihusisha nayo. Inabeba tu madhaifu yote ya watu wanaojihusisha nayo pasipo yenyewe kulazimu makosa, madhaifu yote ya binadamu yanatokea kwenye kazi. Huwezi kuuliza muziki una udhaifu gani? Jibu ni rahisi. Kama fani hakuna udhaifu wa kulaumu fani yenyewe. Ila mambo ya wanamuziki ndio yanajenga au kubomoa fani yao.

Kuhusu uchawi ni kweli haupo kiuhalisia. Naandika kiuhalisia nikimaanisha nacho ni kitu ambacho hakina athari kama inavyodhaniwa. Hakuna namna ya uchawi kufanya kazi. Mfano mtu apasue nazi kama kutaka kitu fulani kitokee kama kutoa kitu kingine kisichoelezeka kama mkosi au jini n.k n.k.... wengi wametoa na wanaendelea kutoa ushuhuda kuona uchawi na wachawi. Shida hapa hatuwezi kuamini na kuchukulia rasmi upo kwa ushuhuda pekee. What if huyo mtu alikuwa anapitia hallucination? Kuna illusions nyingi sana kama kuona vitu kwenye giza, vivuli kuhisi ni vitu hai... utapokea vipi kitu bila uhakika nacho? Bila shaka huwezi pasipo uhakika. Maisha yote kwanini sijarogwa au kuona uchawi? Basi tuseme tusioamini huo ujinga wachawi hutuacha salama hawatuchezei au kututoa misukule. Siku ushahidi wa uchawi utakuwa wazi kila mtu atapokea hayo mambo bila ubishi na kufatilia namna yatasaidia maisha yake. Sayansi haiwezi kukataa mambo ya uchawi kwa vile sio kazi yake kukataa au kukubali bali kuchunguza ukweli wake. Kama hamna ushahidi hakuna la kuongeza zaidi ya kusema hamna uthibitisho wa kitu uchawi unaoongelewa. Usilazimishe kitu kisicho na ushahidi wa moja kwa moja kikubalike tu ili kiendane na kinachodaiwa kwenye jamii. Kukosa ushahidi ni hoja tosha kusema hakuna uchawi.

Nijibu kwa kifupi kwamba: si kila phenomenon ambayo ni halisi "reality" sayansi inaweza kuichunguza, kuielezea na kuitolea hitimisho la kweli
 
Kwenye fani za neuroscience bado consciousness ni suala mtambuka. Ni hivi karibuni tu kumeanza kuwa na vifaa kama mashine ya nuclear magnetic resonance imaging, PET scan vya kuusoma na kuupima ubongo moja kwa moja ili kuuelewazaidi. So hata ukimuuliza mtaalamu consciousness iko sehemu gani hutopata jibu. Hasa atasema bado haijulikani eneo hilo. Sayansi sio dini. Haisemi inajua kila kitu na uiamini tu. Inaelewa na kuweka wazi kikomo cha uelewa kilichofikiwa. Kinasogea kila siku, ni suala la muda tu. Consciousness itaeleweka zaidi ya sasa. Kuna vingi vilikuwa havijulikani siku za nyuma.

Hongera, hili umejibu vizuri kiasi. Sayansi kushindwa kutambua akili ilipo hakuifanya akili iwepo au isiwepo, na hili linagutusha kwamba si kila ambacho sayansi inashindwa kulitolea ufafanuzi hitimisho ni kutokuwepo kwake

Na hilo linagutusha zaidi kwamba kuna phenomenon ambazo ni superior kwa sayansi na akili ni moja wapo, kama sayansi imeweza kuelezea unobservable mystical phenomenon kama atoms na subatoms, inashindwaje kueleza akili ambayo ni innate unobservable qualitative phenomenon?

Ahsante sana, kwa mara ya kwanza umedhihirisha udhaifu wa sayansi hapo ulipoandika "Sayansi haisemi inajua kila kitu", ama kusuhu dini kujua kila kitu hilo sijui umelipatia wapi? Hamna dini inayofundisha hivyo, acha kulisha imani za watu maneno ya uongo

Sasa huo udhaifu wa sayansi ulioutaja hapo ndo phenomena kama JUJU "Uchawi" zinaingia ndani yake. Najua fika kwamba unajua udhaifu wa sayansi japo unajifanya kujificha chini ya kivuli cha dole gumba lako. Sayansi kushindwa kujua kila kitu hakuyafanyi mambo yasiyojulikana na sayansi yawepo au yasiwepo [emoji4]. Nachokupendea huwa unarukaruka wee halafu baadaye unajifunga mwenyewe

Niweke wazi katika maelezo yako yote uliyowahi kuandika, hichi kipengele umeonyesha ukomavu wa ufahamu, umekitendea haki kwa kiasi chake, doa chafu: kuchanganya maelezo kwa kutuhumu dini kujua kila kitu
 
.

Kuhusu Darwin mtu atakeweza kuelewa dhana alizoanza kuzigundua ni mwenye akili wazi inayoweza kupokea mambo yasiyo dhahiri kwa haraka. Kama una akili iliyojifungafunga kiasi kwamba ukiambiwa viumbe vyote vinamauhisiano unashindwa kuelewa lazima akupe shida. Ukisikia sokwe, tumbiri, sisi, binadamu wa kale na primates wote tuna chanzo kimoja lazima ukimbilie kutoelewa na kudhani tulizaliwa na viumbe waliopo hivi sasa!

Achilia tusiojua kusoma wala kuandika ambao kwa wewe unatuona hatuna akili, ni wanasayansi wangapi wakubwa kwa wadogo, wasasa na wakale wamezikosoa vibaya mno nadharia zake za evolution? Hao wanasayansi hawana akili? Wewe ndo una akili sana e? Unachojaribu kufunikafunika na kupakapaka mafuta hapo ni nini?

Huu utahira wa Darwin endelea kujadiliana na wanafunzi wa darasa la kwanza D, tena wale wasio na mtaala wa Montessori, japo hata wao watakuona dishi limeyumba
 
Mungu yupo na ataendelea kuwepona anaepiga uwepo wa Mungu anamattzo ila Yesu na Mohammad hao hawapo na hao ndo utapeli unapoanzia na apo ndo ugomvi huanzia
 
Nakubali. Kuna motivation fulani hivi ya ziada inasukuma kufatilia zaidi haya mambo asilia ili kukimbia upuuzi wa imani potofu kama mambo hayo ya mungu!
?

Ukubali ukatae sisi haituhusu, wewe kuona jambo fulani ni upuuzi hakulifanyi hilo jambo kuwa ni upuuzi. Na huo ufahamu ulioupata kwenye quote ya Einstein ni wewe na akili zako za kukodisha tu, kwa sisi ambao tunamsoma na kumuelewa Einstein tunajua amemaanisha nini alipohusisha hayo mambo mawili 'uhusiano'
 
Unaelewa aina ya mungu aliyedhaniwa kuwepo na Einstein au unaanza kuropoka?
Hilo halijalishi! Eti "dhana", unataka kuthibitisha nini? Iwe ni dhana au ni yakini sisi hilo halituhusu, hayo ni mambo yanayoishi kwenye moyo na fikra za mtu sisi hatuwezi kuyajua, hoja ni kwamba "ALBERT EINSTEIN NI MWANASAYANSI NA ALIAMINI MUNGU YUPO". Sasa je ni Mungu yupi na mwenye sifa zipi? Mjadala wetu haukuwa sifa za Mungu, mada ilikuwa "kuamini au kutoamini uwepo wa Mungu kwa wanasayansi". Kwa kifupi tu ni kwamba mjadala wetu wa awali umeishia hapo na imejitosheleza, yafuatayo ni nyongeza tu

Najua umeuliza hivyo kwa sababu umesoma maelezo machache ambayo Einstein alinukuliwa aliposema anaamini Mungu wa mwanafalsafa Spinoza. Kwa upeo wako finyu utakuwa umesoma sifa chache za huyo Mungu kama makala nyingi zilivyonukuu na umebweteka badala ya kutafuta marejeo halisi ya Spinoza alipojaribu kueleza sifa za Mungu wake. Nikufumbue macho kwamba sifa za Mungu wa Spinoza zinazolandana mno na sifa za Mungu wa Abrahamic Religions kuliko kutofautiana kwake, yaani karibu 65% - 85% ya sifa za Mungu wake alizoeleza zinamsadifu Mungu wa Abrahamu au Mungu wa wengi katika wanadamu

Halafu pia, hivi kuna sehemu au siku uliwahi kuniuliza Mungu wangu ana sifa zipi au ni Mungu gani? Kilichokufanya usiniulize ni nini? Mbona uliendelea tu kujadili uwepo au kutokuwepo kwake? Ni wazi kwamba una utambuzi usiohitajia kuniuliza kujua Mungu wangu ni wa aina gani na ana sifa gani? Ulipoandika "baada ya kuabudu uchukue telescope/microscope umchungulie umuone Mungu" ulikusudia Mungu gani? Ng'ombe au Mwamba? Kwani Miungu hivyo haionekani kwa macho ya nyama hadi utumie hadubini? Ni wazi kwamba ulijua mimi kama theist ni Mungu gani ninayemkusudia na ana sifa zipi kuu

Kwa upeo wako unaona ni jambo linalowezekana wanasayansi/wanafalsafa wote ambao ni theists wakaamini Mungu mwenye sifa zinazofanana kwa 100%? Sasa tunaposema wanasayansi 'theists' wanaamini uwepo wa Mungu huwa tunamaanisha nini? Huwa tunazingatia kufanana kwa 100% kwa sifa za Uungu kwa kila mmoja wao? Au huwa tunakusudia Mungu wa aina gani? Hoja nyingine hata siyo za kuibua, ungekausha tu

Na huenda hujanielewa, ngoja nikukokoteze tena!

Kwani sifa za Mungu aliyeaminiwa kuwepo au kuzungumziwa na Plato au Socrates ndo sifa za Mungu wa Eliyya au Zakaria ?

Je, sifa za Mungu aliyeaminiwa na kuzungumziwa na Faraday au Pasteur ndo sifa za Mungu wa Yesu au Muhammad?

Kwani hata Abrahamic Religions kila dini inayounda hilo kundi inapoelezea sifa za Mungu wao huwa zinafanana kwa 100%?

Ingia ndani kidogo, yaani katika ngazi ya madhehebu ya kila dini, je kila dhehebu linavyoeleza sifa za Mungu wao ndivyo mapote mengine ya dini hiyo yanavyoeleza pasina kutofautiana kukubwa au kudogo?

Shuka katika ngazi ya waumini wa dhehebu moja la kila dini, je kila muumini anayejiegemeza katika dhehebu A au B sifa za Mungu anayemuamini anavyozieleza zinafanana zote na sifa za Mungu wa muumini mwenzake wa dhehebu hilohilo?

Katika kujiuliza hayo maswali bila shaka kuna mambo utakuwa umejifunza ikiwemo hili: ufahamu hutofautiana hata kwa watoto waliotoka kwenye mfuko mmoja wa uzazi, ni mambo ya kawaida watu kutofautiana uelewa kutokana na kutofautiana upeo na daraja la ubobezi wa fani yeyote

Na haswa kwenye hilo kinachozingatiwa ni dhamira ya mlengwa kwa Mungu kwa kubainisha japo sifa zake kuu chache, kukosea au kupatia kumuelezea ni matokeo ya ufahamu tu, na wala hilo haliondoshi kusudi la Mungu wala uwepo wake. Hivi kwani Einstein hata katika sayansi ni vingapi amepatia na vingapi amekosea? Sasa kama yapo hayo kinachokushangaza kwenye hili ni nini na ukizingatia filosofia wala thiolojia si fani zake. Nanukuu maelezo yako "Tafsiri na uelewaji wa mambo mengi yanategemea utashi wa mtu na mipaka atakayojiwekea"
 
Back
Top Bottom