Miradi mikubwa haikuanza kipindi cha Hayati Magufuli pekee


Kikwete alikamilisha miradi mingapi ndani miaka 10, embu itaje hata substandard chinese made udom yenyewe bado haijakamilika kwa 100% ingawaje miaka sijui 20 sasa, …
 
Kikwete alikamilisha miradi mingapi ndani miaka 10, embu itaje ukiondoa substandard chinese made udom?
substandard unamaanisha nini. We hakuna unalojua kuhusu ujenzi. Kikwete miradi yake ni mingi ukianzia na huo wa UDOM kujenga chuo kikuu kikubwa kuliko vyote africa mashariki na kati. Mabarabara; Kuunganisha makao makuu ya mikoa karibu yote kwa lami, aliunganisha Dodoma na Iringa, Songea na Mtwara kupitia Tunduru, Nanyumbu na Masasi. Aliunganisha mikoa ya Arusha, Manyara, Singida na Dodoma. Aliunganisha Mbeya na Sumbawanga. Aliunganisha Sumbawanga na Katavi. Aliunganisha Shinyanga na Tabora kupitia Nzega. Aliunganisha Singida na Tabora kupitia Itigi na Uyui. Aliunganisha Mwanza, Geita na Kagera. Alijenga barabara ya lami kutokea Tinde(Shinyanga) kuipitia Kahama mpaka Karagwe mpakani mwa Nchi yetu na Rwanda.

Alijenga upya barabara kutoka Arusha-Makuyuni-Minjingu. Barabara za mipakani; Alijenga upya Barabara kutoka Arusha-Namanga. Alijenga barabara kutoka Njia panda ya Himo mpaka Tarakea. Alijenga Barabara kutoka Musoma mpaka Sirari. Alijenga barabara kutoka Tanga mpaka Horohoro. Alijenga barabara kutoka Songea mpaka Mbinga ambayo sahivi ndiyo inamaliziwa kuelekea Mbamba Bay wilaya ya Nyasa. Ongezea na wewe km ni mtanzania. Alipanua uwanja wa ndege wa JULIUS NYERERE. Kikwete ndiyo aliyejenga mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar Es Salaam. Hiyo ni baadhi ya miradi na hatukuona makeke yoyote mtu wa watu ni mnyenyekevu mpaka leo.
 
Bomba la umeme linazalisha 60% ya umeme TanzaniA? wewe ni mpumbavu na rofa
 

Nice try, hizo project nyingi unaweza kusema za tangia Mzee Mkapa na alirithi plans nyingi sana mfano barabara za Kusini kutokea Dar kuna sababu kwa nini hata linaitwa Daraja la Mkapa, isitoshe udom mpaka leo hii bado ni underconstruction.

Maraisi wote Tanzania wanarithi miradi aidha mipango au tayari under construction kutoka uongozi uliopita, …
 
Kuna VICHAA watadai hata Daraja la Mwl Nyerere Kigamboni limejengwa na Magufuli
 
Bomba la umeme linazalisha 60% ya umeme TanzaniA? wewe ni mpumbavu na rofa
Hahahah tatizo lenu JPM alijua ni wajinga ndio maana akawageuza mtaji wake. Kumbe ulidhani Maji ndio yanazalisha umeme kuliko gesi? Basi wewe ndio mjinga huku unadhani una akili.

Source: Ewura (2021)
 
Mbona nimetaja hao wote soma para ya mwisho....
 
Utofauti ni kuwa ata akiwa Rais ukiangalia miradi mingi bila uwepo wake isingewezekana, nakupa mfano bwawa la Mwal Nyerere lile Yeye kama yeye kusimama ule mradi ungekufa na hakuna rais yeyeto angeweza kuja kugusa tena, hiyo meli ya mpya Mv Mwanza Hapa kazi tu ni shinikizo lake yeye, Busisi pale ni shinikizo lake, ule mradi wa ujenzi wa njia 8 ulikuwa uende mpaka Chalinze kwa mkopo wa World Bank! Ila World Bank waligoma kutoa hela badae na wakaishia kutoa fedha ya Interchange, Magufuli aliamua Kujenga kwa bajeti ya Tanzania ata kwakuanzia mpaka Kibaha alafu huko mbele tutajua inafikaje Chalinze, kufufua Shirika la ndege ni utashi wake yeye kama yeye tu ila nakukumbusha tena sio kama ndege hazina umuhimu ila sisi wenyewe ni madalali sana wa makabulu, tutashindws kuhudumia zile ndege mwisho wa siku zitauzwa kwa bei chee ata million 500 huko kwa makabulu then wao watazitumia kama alizokaacha Nyerere.

Kingine nikukumbushe kuwa Magufuli ndiye alimshauri Mzee Mkapa kila pato la makusanyo ya mwezi itengwe bilion 2 kwaajili ya ujenzi wa barabara iwe inaenda Tanrods kuliko kusuburi wahusan ambao walikuwa wanajivutavuta.
 
Hivi unajua hiyo gesi ya kikwete ndio unazalisha 60% ya umeme wote Tanzania? Lakini ingekua bwana Fulani duh tusingepumua. Punguzeni ujuaji Kila awamu imefanya miradi mingi tu tusimkuze sana mtu mmoja as if wengine hawakufanya lolote
 
Kama isingewezekana bila JPM imekuaje Sasa hao kina January na Samia tulioambiwa ni mafisadi wamemaliza bwawa na wanalijaza Maji? Au akifanya JPM pekee ndio anaweza wengine hawawezi chochote?
 
Mfuko wa barabara uliasisiwa wakati wa JK? Acha kuongea uongo.
 
Imeisha au bado ipo mingine!
 
Hivi unajua hiyo gesi ya kikwete ndio unazalisha 60% ya umeme wote Tanzania? Lakini ingekua bwana Fulani duh tusingepumua. Punguzeni ujuaji Kila awamu imefanya miradi mingi tu tusimkuze sana mtu mmoja as if wengine hawakufanya lolote
Songas aliianzisha JK? Ni kweli wachina walijenga bomba la gas kutoka Mtwara kwenda Kinyerezi. JK alijenga Kinyerezi Phase 1, 150 MGW. Phase two waliojenga Toshiba, ilifuata wakati wa awamu ya tano.

Kinyerezi one extension ya 185MW iliendelezwa wakati wa awamu ya tano.

Yes JK alifanya kazi. Ila sidhani kama aliifanyia haki kazi aliyoachiwa na Che Mkapa. Tungekuwa mbali sana kama Taifa, kama ile speed ingekuwa maintened
 
Kama isingewezekana bila JPM imekuaje Sasa hao kina January na Samia tulioambiwa ni mafisadi wamemaliza bwawa na wanalijaza Maji? Au akifanya JPM pekee ndio anaweza wengine hawawezi chochote?
Labda kama huna unalolijua kuhusu ilo bwawa, ila unabyomuona Samia na Janauary wanaubunifu wowote? Just be neutral! Samia anavyomuona ni mtu ambae anasumbua kichwa chake kutafuta taarifa? Kubuni vitu?
 
Mfuko wa barabara uliasisiwa wakati wa JK? Acha kuongea uongo.
Uzuri umepata logic nayosema... Road fund ameleta mwingine Barabara kajenga JK..... JK kaweka Bomba JPM kajenga Kinyerezi 2!! And goes on and on. Point ni kwamba Kila Rais alifanya kwa sehemu yake na mwingine kaendeleza so kumtukuza JPM pekee nakusema waliopita hawakufanya kitu inakera sana.
 
Kama isingewezekana bila JPM imekuaje Sasa hao kina January na Samia tulioambiwa ni mafisadi wamemaliza bwawa na wanalijaza Maji? Au akifanya JPM pekee ndio anaweza wengine hawawezi chochote?
How many times the efforts to ditch out the project have failed? Hakuna kitu kinachofanyika gizani kisijulikane mwangani. Mbwembwe za kubeza jina la JPM ndio linalofanya atamkwe sana kwa wema au ubaya.
 
Miaka 10 huwezi kufanya na kumaliza kila kitu. That is not possible. What we miss as a country ni continuity. Tunafanya kama vile kila awamu ni private project ya watu fulani.
We are missing a point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…