Mirathi ya nyumba iliyojengwa na mjane yazua balaa; ukoo wa mume na ukoo wa mke wanaigombania

Kiwanja kilikua cha mume lakin kwa msingi huo wana haki na jasho la ndugu yao
Mume alifariki kitambo mirathi ikagawanywa mama akachukua chake kwa maana hiyo kiwanja kilikiwa Mali hali ya mke .Na ikumbukwe ndoa ya Kikristo kifo kinaimaliza,maana hiyo hakuwa mke wa mtu Tena baada ya kifo mumewe.Sasa ndugu wa mume Mali inawahusuje hapo.
 
Upande wa huyo mama wanazingua. Mke kama aliolewa na mahari ilishatolewa, baada ya kufiwa na mumewe hakuolewa maana yake ni kwamba kila kitu hapo ni halali ya ukoo wa mume.

Hao wapogoro waache ujinga.
Hapana ndoa huvunjwa na kifo huyo alikuwa single wakati kifo kinamchukua
 

Ngoja utaona sheria itakavyoamua ndio utajua nani tapeli
 
Haijalishi kazikwa wapi. Ukweli ni kuwa alikuwa single na no longer wife wa late husband.
Kweli kabisa chief.Hebu wajiulize huyu mjane angeamua kuuza baada ya kifo Cha mwanae walikuwa na nguvu ya kumzuia hao ndugu wa mume.Kama hapana amini Mali za ndugu Yao mwanaume ziliisha baada ya kugawiwa mjane baada ya mwanae kufa.Ndugu wa mume wajitafakar
 
wewe kwa akili yako ndogo huyo mama alioa au aliolewa.?
 
Tofautisha single na mjane.
Yaani wasomi WA siku hizi hata Akili ya kuchambua mambo hamna.
Mjane/single wote hawana waume na wanaweza kuolewa tena. Jikite kwenye hoja na si kuanza kuleta dharau.
 
1.Kuzika marehemu siyo kigezo au sababu ya kuwa na uhalali wa kisheria wa kurithi mali za marehemu uliyemzika.
2.Sheria ya Mirathi inawatambua warithi halali ni (i) Mjane (ii) Watoto wa Marehemu (iii) Wazazi wa Marehemu.
Endapo kama wote hawa hawapo, basi, ndugu zake wa karibu ndio wanaofuata kuwa warithi halali. Ndugu hao ni kama vile dada zake wa damu, kaka zake wa damu, n.k.
3. Kwa kuwa mume wa huyo mama marehemu alitangulia kufa, kisheria hali hiyo inajulikana kama "kaukimbia urithi" kwenye mali/ardhi inayomilikiwa kwa umiliki wa maslahi ya pamoja yasiyogawanyika (joint occupation or matrimonial property ownership), hivyo, ndugu wa huyo mume hawana haki yoyote ile kwenye hizo mali/nyumba kwani ndugu yao alijitoa mapema kwenye umiliki wa hiyo nyumba na kisha umiliki huo wote kuhamia kwa mkewe na mtoto waliobaki hai.
4. Ndugu wa huyo mama wanapaswa kufungua kesi ya mirathi ya usimamizi wa mali za huyo mama na wamteue msimamizi wa mirathi, hao ndugu wa mume wa marehemu endapo kama watakuwa na pingamizi lolote basi watawasilisha huko Mahakamani, na kwa vyovyote vile pingamizi hilo lazima litakosa mashiko na litatupiliwa mbali na Mahakama.
5.Mwisho.
Mali na nyumba zote za huyo mjane ni urithi halali kwa ndugu zake, ndugu wa mumewe hawana haki ya kurithi mali hizo.
 
Nendeni mkaolewe na hao wenye tamaa ya mali ,siku wanaume zenu wakifa ndo mtaona kila rangi kuna watu hawana utu kisa ya mali.
 
Kesi si kesi, kifo si taraka ndiyo sababu mpogoro alizikwa Moshi, mke alirithi mali za mumewe na zake hivyo upande wa mke hauna chao kwani walikwishalipwa chao(mahali).
 


Umasikini kitu kibaya sana
Sasa wewe baba yangu, kaka yangu, mjomba wangu unaendaje kugombea Mali ukweni nilikoolewa mimi lakini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…