Minazi ni miti iliyo hatarini kupotea, dalili zinaonekana

Pia nimekuwa interested ila nakosa taarifa za kutosha.
 
..kuna uzi mmoja niliweka contacts za kituo cha utafiti cha serikali cha zao la minazi.

..ofisi zao ziko Mikocheni Dsm na wana vitalu vya miche viko Bagamoyo na Mkuranga.
Nilikuwa nasearch hapa kuhusu mada ya 🥥 nadhani nilishausoma ule wenye hizo taarifa nitarudi kule nione, umaskini ni kikwazo sana kwangu mkuu nataka kufanya kitu kitakachohakikishia kizazi changu kipato cha kuwasaidia, sitaki wapitie yale ninayoyapitia hivi sasa.
 
Sorry nje ya mada .
Nina mpango wa kulima migomba heka 5.kwangu Mimi Naona zao la migomba linawai kumtoa mtu.manake mwaka mmoja mavuno tayali.ntapanda mwaka huu mwezi wa 9.
Ni wazo mwakani ntajalibu Hilo zao pia
Boss tupe mrejesho
 
Habari boss mrejesho wa minazi maana nataka kuingia miguu yote
Bado mzee, ile 25 niliyopanda ni ya kienyeji, kuzaa ni ndani ya miaka 7.
Kuna mingine hii ya muda inazaa, takribani minazi 70+,shida tu ni wezi, ingekuwa si wezi, basi nazi 2000 kila baada ya miezi mi3 ni suala la kawaida ila wezi wananikomesha mzee.
 
Big up sana
 
Hayo madude si ndio mwarabu aliyaleta hayo?
 
Andiko bora kabisa hili na limenihamasisha kufufua shamba langu la minazi huko Pwani.
 
Government intervantion is inescapable for this bro. Hata uwe na innovation kiasi gani without government intervantion you will stuck.
Upo sahihi. Cha muhimu ni kuweka mikakati na kuihusisha Serikali ili mafanikio yapatikane.
 
Miaka saba siyo mingi mkuu cha msingi hatujachelewa. Tukapande minazi tuondokane na umasikini.
 
Sky Eclat , makaveli10 ,

..kati ya minazi, miembe, michungwa, ipi inaingiza kipato kikubwa zaidi?
Nitakuwa mnafiki mie nina minazi tu. michungwa, kijana wa shamba alileta uhuni, akaifyeka na kutengeneza mkaa.

Sijui hiyo miembe ni ya kisasa ama lah..
Ninachojua nazi unavuna kila baada ya miezi mi3 hivi, yaani unapovuna hutoi zoote, unatoa makole yale yenye nazi kavu, unaacha nyingine, baada ya miezi mi3 unashusha tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…