Nimekufatilia sana majibu yako inaonekana pengine unakitu unakijua zaidi tofauti na watu wengi kuhusu ulimwengu. Hauamini katikati uwepo wa Mungu (Imani). Na unaamini katika mchakato wa kawaida wa maisha, yaani ili kitokee hiki lazima ufanye hivi. Kiufupi iyo ndio sayansi inazingati ushaidi na kweli ( evidence na fact)
Kwasababu kisayansi hakuna kinachoweza kutokea tu bila sababu, mfano: ili mvua inyeshe kunamchakato lazima uafanyike. / giza na nuru kunamchakato unafanyika ndio vinatokea n.k na kunashahidi za kisayansi.
Tusaidie kwa unachojua na sisi tufaidike.
Tuambie basi ni ipi asili ya awali kabisa ya ulimwengu? ( Ulimwengu ulitoka wapi )
Jibu likikosa evidence na fact iyo sio sayansi tena ni Imani, na sitaki kuamini kama sayansi na yenyewe inatumia Imani.
Mkuu science never claims kwamba inajua kila kitu
Sayansi ipo limited
Sayansi haina MIUJIZA yoyote mkuu, ni logic tu, inakusanya taarifa inazifanyia kazi na kutoa majibu.... the process can be complicated lakini hakuna miujiza yoyote.
Tuna apply sayansi kila siku kwenye maisha yetu bila kujijua kwamba tuna apply science.
Mfano ukiwa na banda lako unafuga kuku halafu kila siku kuku mmoja anapotea bandani.... utakachofanya kujua ndio sayansi yenyewe
Ukiondoa sala unayosali kila kitu utakachofanya, utakachotumia utakua una apply science.
Dunia hii ni aridhi maji mimea na viumbe hai..... the rest unachokiona ni matokeo ya SAYANSI, bila sayansi mimi na wewe tusingekuwa tunajadiliana hapa JF
Kama nilivyosema sayansi HAIJUI sababu ya kila kitu mkuu, na hapa ndipo watu wanajichanganya kudhani sayansi inaweza kila kitu na kuanza kuishindanisha na DINI/IMANI..... hii sio SAHIHI
Kwenye sayansi kuna scientific FACT na scientific THEORIES
Nadhani unajua vizuri maana ya FACT.
Theories sio FACT, ni namna science inajaribu kutengeneza uwezekano wa jambo kutokea kulingana na taarifa zilizopo
Sayansi haijui KWAHAKIKA dunia hii imetengenezeka vipi, ndio ikaja na THEORY ya BIG BANG theory.
Theory are open tobe challenged ....... mpaka pale itakapo kuwa scientific FACT
So ukidai theory za kisayansi ni sawa na IMANI ntakuelewa lakini tofauti ni kwamba theory sio fact na zipo wazi kufanyiwa maboresho kulingana na new findings. Hii haipo kwenye IMANI
Mkuu binadamu ni kiumbe mdadisi, na moja ya jambo analolidadisi sana ni ulimwengu huu umetokeaje?
Sayansi haina MAJIBU ikatengeneza theory.
Wengine wakamtengeneza MUNGU ili apatikane aliyeiumba
HAKUNA ANAYEJUA DUNIA IMETOKEAJE...... hakuna