Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

Jamii forum sio unique. Labda uulize social media imetokea tu? Be serious. Obviously swali halina mantiki. Jamii forum sio chanzo bali matokeo ya mambo mengi tangulizi.

Ni sawa uulize wewe hapo Synonym umeumbwa? Jibu hapana. Wewe sio maalum sana. Ni nakala tu. Tena hata hukupangwa, ni random. Kuzaliwa kwako kuna iterations zisizo na idadi. Kwa upande mwingne na wewe kuzaliwa kwako kumetokea tu. Hakuna formula au ingineering iliyofanyika kukutanisha wazazi wako. Existence yako ni random. Ndio, nilichojaribu kumweleza mwanabaiolojia wetu huko juu. Randomness doesn't mean order isn't inevitable. Kutoka kwenye random pairings zote possible(chaos) wazazi wako wakakutana ukatokea wewe(order). Kuanzisha sijui mambo ya roho, mungu na porojo zingne sio sayansi hiyo.


Life is chaotic. Hakuna outside planning yoyote!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]eti mungu mwenyewe.
 
😂🤣🤣🤣 umenikumbusha situatiom halisi niliyokuwa nayo siku hiyo, unajua bro kuna mambo hayaachiki?. Yaani mfano siku nilichanganyikiwa halafu nikajijua kuwa nimechanganyikiwa halafu nikakataa kwamba sijachanganikiwa bhana mbona nimejua kuwa nimechanganyikiwa? Kwa hiyo nipo sawa japo nimechanganyikiwa kwa wakati huo!! lakini kwa kuwa nalijua hilo wakatinhuohuo then nikahitimisha kwamba sijachanganyikiwa. Ivi ndugu zangu nyie mmeelewa? Ukielewa utakuwa hujaelewa it is a paradox. Kwa hiyo elewa tu kwamba huielewi....

Na mi niliposema kutilia shaka kila kitu nilitaka kufuta vyote kwanza na nilipokwamia ndio nikaamua kuwa haswaa hiyo ndiyo mwamba wa kuanzisha logic zangu. Kujitilia shaka nipo kilikuwa kimojawapo;

Sema sasa katika kuiondoa hiyo 'a priori' ni kwamba unapoamua kuwaza kwamba usiwaze kabisa kama upo, tayari utakuwa unawaza hivyo katika namna hiyo kwa hiyo tayari upo na unawaza. Umeona. In fact niliposhindwa kuacha kuwaza ndio nikagundua kwamba kumbe hiyo ndiyo uhalisia wenyewe wa mimi ni nani. Hivyo ninavyowaza ndio mimi, mimi ni wazo hai.!
 
Kuwaza si lazima uwepo.

Unaelewa hilo?
 
Mimi naamini BILA MASHAKA kuwa Mungu YUPO muweza ya yote
Naamini pia kuwa Mungu ni mmoja tu, hana mshirika, hajazaa wala hajazaliwa na wala hafanani na kitu chochote.
Hata kwa akili ya kawaida tu, mtu hawezi kumdhuru mwenzake bila hatia, Kupindisha kesi kwa sababu ya rushwa, kupunja watu kwenye mizani nk eti iishie hapa??? Lazima ipo siku ya hukumu ambapo haki itatolewa kwa aliye onewa. Na atakayetoa hiyo haki ndio Mungu!
 
Sayansi inakua ndugu sayansi inapanuka. Wala usiwaone wajinga sana wanaoshikilia kauli kama 'And let there be light' wanaweza kuwa wapo mbele sana sema tu hatujapata namna ya kuthibitisha.

Mfano leo tulikuwa tunajadili na mwana anayeipenda fizikia na kuipa kipaumbele. Katika zungumzazungumza akagusia sayansi nzito ya kwamba. Unajua kila kitu unachoona ni physics ni energy hata matter unazoona ni condensed energy.

Nikamwambia unajuaje labda sayansi inaendelea labda baadaye tutagundua kwamba energy ni condensed idea? Sasa mfano siku wakapruvu hivyo huoni kama watu wa and let there be light watakuwa walikuwa mbeleeee saaaaana? Unadhani ni kwa nini kila siku wanasema most of matter is empty space ' What if empty space ni vile tu hatuwezi kuipima [hatudetect]idea?
 
Kuwaza si lazima uwepo.

Unaelewa hilo?
Hiyo nitasema hapana.

Kuwaza ndiyo kwamba upo

Na kama leo umekubali kuwa kuwaza sio lazima [mwili] uwepo [maana nahisi uwepo wako ni huu mwili ndio unachukulia uwepo halisi]. Basi jua kwamba umekubaliana na ukweli kwamba sisi ni zaidi ya miili yetu.

Fafanua kauli yako kabla sijaendelea, nisije kuwa najenga logic katika premise hewa. Mr Kiranga ulimaanisha nn kusema kuwa kuwaza si lazima uwepo?
 
Asanye sana ndugu Synonym haya mambo kusaidiana. 👊👊
 
Condensed idea kivipi?
 
Condensed idea kivipi?
I did not clai..... sikuwahi kujitapa kuwa ninafahamu ni kiaje? Imetoka tu kama food for thought

We fikiria maada ilivyo tafauti hivyo na nishati. Na jinsi ambavyo mada kidogo inavyotokeza nishati kubwa kinyama!!
Ukitumia analojia na kusema ona jinsi ambavyo wazo lilivyo tofauti na nishati. Na jinsi ambavyo wazo moja lilivyotokeza nishati kuuuuubwa ajabu. Hapo mwanzo unaambiwa ule mwanga na pure energy ilikuwa na joto la matrilionimatrilioni. Na kulikuwa hata hamna maada kabla[sijui hilo joto lilijiexpress vipi asee] na saizi yake hata ka mpira ka kitenesi ni kakubwa!! Mazee naipenda analogy inaleta majibu hapohapo😂🤣🤣. Sijasema huu ndio ukweli lakini deep down nahisi this is the reality.
 
Mimi nimesoma Physics vizuri tu ( na bado nasoma) hivyo sijaona cha ajabu na watakao weza kubadilishwa mawazo kwa haraka ni wale ambao hawajasoma Physics wanaofuata mkumbo. Nina hundreds of theory, lakini hakuna hata moja inaweza kukupa asili ya hivi vitu vyote vilivyopo duniani zaidi ya blaa blaa nyingi ambazo hazi connect! I have no dought kabisa kuwa kuna nguvu kubwa Sana inamanage hivi vitu vyote na ndio hiyo inaitwa Mungu
 
Safi sana, maana huo ndio ukweli

Kuna watu wanakimbilia tu kutudisi tunaokubaliana hivyo eti 'oooh, wavivu wa kufikiri, mnatafuta majibu rahisi kwamba Mungu alisema'

Wakati kumbe wasomi wanaosoma na kuchunguza mambo wanafikia kukubali uwepo wa nguvu kubwa inayomanage vitu. Akili kubwa sana ilifanyiza haya tunayoyaona leo kwa kusudi.
 
Kwa nini kuwaza kusiwezekane bila kuwepo?
 
Kwa nini kuwaza kusiwezekane bila kuwepo?
Nenda kafanye tahajudi kuhusiana na hii kauli, na ile ya kwanza ya 'Kuwaza si lazima [mwili] uwepo. Unaelewa hilo?'

Usiniulize mimi, jiulize mwenyewe maana tunajaribu kujua sisi ni akina nani/nini hapa kabla hatujaendelea kumtafuta Mungu
 
Nenda kafanye tahajudi kuhusiana na hii kauli, na ile ya kwanza ya 'Kuwaza si lazima [mwili] uwepo. Unaelewa hilo?'

Usiniulize mimi, jiulize mwenyewe maana tunajaribu kujua sisi ni akina nani/nini hapa kabla hatujaendelea kumtafuta Mungu
Hujajibu nilichouliza.

Kwa nini isiwezekane kuwa wewe haupo, ila kuna wazo la wewe kuwaza upo?
 
Jamii forum sio unique. Labda uulize social media imetokea tu? Be serious. Obviously swali halina mantiki. Jamii forum sio chanzo bali matokeo ya mambo mengi tangulizi.

Nikuweke wazi tu: una changamoto ya uelewa, unachagua kumuelewa mtu utakavyo na si alivyokusudia, nimesoma comment zako chache tu, hii ni mara ya pili unafanya hivi, ngoja nijaribu kueleza tena labda awamu hii utaelewa

JF kuwepo kumetokana/kumesababishwa na nini? Kuna kilicho nyuma ya uwepo wake "mfano: waasisi au imetokea tu kusikojulikana"? Haijalishi ni ya kwanza kuwepo, ya pili, ya mwisho au ya ngapi

Syntax za JF zilijitengeneza zenyewe? au yupo aliyezi-process akazi-execute ndo JF ikawepo? Jinsi JF inavyo-operate imetokea tu yenyewe? Hamna set ya commands wala codes ambazo ni instructions zilizo nyuma yake? Je hizo codes/commands zimetokea tu au zimeandaliwa?

Eti JF siyo unique, kutokuwa unique au kuwa unique ndo kumeifanya JF itokee au isitokee yenyewe? Halafu unathubutu kuandika 'swali halina mantiki', unafahamu nini kuhusu mantiki? Tuhamie huko?

Nimesoma nilicho-quote tu kimenitosha kukuelewa, hata ulichoandika chini yake sijasoma na sitasoma, kama utangulizi tu umejaa ufahamu mbovu hivi naamini huko chini hakuwezi kuwa salama
 
Hujajibu nilichouliza.

Kwa nini isiwezekane kuwa wewe haupo, ila kuna wazo la wewe kuwaza upo?
Hilo wazo unalozungumzia ndio mimi, kwa hiyo likiwepo tu na lipo hai [linawaza] basi mimi ndimi.
 
Hujajibu nilichouliza.

Kwa nini isiwezekane kuwa wewe haupo, ila kuna wazo la wewe kuwaza upo?
Na unavyopenda kuwauliza wengine, na tunakujibu vizuri mno na vingine unajibu mwenyewe? Japo wewe kujibu naona unapiga chenga sana.

Nakushauri ujitahidi umeditate upate majibu ya haya maswali;

2. Je inawezekana kuwaza na mimi nikiwa sipo? Inawezekanaje kwani mimi ni nani/nini?

1. Sisi ni nani/nini, yaani tunaposema mtu tunamaanisha mtu hasa ni nani/nini?

Lililo bold tunaomba majibu wana JF wote tulione.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…