Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

Sayansi haisemi inajua kila kitu

[emoji4]

Kuna mtu kakushurutisha au kakulazimisha kwa mabavu kuandika ulichoandika?

Siyo haisemi tu, sayansi haijui kila kitu na wala haitokuja kujua kila kitu kamwe, kuna mambo chungu mzima yatabakia kuwa ni fumbo kwa wanadamu mpaka mwisho wa dunia, hatuwezi kuuelewa ulimwengu kwa kuchukua maarifa yetu yote kwenye fani moja, na hata mchanganyiko wa fani zote pia bado haitatosheleza
 
Daah pole sana, inaonesha bado upo nyuma kisayansi tu kwa ujumla.

Tuhuma ulizotoa zipo katika kanuni za kikawaida zinazotumika kwa mambo ya kawaida na zinajitosheleza. Zipo chini ya Newtonian classical mechanics. Hapa ndio tutalazimishana umbali, muda na nafasi viwe sawa kwa kila atakayepima.

Lakini kakaa sayansi sasa imeendelea, hatufungwi na hizo kanuni tu. Kunakitu kinaitwa General/specific relativity mambo ya quantum mechanics. Huku bro hatuna yale mambo ya ukipima dakika mbili, basi kila mpimaji naye apime na aseme ni dakika mbili. Huku inaruhusiwa kabisa mtu kuuexperience ukweli wake kutokana na perception zake, na circumstance zake.

Mambo ya kiroho ni mambo advanced na ndio maana kila mmoja anaexperience kulingana na kiwango anachoweza kun'gamua katika hiyo infinity Truth. Uhusiano wa mtu na Mungu ni binafsi japo tunapokusanyika katika makundi makundi tunapata kusaidika zaidi maana; Chuma hunoa chuma.
 
Mungu yupo na ataendelea kuwepona anaepiga uwepo wa Mungu anamattzo ila Yesu na Mohammad hao hawapo na hao ndo utapeli unapoanzia na apo ndo ugomvi huanzia
Ahsante kwa kuunga mkono hoja kuu "Uwepo wa Mungu", ama kuhusu kukadhibisha uwepo wa hao walimu wawili wa hizi dini mbili kubwa kuliko zote ulimwenguni nashauri walau ungekuwa na andiko lenye kusupport madai yako kutoka katika vyanzo vya kihistoria vinavyoaminika, nimeandika neno "walau" kwa kusudi

La sivyo, wanafunzi wa hao walimu tunaweza tukakugeuzia kibao kwa hoja kwamba na wewe haupo wala hujawahi kuwepo, una uhakika gani kwamba wewe upo kweli na si fikra tu au wazo hai? Hujawahi kuwepo kweli, uwepo wako ni kama picha mnato mfano au picha kivuli inayochezeshwa kwenye game, au uwepo wako ni kama 'mirage' yaani mazingazinga "illusion" hujawahi kuwepo kweli, au uwepo wako ni kama robot tu na si mtu halisi, unaweza kututhibitishia uwepo wapo? Thibitisha

Kwani kabla ya hao uliowataja hakukuwa na ugomvi wala utapeli?
 
Nimekidownload, ntaendelea kukisomaga

Na kama ulivyosema inaonesha unaelewa kabisa kwamba; believing in a god is a sane idea. Any human of any culture with normal brain development is predisposed to believe in a certain form of a god. Muumba kwa sababu ya upendo wake aliweka hilo katika mwanadamu ili tujitambue na tumtafute yeye. That is evolution.

Sasa kutokana na ufupi wa akili zetu tukaendaaa hadi tukafikia mahala fulani, tukastack. Basi Muumba kwa sababu ya upendo wake kwetu tena akaona atusaidie kwa kutuongezea mafunuo mbalimbali na vitabu ili tumtambue vizuri zaidi. That is revelation.

Hata huu uzi unachojaribu kusema ni kimoja tu kwamba; wazo la Mungu ni wazo halali kabisa, wala sio kusema sijui ni yupi au yupoje. Hicho tu. Ngoja nitafute muda nione na hicho kitabu chasemaje.
 
Hayo maelezo yake ya lini? Mbona kama yana ustawi mzuri, nimeyapenda

Ila ananitatiza, naona kama akijadiliana na wewe anakuwa na point kuliko akijadiliana na mimi [emoji3]

Au hii imekaaje?
 
Hayo maelezo yake ya lini? Mbona kama yana ustawi mzuri, nimeyapenda

Ila ananitatiza, naona kama akijadiliana na wewe anakuwa na point kuliko akijadiliana na mimi

Au hii imekaaje?
😂😂😂 Alijibu post namba 209, sio moja kwa moja kivile ila najaribu kutumia lugha yake kumuonesha kwa uwazi zaidi mambo anayoyajua na kuyaamini tayari.

Alisema hivi [emphasis mine] "Essence ya kuamini na kuabudu iko na sababu. Tamaduni zina mchango mkubwa sana lakini pia baiolojia ya miili yetu. Chanzo mwilini kiko kwenye bongo zetu. Kuna kitabu kimeelezea vizuri na kwa urahisi hii pointi kinaitwa "human brain " cha dr. Rita Carter. Simple explanations za kuanzia. So utakuta kwa vile bongo zetu sote zimeundwa kuhitaji kuabudu vitu vya kuongoza maisha yetu kila sehemu duniani kuna hizi imani. Tofauti zinaibuka kulingana na mazingira au muingiliano wa tamaduni." - masdinero masproblemas

Naona jamaa ameendelea sana katika kujua the 'HOW' anahitaji sasa kuanza kuongezea na hints zinazopoint kwenye the 'WHY'. Baadaye aunganishe why na how maisha yawe matam zaidi😊
 
Ndio, sio sawa mtu kujitambulisha taaluma ya sayansi halafu aendelee kutoa hoja za kiroho. Ni kuchafua tawi husika. Bora atoe maoni yake binafsi na si kutaka kukuza uzito wa hoja kwa kuongezea sifa za taaluma anayodai kujikita. Kuanza kwa kujitambulisha mimi ni "fulani" ni kutaka kujipa mamlaka zaidi wakati hoja ni dhaifu. Jaribu kuelewa sio kurukia maneno tu.
 
Kumbe we ni mtu wa kukariri... aliyekudanganya qualitative phenomenon haziwezi kuelezwa na takwimu ni nani? Unasikitisha. Everything can be quantified. Tusiende mbali, una mengi ya kujifunza.
 
Unachekesha sana. 100% ulizipimaje? Yaani wewe ni mshirikina wa aina zote kumbe... Imani zimekujaa. Ndio maana nikasema tuko parallel. Mitazamo yako ya kale sana.
 
Inabidi uelewe consciousness ni kitendo sio kitu fulani stationary... observation yake inafanyika mubashara. Mfano kuelewa nini kinakuza imani kichwani mwako inabidi ufungwe sensa ukiwa unaomba, au kama huwa unakemea, kutoa ushuhuda nk.. kila sehemu kichwan hubadilika kulingana na tukio unalofanya au kuwaza. Mambo mengi tayari yanajulikana na mengine mengi yatajulikana. Ramani yote itakamilika. Ni suala la muda na si kwamba imeshindikana. Again, mtazamo wako wa kuegemea beyond scientific knowledge ni wa kale. Badilika, uachane na hizo imani zote potofu.
 
Hakuna mwanasayansi au mtu yoyote mwenye kujua kusoma na kuelewa atabisha kuhusu evolution. Hivi vitu vinavyotokea kila siku kudhihirisha kwamba viumbe vinabadilika kila wakati huyajui? Ina maana unaandika based on past experiences na sio dunia ya leo? Ibuka kutoka pango hilo ulilopo uungane na wenzio. Unless umeridhika na hizo imani zako za uongo. Eti mungu umtumainiae!
 
Unadhani ni mimi tu?[emoji1787] iko hivi, imani uliyonayo wewe hapo sio kila mtu anaifata. Kimsingi kama una dini moja au dhehebu unalofata sijali lolote lile, tofauti yako na watu wasiofata ujinga wowote ni ndogo mno. Umekataa imani zote duniani ukabaki na hiyo moja wakati wengine tumeenda mbele zaidi kukataa zote pamoja na hiyo moja yako. Imani yako ni ujinga kama zingine zote. Tua zigo hilo!

Einstein yawezekana alikuwa deist. Wewe hapo ni theist. Kwa namna kubwa deism ni position ngumu kuhoji zaidi ya kwako wewe theism na mungu wako unayemtumainia. Tusiende mbali sana, kama Einstein alikuwa na imani so what? Unataka wote tufate imani kwa sababu ya mtaalamu mmoja? Tumia akili na ujenge hoja yenye mantiki.
 
Unaongea uongo sana. Tufanye umeshinda. Maneno yako hayawezi kuwa karibu zaidi na uzishi. Nanyanyua mikono juu.
 
"...kwa sababu ya upendo wake aliweka..." seriously?
 
Kwa kuongezea *zimeundwa kupitia evolution (sio mungu)
 
Hayo maelezo yake ya lini? Mbona kama yana ustawi mzuri, nimeyapenda

Ila ananitatiza, naona kama akijadiliana na wewe anakuwa na point kuliko akijadiliana na mimi [emoji3]

Au hii imekaaje?
Ukiwa na misamiati hovyo na maswali ya ajabu unategemeaje maongezi ya maana? Mimi sio mwalimu kukuweka sawa na maneno yako yasiyo na weledi.
 

"Zimeundwa kuhitaji kuabudu" Zimeundwa na nini au na nani? Na kwa nini ziwe na hiyo quality ya kuhitaji kuabudu? Kwa nini zisiwe zimeundwa huru 'free' - kinyume na kuabudu?

Yupo vema kumbe, ni dots chache tu ambazo akifanikiwa kuziunganisha basi kajinasua kwenye mabano, safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…