Alama Kuu za kanisa Takatifu
1) Liwe Kanisa la Kristo ambalo yeye mwenyewe Kristo alilijenga juu ya mwamba (Petro)
2) Liwe la mitume
3) Liwe linalotoa mafundisho matakatifu
4) Liwe catholic (yaani lililoeneo Duniani kote) maana Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake, nendeni Duniani kote. Kama walienda Duniani kote basi walilisimika Kanisa lake Duniani kote.
Kuna makanisa ambayo ni ya wanadamu, yameanzishwa na wanadamu, yanamilikiwa na wanadamu.
Lakini Kristo alianzisha Kanisa lake. Na kwa maneno yake alisema, 'Simon kuanzia sasa utaitwa Petro (from the greek word Petera means rock), na juu ya hiyo petera nitajenga Kanisa langu. Kwa hiyo Kanisa la Kristo, alilolianzisha Kristo alilijenga juu ya Petro. Kristo hakuanzisha makanisa bali alianzisha Kanisa. Ubinafsi uliwafanya wanadamu kujianzishia makanisa yao. Ndiyo maana leo utasikia Kanisa la Kakobe, Kanisa la Gwajima, Kanisa la mchungaji God, Kanisa la Luther, Kanisa la Motovia, n.k. Na kuna wajristo wanaenda kwenye makanisa haya ya watu binafsi! Ama kweli, ni utimilifu wa manebo yale, 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'.
Ukweli ni kuwa wanadamu hatutakiwi kuwa na makanisa, Kristo pekee yake ndiye mwenye Kanisa, nasi tulistahili kuwa wafuasi tu wa Kanisa lake lakini siyo sisi kujianzishia makanisa yetu halafu tunajiita ni wakristo. Wakristo, ni wafuasi wa Kristo, ni waumini wa Kanisa la Kristo, siyo la Gwajima au la Kakobe au la mwingine awaye yeyote.
Sent using
Jamii Forums mobile app