substandard unamaanisha nini. We hakuna unalojua kuhusu ujenzi. Kikwete miradi yake ni mingi ukianzia na huo wa UDOM kujenga chuo kikuu kikubwa kuliko vyote africa mashariki na kati. Mabarabara; Kuunganisha makao makuu ya mikoa karibu yote kwa lami, aliunganisha Dodoma na Iringa, Songea na Mtwara kupitia Tunduru, Nanyumbu na Masasi. Aliunganisha mikoa ya Arusha, Manyara, Singida na Dodoma. Aliunganisha Mbeya na Sumbawanga. Aliunganisha Sumbawanga na Katavi. Aliunganisha Shinyanga na Tabora kupitia Nzega. Aliunganisha Singida na Tabora kupitia Itigi na Uyui. Aliunganisha Mwanza, Geita na Kagera. Alijenga barabara ya lami kutokea Tinde(Shinyanga) kuipitia Kahama mpaka Karagwe mpakani mwa Nchi yetu na Rwanda.
Alijenga upya barabara kutoka Arusha-Makuyuni-Minjingu. Barabara za mipakani; Alijenga upya Barabara kutoka Arusha-Namanga. Alijenga barabara kutoka Njia panda ya Himo mpaka Tarakea. Alijenga Barabara kutoka Musoma mpaka Sirari. Alijenga barabara kutoka Tanga mpaka Horohoro. Alijenga barabara kutoka Songea mpaka Mbinga ambayo sahivi ndiyo inamaliziwa kuelekea Mbamba Bay wilaya ya Nyasa. Ongezea na wewe km ni mtanzania. Alipanua uwanja wa ndege wa JULIUS NYERERE. Kikwete ndiyo aliyejenga mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar Es Salaam. Hiyo ni baadhi ya miradi na hatukuona makeke yoyote mtu wa watu ni mnyenyekevu mpaka leo.