Kwa jinsi tulivyoanza na kauli mbiu ya Kilimo ndiyo Uti wa Mgongo wa Taifa letu. Ulitegemea mazao yenye tija yangepewa kipaumbele na wataalamu wa masoko kututafutia masoko nje. Kwakweli sikuhizi Nazi huuzwa tui kwenye makopo au maji ya madafu kwenye makopo...SMZ Pemba wanajitahidi kuboresha zao la minazi. nimesoma mahali kwamba serikali ina vitalu vya kuzalisha minazi ambayo hugawiwa kwa wananchi maeneo mbalimbali.
Kuna miaka kumi ya ku sacrifice lakini baada ya hapo kama una heka moja una uhakika wa milioni 2 kila baada ya miezi mitatu.
Unaweza kuweka robo heka ya kale na 3/4 mbegu mpya. Nina uhakika huko Indonesia ambako uzalishaji wa nazi ni mkubwa wanatumia mbegu za kisasa...kweli.
..lakini " hed ek " inakuja kwenye kuchagua kati ya mbegu za asili au kisasa.
..kwasababu kisasa wanasema inazaa baada ya miaka 4 na asili inazaa baada ya miaka 7.
..vilevile wanasema kisasa inazaa nazi nyingi kuliko minazi ya asili, ila haihimili magonjwa.
Kwa jinsi tulivyoanza na kauli mbiu ya Kilimo ndiyo Uti wa Mgongo wa Taifa letu. Ulitegemea mazao yenye tija yangepewa kipaumbele na wataalamu wa masoko kututafutia masoko nje. Kwakweli sikuhizi Nazi huuzwa tui kwenye makopo au maji ya madafu kwenye makopo.
Kaka yangu amenunua heka sita za shamba lina minazi. Aliyeuza ameuza kwasababu ya matatizo. Kaka ameamua kuongeza minazi shamba zima...serikali ilijitahidi kufanya research ya mbegu bora za minazi ila ilifeli vibaya, naona wameamua kurudi kwenye minazi ya asili.
..lakini hata ukitafuta taarifa za zao la minazi kwa kweli unaona kabisa kwamba hii sekta haijachangamka.
..labda huko ndio kwa kuwekeza ambako watu bado wamelala, ila kama ulivyosema inahitaji uwe mvumilivu.
..i think that is the best way to go about it.Unaweza kuweka robo heka ya kale na 3/4 mbegu mpya. Nina uhakika huko Indonesia ambako uzalishaji wa nazi ni mkubwa wanatumia mbegu za kisasa.
Zamani kati ya Dar na Bagamoyo palikuwa na shamba kubwa la minazi pembeni ya barabara. Sijui bado liko?..i think that is the best way to go about it.
..unaweza kuingia kichwa-kichwa mbegu ya kisasa halafu mingi ikafa.
MIRADI PWANI: Minazi mipya inayokomaa baada ya miaka mitatu pekee
Na LUDOVICK MBOGHOLI MAAFISA wa kilimo katika kaunti ndogo ya Taveta wamezindua ugavi wa miche 10,000 ya minazi kwa wakulima wa kata ndogo, wadi ya Mboghoni. Kwenye uzinduzi huo, mamia ya wakulimataifaleo.nation.co.ke
cc Lily Tony, Malila, PatriceLumumba
Hili mbona liko wazi kwenye post yangu ya awali nimeongea mambo ambayo Serikali inapaswa kuweka mkono wake ili kuwakwamua wakulima hasa hawa wadogo. Nadhani uliona nini kilifanyika kule Mtwara baada ya wanunuzi wa korosho kushindwana bei na wakulima.Mkuu hebu taja Government inaweza fanya nini mwananchi au kampuni ya binafsi haiwezi kifanya tena kwa ufanisi?
Tatizo weziMinazi ni zao la biashara, ni kuwa vijana hawafahamu au hawana subira lakini ukiwa na heka tano za minazi wewe utaangua nazi mpaka mwisho wa maisha yako.
@Sky Eclat mashamba ya minazi bei gani yanapatikana wapi wizi vp na je mnazi mmoja unatoa nazi ngapiKila baada ya miezi mitatu unaangua nazi unalipa ada ya watoto.
Kuna mikoa nazi inauzwa mpaka buku jelo.
Minazi ni fursa kumbe,sijui kwanini inasahaulika hivi.
Hii ya Voda fasta hata mimi siiamini. Sisi tulikuzwa na minazi. Mzazi anakwenda kukopa amana anasema nitarejesha nikishaangua nazi zangu.Maximum bei niliyowahi kununua nazi ni 1500/= ila kipindi cha kawaida ni 1000/= ,nazi nzuri zinazotoka mafia....Za Bagamoyo nyingi za kufukia chini ukiiona kwa nje imekauka kau ila ukivunja ni koroma.
Hii ya Voda fasta hata mimi siiamini. Sisi tulikuzwa na minazi. Mzazi anakwenda kukopa amana anasema nitarehesha nikishaangua nazi zangu.
Bibi alikua na kiunga alichoachiwa na babu, licha ya kuangua nazi kulikua na mgema pombe. Mshahara wa Mgema ulikua pombe ya wiki mbili kwa mwezi. Siku Mgema akileta pesa ya pombe alikuja na pombe pia.
Bibi alikua Don kijijini hakua anakaukiwa na pesa.