Mimi ni mwanaume ninayeonewa na mke wangu, Dkt. Gwajma nisaidie

Mimi ni mwanaume ninayeonewa na mke wangu, Dkt. Gwajma nisaidie

Wasalamu.

Nilioa mke wangu 2017 ila kukawa na mwanajeshi anamdanganya mke wangu.Mimi ni mwalimu kipato changu ni duni ikafikia hatua mke wangu kamtoa mtoto shule.

Natamani kujiua ila naomba waziri wa ustawi wa jamii Dorothy Gwajma nisaidie.

.Ni mwalimu Wilaya ya Babati shule Ngolei. Ni mwanaume ninayenyanyaswa. Nimelipa ada kamtoa mtoto shule bila Ridhaa yangu.
Pole sana mwalimu
 
Dkt. Dorothy akusaidie nini mkuu?
Mafunzo ya kuwasaidia wanaume yanapotoka hapa huwa mnakuwa wapi?
Achana na huyo mwanamke na ufungue ukurasa mpya
Kuna watu wanakupenda na kukutegemea kiasi ukifa leo ndio watakaoumia sana
Kubali ulikosea kuwa na huyo mwanamke achana nae na endelea kutunza mtoto wako
Mwanamke akishakusaliti kingono ni sawa na mbwa mwenye kichaa suluhisho ni kifo yaani achana na huyo mwanamke
Kwani huyo mwanamke ulitongozewa au ulipewa bure, shabash
Umelogwa????
Asante
 
Sasa unataka MTOTO au MKE?.... Kama MKE hapo kwa herufi kubwa ni kuwa HUNA... Pigania tu haki zako kwa mtoto.. Yaani mwanamke keshachukuliwa bado unamlilia aiseeee! Acha uzembe!
 
Njoo sms 0765 345777 tafadhali copy tuma huu ujumbe huko. Ila kesho ndiyo nitasoma na kukupa afisa wa kukusikiliza. Shukrani
Sasa hapa ndo machozi yamenibubujika haswa, Mungu akubariki sana we Mama, majina na id zetu zinaweza kuwa za mchongo ila maombi yetu hua ni ya kweli

Moja ya Viongozi wanaonifanya nijiskie fahari kuwa Mwanachama wa Chama. Unaupiga mwingi alafu kwa kasi ya ajabu!
 
Mjeda anaweza fanyiwa kitu mbaya anytime, sometimes power is powerless .

Kama yupo tayari kujiua means anaweza kuua pia
Mjeda asichukulie poa,huyo raia alipofikia chochote anaweza kukifanya.Ogopa mtu wa hivyo.
 
Sasa unataka MTOTO au MKE?.... Kama MKE hapo kwa herufi kubwa ni kuwa HUNA... Pigania tu haki zako kwa mtoto.. Yaani mwanamke keshachukuliwa bado unamlilia aiseeee! Acha uzembe!
Mtoto
 
Wanaojua kutagi naomba mumtagi Dr Dorothy Gwajma.Ni mwanaume ninayeonewa sina pa kusemea
BUMIJA Salaam, nimesubiri ujumbe wako tangu jana unitumie kwa WhatsApp 0765 345777 au PM sijaona. Naweza kuwa sipo hewani kwani, niko nje ya nchi na naanza safari ya Namibia-Dar mchana huu hivyo, kama kweli unahitaji msaada, nitumie hiyo sms nitoe maelekezo hatua za ustawi wa jamii zianze kukufikia. Huwa, tunapenda kupokea hoja, kujali mtoa hoja, kufanyia kazi, kufuatilia na kutoa mrejesho. Ahsante sana.

Cc. Kwa yeyote hapa jukwaani tafadhali mtag BUMIJA kwa hatua zake.

mbarikiwe, nawatakia Jumapili ya baraka.

GwajimaD, Windhoek, Namibia.
 
Attachments

  • IMG-20250906-WA0013.jpg
    IMG-20250906-WA0013.jpg
    52.5 KB · Views: 28
Pole!

Lazima ujue mitego ambayo wanawake wanatutega na ukishashindwa namna ya ku by pass mitego yao maumivu yake ni makali sana!

Baadhi ya mitego ni kama hii;-

1.Tendo la ndoa,hapa ataanza kukunyima show,hiyo red alert Kuna mtu anapewa game!!

Suluhisho
-Acha kuiomba tena,onyesha waweza ishi bila show yake!utaanzisha chimbo au ishi maisha yako kabla hujampata!hasara ni matumizi kuongezeka ya pesa!!!

Utaanza kuona visirani na mind games zinaanza,ataanza vituko vingine ataacha kupika,kufua,ataanza kuchelewa kurudi nyumbani na kukutia wivu Kwa kuwakubali wengine kwamba ni wanaume rijali kuliko wewe!kelele matusi Kwa watoto n.k!

Utapiga kimya utaendelea na utaratibu,asipopika utaenda kula sehem au pika mwenyewe usiogope,fua mwenyewe !halafu Anza kufikiria kuoa upya au kuishi mwenyewe coz huyo ameshakua mshindani wako badala ya msaidizi!!

2.kusambaza chuki Kwa watoto na majirani,kukupaka mavi uonekane hufai kwenye jamii!!

Suluhisho:-timiza wajibu huku ukiendelea na maisha yako plus ukimya usijibizane nae!!

3.ataanza kutaka uhakika wa kumiliki baadhi ya asset kama mnazo ,kama mmezaa watoto !baadhi achana nae achukue mapato yake pole pole!kama watoto wakikua wamilikishe watoto hizo asset,we jipange na Anza kujitegemea kusimama mwenyewe!!

Baadae tafuta mwingine anzisha maisha!!

Halafu swala la watoto akionyesha kutaka awamiliki yeye kuliko wewe!kana kwamba anakunyima watoto!!suluhisho usigombanie viumbe wa Mungu coz yeye ndio anajua hatma ya kila kitu!Mwachie ahangaike nao Hadi atakapotosheka na kujua kwamba Wana baba yao!!

Ni uzembe na udhaifu mkubwa sana mwanamme kugombania watoto aiseh achana nayo kabisa mkuu!Damu haipotei wakikua watajua!!

USIZEEKE NA WATOTO WA TUMBO MOJA,USIZEEKE NA WATOTO WACHACHE!NI BORA UWE NA WATOTO WE GO UKAWAHUDUMIA KIDOGO KIDOGO,KULIKO WATOTO WACHACHE WA KIZUNGU UKWAHUDUMIA SANA COZ WAKIKUSALITI KWA KUFUATA MDOMO WA MAMA YAO IMEKULA KWAKO MAZIMA!!

ZAA WENGI HUDUMIA BASICS HALAFU WAPIGANIE HATMA ZAO KAMA WEWE ULUVYOPAMBANA HADI ULIPO!!

EPUKA UNIVERSITY SYNDROME INAYOWATAFUNA WAZAZI WENGI ETI KILA MTOTO LAZIMA AFIKE CHUO KIKUU KANA KWAMBA WALIOFIKA CHUO KIKUU NDIO WENYE PESA AU WAMEJIPATA KUMBE KANUNI YA PESA HAIFUATI MFUMO WA MAKARATASI YA SHULENI KAMA TUNAVYOAMINISHWA TANGU WADOGO!!

KWENYE MAISHA HAYA PESA ANAPATA MTU YEYOTE NA KUJIPATA ANAJIPATA MTU YEYOTE KUTOKA ANGLE TOFAUTI ZA MAISHA !!

USITISHWE NA MTU KUHUSU ELIMU KUBWA AU NDOGO COZ WOTE TUNAKUTANA KITAA KUTAFUTA PESA NA YEYOTE ANAWEZA KUIPATA KIVYOVYOTE!!

WEWENI KIUMBE HURU MWENYE MAHITAJI YA KIMAUMBILE DINI ZILIKUJA BAADA YA KIUMBE KUUMBWA USIFINYANGWE NA DINI KISA MAHITAJI YAKO YA KIMAUMBILE,NAJUA WAKRISTO NDOA ZINAWATESA SANA KWASABB YA IMANI YA MKE MMOJA,FUATA MAHITAJI YA KIMAUMBILE NA UPEPO WA MAISHA UNAVYOENDA!UTAKAPOISHIA HAPO HAPO!!

MUNGU AKUBARIKI!!
 
samahani mkuu,watu tunatofautiana kufikiria lakini ngoja nikuulize kwani huyo mtoto mazingira aliyopo sasa hivi ananyayasika? kama sio hivyo basi achana na kumuwazia huyo mtoto kabisa badala yake hizo hela ulizokua unatoa kumhudumia fanya maswala mengine ya msingi au kunywa hata pombe kila mwsho wa mwezi.

hebu waza miaka 30 mbele ndo unaishi, kwanza huyo mtoto atakua na mke wake kama hatokua padri.
ni kama ambavyo leo hii baba yako hawez kukuzuia kwenye maamuzi yako.

Sasa chakufanya hapo tafuta watoto wengine bila kuwalinganisha na huyo unaempigania sasa hivi,na hata usipokua na mtoto hakuna atakae kudai zaidi ya kua na uhuru sana kwenye maisha yako kwanza pesa zako zitakua zakwako mwenyewe tu usifanye biashara za kubahatisha unaweza kupigania hivuo halafu baadae mtoto akaja kukukataa kabisa au akawa hata teja,mvuta bangi, mwizi, ni maumivu makubwa sana hayo.

zingatia kama mtoto alipo sasa hivi hateseki na mahitaji ya msingi anapata we achana nae tu.
 
Umempa ushauri mzuri sana kama atataka kujiua sasa ajiue tu kwa ushauri huu uko clear mno ujue sometime unapambana na ntoto ivo mpk kutaka kujiua mwisho wa siku haji kukuthamini wala nn yy atulie afanye mishe zake nyengine ka akijisikia kujinyonga atakuwa na ishu nyengine ss
 
Nimemuelewa kaka, shida yake ni mtoto wake, kamlipia ada mwaka mzima. Mwanamke kwa ujeuri anaopewa na mwanajeshi kamuhamishia mtoto shule nyingine bweni. Halafu mtoto ana vyeti viwili, ni kwamba ana wababa wawili.

Waziri akimpa huyo mtu, atamsaidia na hili, la vyeti viwili, je ni mtoto wake au wa mwanajeshi? Hii migogoro ya ndoa, watu hawataki kukaa kwa amani kabisa. Mpaka atafute tatizo. Mtu ajiuwe roho yake itulie aah.
Duu na waelewa sana baadhi ya wanaharakati wa US wanao push swala la DNA liwe la lazima kabla ya baba hajasaini cheti cha kuzaliwa cha mtoto. Huyu jamaa anayo ya pitia anahitaji msaada mkubwa, kwanza ni kwa yy mwenyewe, pili ni kwa mtoto wake.
 
Hizi ndoa za kutoshikiana simu zimeenda mbali sasa hata chumbani kwangu hakuna kuingia :2Head::2Head:

Msiusingizie ukristo hapa, The LORD'S laws are good and support none of this foolishness people put themselves through these days.
 
Nishasikia mtu anasema kabatini kwake mke haruhusiwi kufungua. Afue nguo azikunje aweke kitandani, kabatini atakuja kuweka mwenyewe. Speaking of being a glorified house maid.

Kwahiyo kila mtu na simu yake, kila mtu na kabati lake, kila mtu na chumba chake....nafikiri kila mtu aishi kwake tu na usithubutu kwenda kwa mumeo / mkeo bila taarifa:2Head:
 
Wasalamu.

Nilioa mke wangu 2017 ila kukawa na mwanajeshi anamdanganya mke wangu.Mimi ni mwalimu kipato changu ni duni ikafikia hatua mke wangu kamtoa mtoto shule.

Natamani kujiua ila naomba waziri wa ustawi wa jamii Dorothy Gwajma nisaidie.

.Ni mwalimu Wilaya ya Babati shule Ngolei. Ni mwanaume ninayenyanyaswa. Nimelipa ada kamtoa mtoto shule bila Ridhaa yangu.
BUMIJA una shida ya kweli? Mbona waziri anakutafuta hapa na wewe hujibu? Amekupa namba ya simu ya mawasiliano zaidi
 
Back
Top Bottom