Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Pascal Mayalla umenena kiungwana kabisa.
Sio Sweden pekee bali nchi zote za Scandnavia, utsjikuta upo super market na Waziri mkuu bila kujua, mara nyingine wanaendesha hadi baiskrli mtaani, nimeliona Denmark.
Kuona polisi hasa wa usalama barabarani ni mara chache sana.
Misafara ya Tz inaboa, inapoteza muda na pesa nyingi, imejini umezuia watu 3,000 kwa nusu saa wanapoteza kiasi gani?
Hii ni kila siku kwa barabara tofauti za jiji la Dar.
Lingine ni uongo mtupu wananchi kuzuia misafara hilo nakataa, anayebisha ajaribu kusimama barabarani msafara wa raisi ukikaribia kama hutauawa.
Hivi rais huwa amejipanga saa ngapi kuhutubia hao wananchi na kueleza changamoto zao kama sio smepangwa na wananchi wameandaliwa?
TUACHE KUDANGANYANA
 

Kuna siku nilikuwa nakaribia kuingia Shinyanga nikakutana na dhahama hiyo ya kusimamishwa kwa ajili ya msafara lakini raia wema wakanionyesha njia ya kuingia mjini bila tatizo nikaitumia na wakati huo huo gari nyingine ya mwenzangu ilikuwa nyuma yeye hakupata bahati ya kuelekezwa njia niliyotumia mimi, basi pale mjini napo nilipokaribia Chuo cha Veta nikaambiwa niweke kushoto lakini napo nikapata uchochoro kushoto kwa barabara ndani ndani baadae kwa mbele nikarudi barabarani nikaendelea na safari yangu hadi nilipokaribia Nzega ndio nikasimamishwa na ndipo msafara ukapita wakati huo namuuliza mwenzangu yupo wapi yeye anasema bado yupo Shinyanga kazuiliwa na Askari..Kuna kitu tunakosa akilini mwetu?
 
Kweli muda mwingine ni kero...lakini kwa hili viongozi wetu wa mikoani wa kisiasa wakishirikiana na wa kitaifa ndo wametufanya wananchi kuwa hivi ...unakuta kero za kutatuliwa na level ya ngazi ya chini hadi isubiri msafara wa Rais ...halafu wanaanza kuhamasisha WATU Rais atapita wananchi mjitokeze kumlaki ilihali msafara huo unaenda mkoa Mwingine tofauti na aliposimama kwangu kiongozi kama Rais akienda mkoa kama wa Mwanza akitoa Dodoma haina haja ya kusimama simama mikoa ambayo hana ratiba ya kiziara pale, kama anapita barabani bora apitilize na apange ratiba ya kufika eneo hilo lenye tatizo siku nyingine ..

Kupangana barabara ni utumwa pia ..dunia ya sasa tunaheshimu sana muda (time values) muda ni rasimali ambayo ni haiguswi..
Tujitafakari Rais akipita ahakikishiwe usalama wake lakini pia ahakikishe wengine wanapata haki zao ...yaliyotokea barabara ya MWANZA akiwa Kahama inatia hasira, Rais yupo Kahama gari zinasimamishiwa Singida...takriban masaa 5 haijalishi mpo sehemu ya por wala wapi, haijalishi hali za watu kama ni wagonjwa ,wajawazito watoto wazee...
Jeshi la polisi na vyombo vingine vya kiitelejensia tafuteni mbinu mbadala ya kutatua kero hii .
 
Nilikuwa mdogo, shule ya msingi. Tulikuwa tukimsubiri Nyerere apite toka Mwanza kwenda Musoma tangu saa 4 asubuhi mpaka saa 10. Akipita nilichokuwa nakiona ni mkono akitupungia, gari mbili mbele, yake kati na mbili nyuma. Hapakuwa na pikipiki, nahisi kwa umbali wa mwendo. Msururu wa magari leo ni utukufu wa viongozi miungu watu, wanao simama barabarani kuongea na watu waliopangwa na wachumia tumbo, barabara zikiwa zimefungwa.
 
Mbwa za kiafrika haziwezi kufanya haya. Wao ukuu ndiyo first priority kwao.
Miafrika abadani haitakuja kuwa developed kuendana na kasi za wenzetu hata ikisoma kiasi gani. Uafrika ni laana tu mi naona.
 
Uku kwetu sisi ukisikia waziri furani anakuja idara zote zinawasha magari yani anakuja waziri wa michezo unashangaa kwenye msafara yupo mkuu wa idara ya kilimo, elimu, mipango 😀😀😀 wanafunga ofisi uko siku nzima kisa kuna ugeni
 
Nilitoka tunduma saa mbili asubuhi nilikuwa nasafiri na air tz songwe to dar,nilifika songwe airport saa tatu na nusu tayari kuanza hatua za ukaguzi ili tuingie kwenye ndege,basi nakaribia kuingia lounge ikaja taarifa kuwa ndege tunayotarajia kutumia ndio mh anatarajia kutoka nayo Malawi basi tumekaa pale songwe huku naona hotuba yake Malawi live tbc,amekujakuingia mbeya kama sijakosea saa kumi au zaidi basi tukaanza kupanga folen ili tuingie kwenye ndege Mara ndege ikaondoka tukataarifiwa tusubiri bombadear inatoka mwanza ilipokuja ikabeba baadhi ya watu sisi tukasubiri trip ya pili ambayo nadhani ilikuwa zaidi ya saa 12,watu walichoka sana na mipango mingi ilivurugika

Maana yangu kuandika haya nikuwataka wenye mamlaka wakati mwingine kujaribu kuheshimu muda wa watu wengine mfano rais anatoka Malawi saa kumi jioni kuna haja gani yakuweka watu uwanjani toka asubuhi?kwanini tusingepewa taarifa kabla kuwa nitakuwa na mabadikiko ya muda wa safari?hili kwetu sisi linaweza lisiwe na madhara makubwa ila kumbuka pale kuna wasafiri wamataifa mbali mbali wanachukuliaje hili
 
Yaani wewe huwa huelewagi na huelewekagi.
Ungesema je kwa Mabeberu kiongozi wa nchi anapopita huwa anaunga foleni na yeye ili na sisi tujifunze

Ila Kumbuka jamii yetu bado tupo nyuma kwa kifupi hatujastaarabika.
 
Visingizio
 
Another stupid excuse
 
Hii ni kero sana kuwasubirisha watu zaidi ya masaa matano. Wangejiwekea standard ya walau dk 15. Kwa jinsi ulivyosema hapo mbona inawezekana kabisa sio teknolojia kubwa sana ni ya kawaida tu. Tunaweza kusimamisha magari kwa muda usiozidi dk 15 kiongozi akawa ameshapita watu wakaendelea na shughuli zao.

Alafu kibaya zaidi siku hizi kila kiongozi ana motorcade yaani mpaka naibu waziri anasimamishiwa magari hii ni hatari sana kwa maendeleo yetu. Muda ni mali jamani.
 
Mdomo Mwepesi, karibu, shuhudia jinsi ninavyosifu
P.
 
Inchi hii ya visasi na vinyongo hilo litaleta balaa,na msingi mama wa haya yote ni kupuuzwa kwa demokrasi hivyo kusababisha viongozi kujiona hawapo kihalali hivyo kuhitaji ulinzi mkali kila wakati.(
 
Huyu Bwana Pascal Mayalla ni Janga kweli, bado anaamini kuwa Rais atamfikiria
Jamii ya Kujipendekeza na Kusifu tu! Hovyo kabisa.
Hapa ni juzi tuu nasifu msafara wa kiongozi fulani ili niteuliwe.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…