Miongo miwili wamekataa kubadilisha jina la mtaa wa Tandamti kuwa Mshume Kiyate

Miongo miwili wamekataa kubadilisha jina la mtaa wa Tandamti kuwa Mshume Kiyate

Hao wazee hawajulikani popote ktk historia rasmi ya Tanzania pengine ndio maana hawa viongozi vijana wa sasa hawana khabari nao. Hawa wazee imekuwa ni kama mfano wa kobe hata acheze kiasi gani kuna gamba ambalo linazuia asionekane. Hilo gamba ndio linawaogopesha waliojuu kuiandika historia ya nchi hii. Hawataki wajulikane wanyonyaji walikuwa nani na wapambanaji walikuwa nani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kajirutaluka,
Historia rasmi kwa sasa haina maana tena baada ya kuwapo kitabu
cha Abdul Sykes (1998).

Ikiwa hujakisoma kitabu hiki kisome kuna mengi:

ciTsGU3Sn-CSOlCgpXUtMPnGQMMebtW0GIlcIw8E2ZgEUhPmSweBBKRcKzjuov9KEA9eBtTMO91uI_y8uubg9xDXaiqHOoKTaQEWpX9cssMMMaH3dZ8HqTu9BCxmNbCmk2uXT2JizldxPNE1k3BnhPK2DX30oPz7h47w5rN1phxWGYWCKaudtLXRJNznP66JTJWxDQjHmzd78_frKZZPCVKgOSiA2RCiOZ-RpLK9fsyssvc-nq_XFSBQuQI_6V8FTic6xeKOaTBCuB712KafvU6wha_bOBf9P48vHLXk1-A_SLtSJlxB4o5Z8hHMObBQTtJQP9hr1V7OS6lElOuclYQkExKogi05jZIdEVYElIjTFI5vjRY3wj1KqwRa361MxTn5qETXxQFuKh54GR-_-ynkJ7Zi_y0RENeWXeH2TEl4e2DzHHyEwrJJ4wcjjUpNDc9W6OP5VoduAfsGz0K034n_pwBzIhjOiVf5MmEdVlll-31ofXdmWlDmwoPue5BaaXtopTxgMUX5YnnE9L6YX7h5A3T_83-bFb01amxcVLpKhM0i544aFm6JF_U_iwtjxuO6WXG4Sx9bwugW7JtQ-l9iYkKx6oUJPWEm4ishFg=w852-h629-no
 
Ndio alikua anatoa mfano kwamba hakukua na kupigania uhuru kutoka kwa Muingereza.
Kwake yeye mapambano ya wakati wa Mjerumani ndio yalifaa kuitwa "kupigania uhuru".

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila Mbongo,
Tukubaliane kuwa mapambano dhidi ya Wajerumani 1905 - 1907 ndiyo
harakati za kupigania uhuru.

Je, Kitali anaijua historia ya Sultani Abdulrauf Songea Mbano
aliyepigana na Wajerumani katika Vita Vya Maji Maji?

Hili swali nimemuuliza lakini hjaweza kutoa jibu.
Anaweza akaingia hapa kumjua shujaa huyu:

CYgjIZKWYAA1G2j.jpg


Mohamed Said: CHIEF ABDUL RAUF BIN SONGEA MMOJA WA MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI NDIYO HUYU SONGEA MBANO?
 
Kitali,
Tafadhali toa hoja bila kutukana na kejeli.

Hatari ya matusi ni kuwa tutawakaribisha katika mjadala huu mabingwa
wa kutukana na mjadala utavurugika.

Mzee Said Chamwenyewe na mfano kama wake wakivaa kanzu na
kikoi na ndiyo waliojenga TANU na kuingiza wanachama wa mwanzo
kutoka Rufiji 1954 baada ya Msajili wa Vyama kukataa kuisajili kwa
kukosa wanachama.

Hiyo historia ya Uganda si sawa.

Soma kitabu cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika,'' utajifunza
mengi.

WG4h7tQPP0hM5JvmrwXId3a6nnsr9HUvh0Zyjt6U0a34Le1Yrz2qh7sh_owwg7h5t3o1vKXFU7LJa65Okri7FZZgZxL9Ic2OplHYor5knOS6ZlmRR-l3tmElLiONVBnEOtote0Zidjd_YaOqZSTIaiy75aqmL8u_cLzyKxPek0OIUElK2yBlWVDlsHiCCzLjmLmDwIoibRARplAMUKHGD1bSLaXg4RAuemjXDePsktqezTQp7X7KEbl8NvwQmzzyAx7HfUIqMF-iZ7VCI9VaSlxJ3evjXf7ucUVT7nWcLpQr4hXy4mpZwvXsvOSl5ew_7gLRCA1eF8MkHzbdr4nXdNKzsRXamSH1iIiB3K1VgBv2gPpNRY5VVUx0vxcw_SwDDP7W_8NPEygwQNRHYQts-4BjMGQwLnARRdmwXEer-cL_XBSt-Wh0Seh3nt0xBYIUDQ6Ap20nV8e2Xqi73q1ILUUE2lW_mHHHYuvJkITHWwvoKYygcjZYmWkglEsEE1woXMXu0nJ-H-ZyhDAh4Svo_xf8oz2b6s3dRxt7JZYo4WXhAJMagML3-UznzYnGn_8cwwcmDbRmgJI6SKdiECL-T0roIRGc_jfV4XF5cXbvI74=w423-h629-no


Uongozi wa TAA kuanzia 1950 ulikuwa na vijana hawa wazeee
unaowazungumza wewe walikuwa wawili tu - Mufti Sheikh Hassan
bin Amir
na Sheikh Said Chaurembo.

Waliobakia Abdul Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu,
Stephen Mhando, Dossa Aziz,
hawa walikuwa vijana.

Hawa ndiyo walikuwa wajumbe wa TAA Political Subcommittee kamati
iliyokuja kuunda TANU 1954.

Katika hawa hakuna yeyote aliyekuwa na mawasiliano na Nyerere akiwa
Uganda.

LIWALI%2BAHMED%2BSALEH.jpg


Kulia ni Sheikh Said Chaurembo
Mzee elewa nimesema hawa Watu hawakuwa na kitu cha kambana nacho walipokuwa wanataka kujitawala so kutumwa tu kuwashawish Watu waungane na nyie kutaka kujitawala hiyo Sio kupigania uhuru hiyo Ni kutafuta madaraka Kama vyama vyingine tu Ndio maana nikakwambia Huwez kuvaa vikoi halafu unaniambia unapigania uhuru. Nenda Kenya hapo wakuambie mai mai walivyopigania uhuru ndio utaelewa nisemacho.
 
Kila Mbongo,
Tukubaliane kuwa mapambano dhidi ya Wajerumani 1905 - 1907 ndiyo
harakati za kupigania uhuru.

Je, Kitali anaijua historia ya Sultani Abdulrauf Songea Mbano
aliyepigana na Wajerumani katika Vita Vya Maji Maji?

Hili swali nimemuuliza lakini hjaweza kutoa jibu.
Anaweza akaingia hapa kumjua shujaa huyu:

CYgjIZKWYAA1G2j.jpg


Mohamed Said: CHIEF ABDUL RAUF BIN SONGEA MMOJA WA MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI NDIYO HUYU SONGEA MBANO?
Mbona walikuwa wengi we umemkariri Huyo tu watemi karibu wote na mangi Sina kule Kibosho walipigania uhuru
 
Mzee elewa nimesema hawa Watu hawakuwa na kitu cha kambana nacho walipokuwa wanataka kujitawala so kutumwa tu kuwashawish Watu waungane na nyie kutaka kujitawala hiyo Sio kupigania uhuru hiyo Ni kutafuta madaraka Kama vyama vyingine tu Ndio maana nikakwambia Huwez kuvaa vikoi halafu unaniambia unapigania uhuru. Nenda Kenya hapo wakuambie mai mai walivyopigania uhuru ndio utaelewa nisemacho.
Kitali,
Huna uwezo wa wewe kunifunza mimi historia ya Kenya au yoyote iwayo ile.

Ninachokisoma kwako ni kibri na jeuri tu.
Huna ulijualo.

Mwenye elimu hatukani wala hana fedhuli.
Utakuwa unaelimika na kalamu yake.

Mwaka wa 2014 French Research Institute Kenya walifanya kongamano la mashujaa waliopigania uhuru Afrika Mashariki lakini historia imewasahau.

Nilitoa mada katika kongamano hilo lililofanyika Nairobi.

Ukitaka naweza kukuwekea hapa hiyo mada yangu na iliwauma wengi mfano wa wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jina la Mshume Kiyate kwa sasa si geni tena katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mzee Mshume alikuwa katika Baraza la Wazee wa TANU kuanzia lilipoundwa 1955.

Mshume Kiyate alikuwa kiishi Mtaa wa Tandamti na akifanya biashara Soko la Kariakoo toka miaka ya 1950. Yeye ndiye aliyekuwa dalali wa samaki wote walioletwa pale sokoni. Kazi hii ilimtajirisha kwa kiwango cha nyakati zile na yeye alitumia fedha zake nyingi katika harakati za kuijenga TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kubwa ambalo lilimpambanua Mzee Mshume katika historia ya uhuru ni kule yeye kujitolea kubeba jukumu la chakula cha nyumba ya Baba wa Taifa kuanzia miaka ya mwanzo ya TANU hadi uhuru unapatikana mwaka wa 1961 na kuendelea kufanya hivyo hata pale Baba wa Taifa alipomwambia, ‘’Mzee Mshume sasa basi hivi vikapu vyako vya chakula, mimi sasa nalishwa na serikali.’’

Jibu la Mzee Mshume lilikuwa, ‘’Hapana Mheshimiwa sitoacha kuleta chakula nyumbani kwako kwani nataka wewe na watoto wako mle chakula hiki na hicho cha serikali wape wageni wako.’’

Huyu ndiye mzalendo mpigania uhuru wa Tanganyika na rafiki kipenzi cha Baba wa Taifa, Mzee Mshume Kiyate.

Miaka takriban 20 iliyopita aliyekuwa Meya wa Jiji ;a Dar es Salaam marehemu Kitwana Selamani Kondo katika kutambua mchango wa Mzee Mshume Kiyate alibadili jina la Mtaa wa Tandamti kuwa, ‘’Mtaa wa Mshume Kiyate.’’

Hadi hivi ninavyoandika na nimepita mtaa huu leo nimekuta kibao kipya kimewekwa lakini jina ni lile lile la zamani.

Hii nini maana yake?

Dharau, khiyana au nini?

kZ5LlMCgqPD9R9E5MUJWPN7_q0YkFwuZ732t0R3I0t0syOWSj010wSWEJ86ITul2cP47F7129sUqM_HUpVtOZjmFQio9OsxRtKebLa_HpMKZKvafFEQbCGKmZVMIAIy__ySItYdDqt7qArsJxhbL94SDaa8gHX6hoZpGwr_BZWnKCfRt5w9jmYUazcP2VmGSkm0cQcl_24UlzGW6nurImglkiFErzw2lThH2yfJqBaR1NQbLykO7Jj5X7oQ9f5mUtNQGRalLpkbPXz2fltNHdud0_qd4z41aJRz71KAJw7QNF3TBcArqWCduGyG9rZ_pmKzuTNdJwH1-8RGPhoFE2op62QgcQ4VMElKTyYSS0J_WUnDuQfHnDiy0z_NmziEGDLv400xMrWNXpeShnklbBKYS-WBI0O1mCax5BpkS7yZXOH74IUl8Iv6c1uVoDei5gxhl9uBNMnDjfNJyvnBPe9n6SLIKGbKkogeWR_0J3s0Zckv0FkQBAqwDp_5lnIg_M-bUlyjn1wfjCdxL7sX4aTo9__UZNTAt8dtxiEQwDl6wcJBmROaxXXAqfD1mFmUhz2s4644v8HFr6Ac_kVCyU9uUqngP49U=w360-h480-no


Picha hiyo hapo juu ilipigwa mwaka wa 1964 baada ya maasi ya wanajeshi na Baba wa Taifa kurejeshwa madarakani na Jeshi la Waingereza. TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Jangwani na Mzee Mshume Kiyate siku ile alimvisha Baba wa Taifa kitambi kama ishara ya kuonyesha kuwa Wazee wa Dar es Salaam wale waliompokea na kuwa na yeye bega kwa bega kupigania uhuru wa Tanganyika bado wako nyuma yake na wanamuunga mkono.

Huyu ndiye Mzee Mshume Kiyate.

WAZEE+WA+TANU.jpg

Waliosimama wa pili kulia ni Mzee Mshume Kiyate





tAZ7Q0CbeIpy9U9VrFhQRXVT3KiZoLVWyGRWVQGRN9MQ2MWqQTn6Pdw3hADo7z3DvALdD5Hr-xQ=w724-h567-no

Mshume Kiyate wa kwanza kulia aliyemshika mkono Baba wa Taifa na
pembeni kwa Baba wa Taifa ni Mzee Max Mbwana akifuatiwa na Mzee

Mwinjuma Mwinyikambi

Kuna picha mashuhuri ya Mzee Mshume na Baba wa Taifa iliyopigwa Novemba 1962 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Picha hiyo inamuonesha Mzee Mshume akiwa amevaa koti, kanzu na kofia amemshika Nyerere mkono akimsindikiza kupiga kura.

Karika utawala wa Baba wa Taifa, magazeti ya ''Uhuru'' na ''Daily News,'' yamekuwa yakiitumia picha hii kila baada ya miaka mitano katika uchaguzi wa rais kama njia ya kuwahamasisha watu kupiga kura na kumchagua Baba wa Taifa.
utakufa kihoro mfia dini inabidi utengwe km huyo dalali mwenzio mshume kiyate
 
Mzee Mshume Kiyate ni shujaa wa kweli wa Uhuru.

Sijapatapo kumsoma popote nje ya historia tunayoletewa na Alama Mohamed Said.

Hizi ndiyo Lulu za kuhifadhiwa vizazi vijavyo wazikute.

Halafu anakuja punguani anaejiita Yericko Nyerere au mwengine anaejiita Mag3 au mwengine anaejiita Nguruvi3 wanajidai wanaijuwa historia ya Uhuru wa Tanganyika.

Nna uhakika hawajapato kuijuwa historia ya ukweli inayoambatana na ushahidi wa mapicha nje ya maandiko ya Mohamed Said.

Hawa ndiyo wazee wetu wa Dar. Waje watuelezee na wazee wao wana historia ipi ya Uhuru wa Tanganyika.
huyo aliyekufa kihoro kwa kutengwa historia yake peleka msikitini
 
km porojo za mudi toka kwakina daisy sykes
Ndugu zangu,
Yericko tunafanya mjadala nami sioni tabu kumjibu kwani hajanitukana
kwa kiasi cha mie kumsusa na pale anapotoka nje ya mstari yeye huwa
mwepesi wa kunitaka radhi.

Lakini huyu mtu yeye kawaida yake ni kuja nyuma ya Yericko na kunitusi.
Akutukanae katika pombe nawe mrudishie hapo hapo kwenye ulevi:

Huyo hapo chini ni Emily Calachi (University of Winsconsin) msomi katika
historia ya Afrika hapo tuko New York, Brooklyn Heights, 2011.



Sikwenda kwake kumuomba fedha.
Kilichotukutanisha ni ujuzi wetu katika African History.

Nimepata taarifa siku chache zilizopita kuwa Emily ana kitabu
kitatoka hivi karibuni.

[IMG]

Huyu ni Benjamin Kirby (University of Leeds) leo asubuhi nimepokea
Ph D Thesis yake na kanitaja kama mmoja wa watu waliomsaidia katika
kukamilisha ''thesis,'' yake.

Picha hii tumepiga nyumbani kwangu 2015 na sikumwita kuja kumuomba
fedha kwa ajili ya ''njaa kali,'' yangu.

[IMG]

Nathaniel Mathews (Northwestern University), hapo ni Chicago sikwenda
kwake kumuomba fedha ila yeye aliposikia niko mjini alikuja hotelini kwangu
Hilton, Evanston kuniamkia.

Huyu bwana kama ana hoja na azilete lakini huku kuwa yeye ananivunjia utu
na heshima yangu si uungwana.

Nina picha nyingi na ''Wazungu,'' hizo hapo juu nadhani zinamtosha.
Muhimu kwake ni kuwa sijakutananao kama omba omba.

Alhamdulilah Allah kanisitiri kwa hilo riziki yangu hijapatapo kutoka kwenye
mkono wa binadamu.

Sent using [URL=http://r.tapatalk.com/byo?rid=77694]Jamii Forums mobile app[/URL]

 
Abunuwasi,
Makamba anaweza kupewa mtaa Lushoto lakini si Gerezani wakaachwa wazalendo wazawa wa sehemu hiyo waliofanya makubwa katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hili jambo mie limenistaajabisha sana na khasa ukirejea nyuma ukaangalia historia yake kwa yale yaliyotokea Msikiti wa Mwembechai mwaka 1998.

Sent using Jamii Forums mobile app
hapa bdo umetema pumba za karne,kuzaliwa tu haitoshi kupewa mtaa! kwa poroho zako si hata wewe ungekuwa na mtaa!
nkrumah,selasi,azikiwe wamepewa mitaa na sio wazawa!
km inakuuma kaipe miskiti yen majina yao!
 
Hakuna kitu Kama hicho Nyerere tayar akiwa Uganda walishaunda chama Ndio hawa wazee wakawambia tayar kipo chama njoon mje kukiendeleza so usiishi kwa kusikiliza story za upande mmoja tu utapotea njia. Narudia kuwaambia uhuru huwez kuudai kwa kuvaa kikoi wewe
.
Kwa faida ya JF Nyerere aliunda chama gani kisha akawambia kina nani waje kukiendeleza?

Ofisi zake zilikuwa wapi Dar es Salaam?

Tunasubiri majibu.
 
MEDALI YA ABDULWAHID SYKES: MWENGE WA UHURU 1961 - 2011
Mohamed Said April 29, 2017 0
Utangulizi
''Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa. Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh abdallah Chaurembo. Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima. Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu. Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana. Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka. Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandizi, maili chache nje ya Dar es Salaam. Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani.''
(Kutoka, ''Maisha ya Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...'')

Jina la Abdulwahid Sykes (1924-1968) katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa sasa halihitaji kuelezwa sana.
Historia yake imekuwa ni historia ya kusisimua unapomsoma kuhusu yale aliyofanya katika kuunda chama cha TANU 1954 akianza na kubadilisha mwelekeo wa TAA alipoingia katika uongozi wake 1950.
Historia ya Abdul Sykes pia ina masikitiko pale baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 juhudi za makusudi zilipofanywa kulifuta jina lake katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kwa hili si tu kuwa lilifutika jina lake peke yake bali na jina la mdogo wake Ally na la baba yao Kleist Sykes aliyekuwa muasisi wa African Association mwaka wa 1929.



Kulia: Ilyas Abdulwahid Sykes, Daisy Abdulwahid Sykes, Mwandishi akiwa ameshikilia Medali ya Mwenge wa Uhuru
Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes

Ilichukua miaka 50 kwa Abdulwahid na mdogo wake Ally kutunukiwa medali ya ‘’Mwenge wa Uhuru,’’ kama utambuzi wa mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika wakiwa bega kwa bega na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliyemfahamu mwaka wa 1952.
Leo nimebahatika kuiona medali ya ''Mwenge wa Uhuru'' aliyotunukiwa Abdulwahid Sykes (post homous) na Rais Kikwete katika Viwanja vya Ikulu 9 Desemba, 2011 katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Kuishika medali hii kwa mikono yangu kwangu kilikuwa kitu kilichokuwa na nafasi ya pekee katika moyo wangu.


Medali ya mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa Abdulwahid Sykes katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa
Tanganyika 2011
(Picha kwa hisani ya mjukuu wa Abdul Sykes Aisha Kleist Sykes)

Mwandishi akiwa Azam TV akifanya kipindi cha Saba Saba 2015


historia
kufanya kipindi haimaanishi ndo ukweli hata mama tapeli wa tanga aliyelia mbele ya magu alikuwa anafanya vipindi ilhali tapeli!
 
Mbona walikuwa wengi we umemkariri Huyo tu watemi karibu wote na mangi Sina kule Kibosho walipigania uhuru
Tupe ushahidi watu wajifunze hapa JF tufahamishe hizo harakati za kupigania uhuru za Mangi Sina kule Kibosho zilianzia wapi na kuishia wapi?

Tunasuburi jibu vizuri zaidi utuwekee na picha za hao mashujaa wetu wa Kibosho.

Ahsanta.
 
Back
Top Bottom