Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #41
Joka Kuu,..wakati mwingine huwa nakuonea huruma sana.
..unajua vijana wa siku hizi, unaohangaishana nao, hawana mazoea ya kusoma vitabu vingi.
..mtu mwenye mazoea ya kusoma vitabu hatokuwa na shida, au hatotaharuki, akikutana na maandiko yako.
Joka Kuu,
Usinionee huruma mimi hii kazi ya kufundisha naipenda sana ndiyo
maana unaniona sibanduki hapa.
Wala sihangaishani na mtu yoyote tuko kufunzana nikitegemea kuwa
wako watakaojua starehe iliyomo ndani ya vitabu.
[emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]Kadoda,
Ilikuwa katika vipaumbele vyao na wakaandika historia yao kupitia Chuo Cha Kivukoni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Joka Kuu,..hapo niliposema "kuhangaishana" usinielewe vibaya.
..unajua sisi watu wa bara Kiswahili chetu hakijanyooka.
..nilichotaka kusema/kusisitiza ni kwamba USICHOKE kutoa elimu.
Si unukuu kaandikaje. Bila citation historia ya "baba wa Taifa" ni kama hayo unayaleta wewe tu na kusingizia kaandika mlinzi wake.Unataka ushahidi upi zaidi ya alichoandika mlinzi wake au unafikiri historia hadi aandike Mzee Mohammed
Alafu Mzee Mohammed anaandika historia za wazee wa DSM waliopigania Uhuru sio historia ya kilichotokea 1964 ambacho ni watu wa karibu tu ndio wanafahamu
Punguza chuki na kufurahi Baba wa Taifa aandikwe kwa Mabaya
Kitalii,Achen utan bana. Tangu lin wapigania uhuru wakavaa msuli unacheza na kupigania uhuru Sio. Hawa walikuwa wanywa kahawa wa kijiwen.
Kitalii,
Nakuwekea hapo chini picha za waliopigania uhuru wa Tanganyika wakiwa
katika misuli na kanzu zao kwa wanaume na kwa akina mama wakiwa na
mabaibui yao:
Tanganyika baada ya ujeruman haikutawaliwa tena we Mzee Watu walikaa kwenye vikao vya kahawa wakahc wanaweza kujitawala Ndio wakaona wenyewe hawawez wakampa hiyo shughuli ya maneno Nyerere. Na hapa Ndipo mnapopotea na mentality hii hamko huru hadi Leo. Sasa Kama nyie mlipigania uhuru Kenyatta hapo Kenya asemeje
Kitalii,
Nitafurahi kupokea kutoka kwako picha za wavaa tai, na suti wakipigania uhuru
wa Tanganyika.
Al Abry,Kuna tatizo kubwa la kisera kuhusiana na issues za historia ya taifa letu.hakuna commitment kama taifa kulinda na kuhifadhi historia adhim ya nchi yetu katika harakat zote za uhuru.nahis na mzee mwenyewe hakupenda kuwaweka katika historia wenzie waliomuongoza katika harakati zile.
Alikua na uwezo huo ila nahis hakupenda au pengine alivyofanikisha alichotaka akawasahau wenzie na akaliaminisha taifa kua harakati zile ni kwa juhudi zake binafsi.
Nakushukuru sana mzee mohammed said.umeniongezea kitu kikubwa katka mafhum yangu.jazakka llah khyr
Sent using Jamii Forums mobile app
unataka kutuambia kwamba uhuru wa Tanganyika ulipiganiww na "wazee wenu " tu,..we nawe.Mzee Mshume Kiyate ni shujaa wa kweli wa Uhuru.
Sijapatapo kumsoma popote nje ya historia tunayoletewa na Alama Mohamed Said.
Hizi ndiyo Lulu za kuhifadhiwa vizazi vijavyo wazikute.
Halafu anakuja punguani anaejiita Yericko Nyerere au mwengine anaejiita Mag3 au mwengine anaejiita Nguruvi3 wanajidai wanaijuwa historia ya Uhuru wa Tanganyika.
Nna uhakika hawajapato kuijuwa historia ya ukweli inayoambatana na ushahidi wa mapicha nje ya maandiko ya Mohamed Said.
Hawa ndiyo wazee wetu wa Dar. Waje watuelezee na wazee wao wana historia ipi ya Uhuru wa Tanganyika.
Luggy,unataka kutuambia kwamba uhuru wa Tanganyika ulipiganiww na "wazee wenu " tu,..we nawe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Shukran sana mzee wangu.Al Abry,
Ahsante sana.
Mimi niajua vyema historia hii kwa kuwa baadhi ya wazee wangu ndiyo waasisi wa African Association 1929 kisha Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 na TANU 1954 na walishiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Unaweza kusoma historia zao katika blog yangu www.mohammedsaid.com.
Sent using Jamii Forums mobile app
Luggy,unataka kutuambia kwamba uhuru wa Tanganyika ulipiganiww na "wazee wenu " tu,..we nawe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Jee Mapinduzi ya Unguja waliohusika wakuu kwenye ile siku walikuwa kina nani? Jibu- watu wa kawaida tu [wakulima,wakwezi,wavuvi,wafanyabiashara wadogo nk] Wakubwa wengi walijitokeza baada ya mafanikio.Achen utan bana. Tangu lin wapigania uhuru wakavaa msuli unacheza na kupigania uhuru Sio. Hawa walikuwa wanywa kahawa wa kijiwen.
Mganda ndio aliyeratibu na kufanya yale Mapinduz wewe hawa wavaa vikoi wanaweza nini zaid ya kula orojorojo tu. Mshukurun OkeloJee Mapinduzi ya Unguja waliohusika wakuu kwenye ile siku walikuwa kina nani? Jibu- watu wa kawaida tu [wakulima,wakwezi,wavuvi,wafanyabiashara wadogo nk] Wakubwa wengi walijitokeza baada ya mafanikio.
Hii nchi haijawah kuwa na wapigania uhuru zaid ya akina mkwawa Mzee. Hawa ni Watu tu walikuwa wanataman kujitawala wakiwa kijiwen wakashindwa namna nzur ya kuiwasilisha hoja yao wakawashirikisha mawazo yao akina Nyerere na Nyerere kwa usomi wake akaenda UN kuwasilisha hilo wazo akakubaliwa ukafanyika uchaguz Tanganyika ikapewa utawala wao. Lakin Hakuna aliyepigania hii nchi walipewa waingereza kuiongoza mpaka hapo wenyeji watakapoweza kujitawala so hii kutuletea story cjui nimeenda vyuo gan cjui nan alitoa nini Mbona za kawaida Sana hujaona hata Nyerere baada ya kushika madaraka hakuwapa madaraka hao wavaa vikoi maana hawakuwa na wazo jipya zaid ya yale ya kwenye kahawa. Unawapaje utawalaKitali,
Napenda mjadala lakini sipendi shari.
Naona umeghadhibika lugha inakuwa ya kifedhuli.
Maneno, ''we mzee,'' hayafai kwani si uungwana.
Ukishajua kuwa mtu unaezungumzanae ni mzee heshima
ndipo mahali pake.
Sasa tuendelee na mjadala.
Ikiwa wewe unaona hapakuwa na kupigania uhuru hiyo
Tanganyika huu ni fikra yako na una haki nayo kwani
ikhtilafi ndiyo sifa ya mjadala.
Mimi nimeandika kitabu kizima cha uhuru wa Tanganyika
na ni kitabu maarufu kwingi katika vyuo vinavyosomesha
historia ya Afrika.
Si hivyo tu nimeshirikishwa na vyuo maarufu duniani katika
miradi ya kuandika historia hii ya Tanganyika na kazi zangu
zimechapwa kitabu.
Unaweza ukabaki na fikra yako hiyo kuwa hapakuwa na
kupigania uhuru Tanganyika.
Hakuna neno.