Misa ya Mkapa: Nimeona tofauti kubwa kati ya maaskofu wa Katoliki na wale wa makanisa kama la Gwajima!

Kuna tofauti kati ya kufananisha na kulinganisha!
 
Kiukweli katika madhehebu yanayozingatia muda Katholic wanaongoza,wanakwenda kwa muda sahihi,tofauti na madhehebu mengine,nimesali madhehebu tofauti tofauti nimeona jinsi gani mengine wasivyozingatia muda
Hakika mkuu.

Ile misa ya Mkapa ingeongozwa na Lusekelo tungekesha pale uwanjani..... Sadaka pekee zingekuwa zaidi ya 10!
 
Lutheran wanafanana na Anglican wale wanaoitwa Low Church mfano Dodoma.

Katoliki wanafanana na Anglican High Church mfano Tanga/Zanzibar
Hivi nan alianzisha hili dhehebu lililojikita ulimwenguni pote au Paulo kama. Sio petro
 
John, unalinganisha self proclaimed Bishops na Consecrated Bishops !
 
Hivi nan alianzisha hili dhehebu lililojikita ulimwenguni pote au Paulo kama. Sio petro
Ukatoliki ni mapango wa shetani katika kulififisha Kanisa la Kristo duniani. NI WAABUDU SANAMU!

"WATU HAWA HUNIABUDU KWA MIDOMO YAO ILA MIOYO YAO IKO MBALI NAMI. NAO WANIABUDU BURE,WAKIFUNDISHA MAFUNDISHO YA WANADAMU."
 
Ulitaka wafanane? Umeshatofautisha huduma zao sasa unataka wafanane vipi? Au umevutiwa na kanzu na lugha ya upole? Unataka hao wengine watoe pepo kwa kubembeleza? Hata Yesu hakufanya hivyo. Ni mitazamo tu.
Yesu hakuwahi kupiga kelele na kurukaruka madhabahuni kama baadhi ya matapeli wa kutumia dini wanavyofanya.

Yesu tena alisema, jifunzeni kwangu kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu. Na tena maandiko yanasema, Yesu hata wakati wa kuteswa kwake na hata katika safari yake ya kuelekea kwenye kifo cha mwili, alibakia mpole na mnyenyekevu kama kondoo anayepelekwa kuchinjioni.

Hawa wapiga kelele labda kuna wanayemuiga lakini siyo Kristo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukatoliki ni mapango wa shetani katika kulififisha Kanisa la Kristo duniani. NI WAABUDU SANAMU!

"WATU HAWA HUNIABUDU KWA MIDOMO YAO ILA MIOYO YAO IKO MBALI NAMI. NAO WANIABUDU BURE,WAKIFUNDISHA MAFUNDISHO YA WANADAMU."
Nakuona mfuasi wa Ellen G White katika ubora wako [emoji23][emoji23][emoji23] Usishindane na kanisa la Kristo!

MT 6: 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
 
Alama Kuu za kanisa Takatifu
1) Liwe Kanisa la Kristo ambalo yeye mwenyewe Kristo alilijenga juu ya mwamba (Petro)
2) Liwe la mitume
3) Liwe linalotoa mafundisho matakatifu
4) Liwe catholic (yaani lililoeneo Duniani kote) maana Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake, nendeni Duniani kote. Kama walienda Duniani kote basi walilisimika Kanisa lake Duniani kote.

Kuna makanisa ambayo ni ya wanadamu, yameanzishwa na wanadamu, yanamilikiwa na wanadamu.

Lakini Kristo alianzisha Kanisa lake. Na kwa maneno yake alisema, 'Simon kuanzia sasa utaitwa Petro (from the greek word Petera means rock), na juu ya hiyo petera nitajenga Kanisa langu. Kwa hiyo Kanisa la Kristo, alilolianzisha Kristo alilijenga juu ya Petro. Kristo hakuanzisha makanisa bali alianzisha Kanisa. Ubinafsi uliwafanya wanadamu kujianzishia makanisa yao. Ndiyo maana leo utasikia Kanisa la Kakobe, Kanisa la Gwajima, Kanisa la mchungaji God, Kanisa la Luther, Kanisa la Motovia, n.k. Na kuna wajristo wanaenda kwenye makanisa haya ya watu binafsi! Ama kweli, ni utimilifu wa manebo yale, 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'.

Ukweli ni kuwa wanadamu hatutakiwi kuwa na makanisa, Kristo pekee yake ndiye mwenye Kanisa, nasi tulistahili kuwa wafuasi tu wa Kanisa lake lakini siyo sisi kujianzishia makanisa yetu halafu tunajiita ni wakristo. Wakristo, ni wafuasi wa Kristo, ni waumini wa Kanisa la Kristo, siyo la Gwajima au la Kakobe au la mwingine awaye yeyote.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani katoliki ndio kanisa halisi?

Kama ilivyo kwa Gwaji boy ndivyo ilivyo kwa katoliki wote ni wapita njia tu na wasanii wakubwa

Mwanzilishi wa ukristo hakuwahi kutembea na silaha wala walinzi wa kumlinda na wala hakuwahi kuwaagiza wafuasi ama watumishi wake wajilinde kwa silaha ama walinzi.

Leo hii maparoko wanahubili huku wakiwa na bastora ktk kanzu zao 😂😂maana yake nn? 😔
Hawajawahi kumwamini huyo wanaye mhubiri sasa tuseme nn juu ya hilo je ni kanisa la Kristo? Hapana kwa taarifa yako ktk hiyo ibada kanisani kulijaa bastora zilizofichwa ktk makoti na makanzu ili kujilinda ama kuwalinda watu fulani

Gwajima & katoliki wote ni wasanii tu ila kanisa la kweli halitegemei guns ama walinzi kuwalinda watumishi
 
Bado sijakuelewa
 
Kasome biblia uimalize yote ukianza kuhubiri hutohubiri kwa kuwabembeleza watu, utahubiri kwa nguvu zote tena kwa sauti kubwa. usije ukadhani wanapenda kuhubiri vile yule ni Roho mtakatifu akisha jaa unajikuta unahubiri kwa nguvu.
Hahahahaha JUHA WEWE KWELIKWELI
 
Umechangia vyema sana kati ya wachangiaji wote.Lazima utakuwa Shemasi au Frateri! Hongera kwa kazi nzuri ya utume na endelea kuutangaza ukweli kusudi watu waujue.
 
Nikutafute !!!??? Pole na Pole kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…