Minazi ni miti iliyo hatarini kupotea, dalili zinaonekana

Hakika kilimo hiki ni cha kimkakati na uwekezaji ukiwa mzuri kitatutoa kimasomaso.
Tui la nazi ni bidhaa inayouzika mno duniani, kutokana na utandawazi dunia nzima inakula curry na curry bila tui la nazi haiwi curry. Bado mapishi mengine.
 
Government intervantion is inescapable for this bro. Hata uwe na innovation kiasi gani without government intervantion you will stuck.
 
Sorry nje ya mada.
Nina mpango wa kulima migomba heka 5. Kwangu Mimi Naona zao la migomba linawahi kumtoa mtu manake mwaka mmoja mavuno tayari, ntapanda mwaka huu mwezi wa 9.

Ni wazo mwakani ntajaribu Hilo zao pia
 
Sorry nje ya mada .
Nina mpango wa kulima migomba heka 5.kwangu Mimi Naona zao la migomba linawai kumtoa mtu.manake mwaka mmoja mavuno tayali.ntapanda mwaka huu mwezi wa 9.
Ni wazo mwakani ntajalibu Hilo zao pia
Mama yangu alipanda ndizi mzuzu mashina 200 na yote anavuna Ramadan hii. Mkungu sh 5,000 shambani.
 
Kila baada ya miezi mitatu unaangua nazi unalipa ada ya watoto.
Mwaka 1986 hivi, Mheshimiwa Rais Mwinyi alitoa hadhari kuhusu kudharaulika kwa zao la nazi. Hasa uvunaji uliopindukia wa madafu, n.k. Akasema, itafika siku nazi itakuwa inauzwa moja sh. 100. Adjusting for inflation, bei ya nazi itakuwa imepanda kama alivyosema Mheshimiwa Mwinyi sr.
 
..wakati mwingine nadhani minazi ni investment nzuri kuliko uwekezaji ktk miti ya nguzo/mbao.

..tatizo linakuja kwenye matunzo ya minazi toka kupanda mpaka itakapoanza kutoa matunda.
Kuna miaka kumi ya ku sacrifice lakini baada ya hapo kama una heka moja una uhakika wa milioni 2 kila baada ya miezi mitatu.
 

..SMZ Pemba wanajitahidi kuboresha zao la minazi. Nimesoma mahali kwamba Serikali ina vitalu vya kuzalisha minazi ambayo hugawiwa kwa wananchi maeneo mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…