Miradi mikubwa haikuanza kipindi cha Hayati Magufuli pekee

Kwanini Nyerere hakujenga na kwanini JPM aliweza kujenga?
Mahitaji ya umeme ya kipindi kile ni sawa na Sasa? Angetumia matrilioni enzi zile ilihali Kulikua Bado hata mashule, Barabara, na hospitali hamna? Huwezi mlaumu Nyerere Kuna wakati priorities zinatofautiana kuendana na mahitaji ya wakati husika. Itafika kipindi hata Internet itafungwa kwenye Kila shule Tanzania maana mahitaji yatalazimu Hilo.
 
Hiyo miradi ya awamu ya Kikwete uliyoorodhesha, Magufuli alikuwepo kama waziri! Hivyo pia miradi hiyo alihusika sana, tena pakubwa. Lakini awamu ya tano, viongozi wa awamu zilizo tangulia hawakuhusika na utekelezaji wake. Hivyo, Kongole liende kwa Magufuli
 
Nani aliyekwambia JK hakuwa waziri kipindi Cha Mkapa? Or hujui hata mkapa alikua kwenye system tokea enzi za Nyerere? Tukienda kwa staili hiyo ndio tutaelewana kwamba Kila kiongozi ameshiriki kwenye miradi na sio kwamba ilianza kwa JK.

Otherwise useme JPM hakufanya mradi wowote akiwa Rais sababu Kulikua na waziri wa ujenzi!! Kama ambavyo JK hakufanya mradi wowote sababu aliyefanya alikua waziri JPM!
 
Dadadeki kawambwa alichemsha ikabidi chuma kitolewe uvuvi kiletwe ujenzi ndani ya wiki lema alikuwa ashikiki alitoka kazi ikafanyika mbele ya chuma mwamba taka chato R.I.P
 
Kikwete alifanya mambo mengi sana wakati wa utawala wa Mkapa yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi aliitangaza vizuri nchi yetu Kimataifa mpaka Ikafutiwa madeni iliyokuwa inadaiwa,Kikwete bado ataendelea kuwa kiongozi muhimu katika nchi yetu,Afrika Mashariki na Sehemu mbali mbali za dunia.
 
Kumbe hata JPM alipokua Rais hakujenga SGR sababu msimamizi hakua yeye Bali makame Mbarawa!! Logic yenu ya kijinga Sana.
Ndo ujue ukiona mradi mkubwa uliofanyika hapa Tanzania tambua Kuna mkono wa magufuli pia umehusika haijalishi akiwa rais au akiwa waziri Kwa hyo magufuli Bado ni habari nyingine mchapakazi hakuwa mpiga Domo ndo maana aliaminika na kupewa hizo wizara na akawamini CCM walipoona chama kipo ICU Bado wakawa hawana budi mwamba awawakilishe kukiokoa japo kuwa walikuwa hawapendi ila Kwa faida ya chama na taifa Kwa ujumla mwamba alipoingia kwenye urais Sasa ndo hapo wale wavivu majizi mafisadi mashoga wauza ngada vyeti feki walipoanza kujinyeanyea na ndio wahanga wanaoteseka na magufuli hivi Sasa!!!!
 
Isipokuwa Magufuli alitaka kuaminisha Wajinga kwamba yeye ndiye alianzisha Tanzania na kila kitu kilichomo
Tanzania ina wajinga kama 80% ya population na Magufuli alijuwa hilo, kawajaza propaganda za uwongo na kuwafanya mtaji wake wa kisiasa.
 
Tanzania ina wajinga kama 80% ya population na Magufuli alijuwa hilo, kawahaza propaganda za uwongo na kuwafanya mtaji wake wa kisiasa.
Kama mbowe jinsi anavyowajaza ujinga Leo hii πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Ukija kinamna hiyo itabidi sasa twende kwa Mainjinia wenyewe waliofanya kazi kwenye saiti ya kujenga hiyo mioindombinu. Maana yeye alikuwa Waziri tu. Mimi nashauri tumfananishe Magufuli Rais na Mkapa au Kikwette Rais, period
 
Acheni double standards, kwahiyo Mama Samia anavyojenga Bwawa la mwalimu Nyerere je JPM ndio yupo site anasimamia mafundi? Au huo mradi wa trillion 60 wa gesi una mkono wa JPM?

Acheni ushamba Kila awamu imefanya miradi maana ipo kwenye Mpango wa taifa whether Rais ni CCM au Chadema itajengwa tu. Tupunguze ushamba kudhani miradi ni ubunifu wa mtu mmoja.
 
We umetokea wapi mkuu au unataka utuoneshe na we unajua kushika kalamu!!! wapi nimemtaja Samia au nimempondea Samia muwe mnasoma thread vizuri siyo kudandia treni Kwa mbele pinguza shobo!!!!
 
Uwanja wa Mpira wa Taifa Magufuli alihusika?Chuo Kikuu Dodoma Magufuri alihusika?Ukumbi wa Bunge Dodoma Magufuri alihusika?TCRA TOWER pale karibu na Mlimani Magufuri alihusika?Ofisi za TRA nchi nzima Magufuri alihusika?
 
Uwanja wa Mpira wa Taifa Magufuli alihusika?Chuo Kikuu Dodoma Magufuri alihusika?Ukumbi wa Bunge Dodoma Magufuri alihusika?TCRA TOWER pale karibu na Mlimani Magufuri alihusika?Ofisi za TRA nchi nzima Magufuri alihusika?
Je hiyo miradi yote uliyoorodhesha kipindi hicho yanatekelezwa magufuli alikuwa katika wizara ipi?tuanzie hapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…