Misa ya Mkapa: Nimeona tofauti kubwa kati ya maaskofu wa Katoliki na wale wa makanisa kama la Gwajima!

Misa ya Mkapa: Nimeona tofauti kubwa kati ya maaskofu wa Katoliki na wale wa makanisa kama la Gwajima!

Kuna watu hawana akili, na ndio hao wanakuwa mboga za matapeli kama akina Gwajima, Marehemu Mam Lwaikatare, MWINGIRA, na kadhalika. Hao wote ni wapiga dili zao binafsi, ni kundi la mashetani, huwezi wafananisha na watu wanao fanya kazi ya Mungu kwa dhati.
Kuna tofauti kati ya kufananisha na kulinganisha!
 
Kiukweli katika madhehebu yanayozingatia muda Katholic wanaongoza,wanakwenda kwa muda sahihi,tofauti na madhehebu mengine,nimesali madhehebu tofauti tofauti nimeona jinsi gani mengine wasivyozingatia muda
Hakika mkuu.

Ile misa ya Mkapa ingeongozwa na Lusekelo tungekesha pale uwanjani..... Sadaka pekee zingekuwa zaidi ya 10!
 
Lutheran wanafanana na Anglican wale wanaoitwa Low Church mfano Dodoma.

Katoliki wanafanana na Anglican High Church mfano Tanga/Zanzibar
Hivi nan alianzisha hili dhehebu lililojikita ulimwenguni pote au Paulo kama. Sio petro
 
John, unalinganisha self proclaimed Bishops na Consecrated Bishops !
 
Hivi nan alianzisha hili dhehebu lililojikita ulimwenguni pote au Paulo kama. Sio petro
Ukatoliki ni mapango wa shetani katika kulififisha Kanisa la Kristo duniani. NI WAABUDU SANAMU!

"WATU HAWA HUNIABUDU KWA MIDOMO YAO ILA MIOYO YAO IKO MBALI NAMI. NAO WANIABUDU BURE,WAKIFUNDISHA MAFUNDISHO YA WANADAMU."
 
Ulitaka wafanane? Umeshatofautisha huduma zao sasa unataka wafanane vipi? Au umevutiwa na kanzu na lugha ya upole? Unataka hao wengine watoe pepo kwa kubembeleza? Hata Yesu hakufanya hivyo. Ni mitazamo tu.
Yesu hakuwahi kupiga kelele na kurukaruka madhabahuni kama baadhi ya matapeli wa kutumia dini wanavyofanya.

Yesu tena alisema, jifunzeni kwangu kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu. Na tena maandiko yanasema, Yesu hata wakati wa kuteswa kwake na hata katika safari yake ya kuelekea kwenye kifo cha mwili, alibakia mpole na mnyenyekevu kama kondoo anayepelekwa kuchinjioni.

Hawa wapiga kelele labda kuna wanayemuiga lakini siyo Kristo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukatoliki ni mapango wa shetani katika kulififisha Kanisa la Kristo duniani. NI WAABUDU SANAMU!

"WATU HAWA HUNIABUDU KWA MIDOMO YAO ILA MIOYO YAO IKO MBALI NAMI. NAO WANIABUDU BURE,WAKIFUNDISHA MAFUNDISHO YA WANADAMU."
Nakuona mfuasi wa Ellen G White katika ubora wako [emoji23][emoji23][emoji23] Usishindane na kanisa la Kristo!

MT 6: 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
 
Kanisa linapimwa kwa kutumia nini mkuu?
Wewe bila shaka utakua ni mpumbavu ambaye huelewi kitu.

Wewe una uwezo wa kulipima kanisa. Mwenye uwezo ni Mungu peke yake.

Hivyo hiyo kazi mwachie Mungu. Mungu ndiye anayejua ni yepi makanisa ya kweli. Yale yaliyo jengwa kwa msingi wa Yesu Kristo Mungu wetu wa kweli.
Alama Kuu za kanisa Takatifu
1) Liwe Kanisa la Kristo ambalo yeye mwenyewe Kristo alilijenga juu ya mwamba (Petro)
2) Liwe la mitume
3) Liwe linalotoa mafundisho matakatifu
4) Liwe catholic (yaani lililoeneo Duniani kote) maana Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake, nendeni Duniani kote. Kama walienda Duniani kote basi walilisimika Kanisa lake Duniani kote.

Kuna makanisa ambayo ni ya wanadamu, yameanzishwa na wanadamu, yanamilikiwa na wanadamu.

Lakini Kristo alianzisha Kanisa lake. Na kwa maneno yake alisema, 'Simon kuanzia sasa utaitwa Petro (from the greek word Petera means rock), na juu ya hiyo petera nitajenga Kanisa langu. Kwa hiyo Kanisa la Kristo, alilolianzisha Kristo alilijenga juu ya Petro. Kristo hakuanzisha makanisa bali alianzisha Kanisa. Ubinafsi uliwafanya wanadamu kujianzishia makanisa yao. Ndiyo maana leo utasikia Kanisa la Kakobe, Kanisa la Gwajima, Kanisa la mchungaji God, Kanisa la Luther, Kanisa la Motovia, n.k. Na kuna wajristo wanaenda kwenye makanisa haya ya watu binafsi! Ama kweli, ni utimilifu wa manebo yale, 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'.

Ukweli ni kuwa wanadamu hatutakiwi kuwa na makanisa, Kristo pekee yake ndiye mwenye Kanisa, nasi tulistahili kuwa wafuasi tu wa Kanisa lake lakini siyo sisi kujianzishia makanisa yetu halafu tunajiita ni wakristo. Wakristo, ni wafuasi wa Kristo, ni waumini wa Kanisa la Kristo, siyo la Gwajima au la Kakobe au la mwingine awaye yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani katoliki ndio kanisa halisi?

Kama ilivyo kwa Gwaji boy ndivyo ilivyo kwa katoliki wote ni wapita njia tu na wasanii wakubwa

Mwanzilishi wa ukristo hakuwahi kutembea na silaha wala walinzi wa kumlinda na wala hakuwahi kuwaagiza wafuasi ama watumishi wake wajilinde kwa silaha ama walinzi.

Leo hii maparoko wanahubili huku wakiwa na bastora ktk kanzu zao 😂😂maana yake nn? 😔
Hawajawahi kumwamini huyo wanaye mhubiri sasa tuseme nn juu ya hilo je ni kanisa la Kristo? Hapana kwa taarifa yako ktk hiyo ibada kanisani kulijaa bastora zilizofichwa ktk makoti na makanzu ili kujilinda ama kuwalinda watu fulani

Gwajima & katoliki wote ni wasanii tu ila kanisa la kweli halitegemei guns ama walinzi kuwalinda watumishi
 
Mzee wetu "belongs to many societies in his faith" Wakatoliki wamekwisha maliza heshima yao kwake, bado tusubiri wale wa "Paris Club" ambao ni lazima "chronologically" Mkulu wetu akapate kuwa ndiye mwana mrithi na kupewa ile pete ya maagano.

Ile zawadi ya tausi wale, wale, wale! Nje ya maagano ya mbio za mwenge wa uhuru, ni balaa tupu, ni misiba baada ya misiba. Ingawaje ni " consipiracy theory" bali yanayokwenda kutokea ni kifo rasmi ya chama tawala. Mods lirudisheni jukwaa la dini/imani ili yale yaliyokusudiwa kwa taifa hili, watumishi wa Mungu aliye hai wakapate kuyaweka hadharani.
Bado sijakuelewa
 
Kasome biblia uimalize yote ukianza kuhubiri hutohubiri kwa kuwabembeleza watu, utahubiri kwa nguvu zote tena kwa sauti kubwa. usije ukadhani wanapenda kuhubiri vile yule ni Roho mtakatifu akisha jaa unajikuta unahubiri kwa nguvu.
Hahahahaha JUHA WEWE KWELIKWELI
 
Alama Kuu za kanisa Takatifu
1) Liwe Kanisa la Kristo ambalo yeye mwenyewe Kristo alilijenga juu ya mwamba (Petro)
2) Liwe la mitume
3) Liwe linalotoa mafundisho matakatifu
4) Liwe catholic (yaani lililoeneo Duniani kote) maana Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake, nendeni Duniani kote. Kama walienda Duniani kote basi walilisimika Kanisa lake Duniani kote.

Kuna makanisa ambayo ni ya wanadamu, yameanzishwa na wanadamu, yanamilikiwa na wanadamu.

Lakini Kristo alianzisha Kanisa lake. Na kwa maneno yake alisema, 'Simon kuanzia sasa utaitwa Petro (from the greek word Petera means rock), na juu ya hiyo petera nitajenga Kanisa langu. Kwa hiyo Kanisa la Kristo, alilolianzisha Kristo alilijenga juu ya Petro. Kristo hakuanzisha makanisa bali alianzisha Kanisa. Ubinafsi uliwafanya wanadamu kujianzishia makanisa yao. Ndiyo maana leo utasikia Kanisa la Kakobe, Kanisa la Gwajima, Kanisa la mchungaji God, Kanisa la Luther, Kanisa la Motovia, n.k. Na kuna wajristo wanaenda kwenye makanisa haya ya watu binafsi! Ama kweli, ni utimilifu wa manebo yale, 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'.

Ukweli ni kuwa wanadamu hatutakiwi kuwa na makanisa, Kristo pekee yake ndiye mwenye Kanisa, nasi tulistahili kuwa wafuasi tu wa Kanisa lake lakini siyo sisi kujianzishia makanisa yetu halafu tunajiita ni wakristo. Wakristo, ni wafuasi wa Kristo, ni waumini wa Kanisa la Kristo, siyo la Gwajima au la Kakobe au la mwingine awaye yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umechangia vyema sana kati ya wachangiaji wote.Lazima utakuwa Shemasi au Frateri! Hongera kwa kazi nzuri ya utume na endelea kuutangaza ukweli kusudi watu waujue.
 
Imani ya makanisa ya Kikatoliki, na makanisa yote ya kiprotestanti k.v Lutheran, Anglikana, Moravian, Menonite, nk ni makanisa yanayomwabudu Mungu kwa kuishia kwenye nafsi. Nafsi ya mwanadamu imeundwa na components kuu tatu UTASHI, AKILI, na HISIA. Ibada zao zote huwa hazivuki hapa na kuingia rohoni.

Ibada zao zimekaa kiakili-akili, na kihekima-hekima tu,,. Ndio maana utakuta mtu anaitwa askofu mkuu ila hawezi kukemea viumbe vya rohoni kama mapepo/majini, ... kwa sababu roho hizi chafu hukemewa kwa namna ya rohoni.

Ninapoyasema haya sio kwamba ninamsapoti Gwajima, ila lipo Kanisa la kweli (sio Gwajima, na sio Katoliki). Ukitaka kulijua nitafute.

Jesus is Lord .
Nikutafute !!!??? Pole na Pole kweli
 
Back
Top Bottom