Mirathi ya Kobe Bryant yazua gumzo USA, utajiri wote wagawanywa kwa mke na watoto huku wazazi wakiishi kimaskini

Utamu uko wapi sasa hapo?!
 
Huna mtoto wewe eti mpenzi mtazamaji .
....hta wewe utazeeka na unakuta umefanya effort ila pesa ulilipia ada watoto na wakipata baadae wasikuangalie wewe Uwe mpenzi mtazamaji ni wao na wake zao tu how will you feel?fucking ushauri....
Kutunza wazazi ni hisani tu, sio wajibu.
Wazazi wanatakiwa watafute pesa zao wawaachie watoto wao urithi.
 
Kw nini wazazi wake hawakutafuta pesa ??
 
Eti wakamzaa Kobe [emoji23][emoji23]
 
Huu ujinga ndio sitarajii kufanya kama nitakuwa na mali nyingi.

Tunafika pahali tulipo ndugu na wazazi wakiwa wamepambana kwa jasho na damu tena kwa kuuza mali zao, tena kwa kujinyima kula na kuvaa.

Tukishapata mali na mungu akatuchukua wanabaki wanafaidi mke na watoto ambao kiuhalisia hawana mchango wowote wewe kufika hapo ulipo zaidi ya kutumia walichokukuta nacho.

Mtu kama umejaliwa mali andika mapema angalau 35% hadi 40% irudi kwa familia yako waliokutengeneza kufika hapo ulipo.
 
Ni wajibu wa kisheria na maadili wazazi kulea na kutunza watoto wanaowazaa, sio wajibu wa watoto kutunza waliowazaa, ni hisani tu. Ndio maana mzazi anaweza kupelekwa mahakamani akaamriwa na mahakama kisheria kutoa matunzo ya mtoto ila mtoto hawezi kupelekwa mahakamani akaamriwa kutoa matunzo ya wazazi au ndugu.
 
Nimeshaamua hivyo, Mali zangu lazima wazazi wangu wafaidi, wao ndio walionitengeneza. Imefika hatua wanaume tunatafuta mali za kunufaisha ukweni.

Ukiondoka wanaobaki wanakenua meno na kufaidi mali zako ni mke, watoto na ndugu wa mkeo. Huu upumbavu sifanyi
 
Ni haki yako kuamua hivyo, ila usiwashangae au kuwazodoa wanaoamua tofauti na hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…