Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Pascal Mayalla umenena kiungwana kabisa.
Sio Sweden pekee bali nchi zote za Scandnavia, utsjikuta upo super market na Waziri mkuu bila kujua, mara nyingine wanaendesha hadi baiskrli mtaani, nimeliona Denmark.
Kuona polisi hasa wa usalama barabarani ni mara chache sana.
Misafara ya Tz inaboa, inapoteza muda na pesa nyingi, imejini umezuia watu 3,000 kwa nusu saa wanapoteza kiasi gani?
Hii ni kila siku kwa barabara tofauti za jiji la Dar.
Lingine ni uongo mtupu wananchi kuzuia misafara hilo nakataa, anayebisha ajaribu kusimama barabarani msafara wa raisi ukikaribia kama hutauawa.
Hivi rais huwa amejipanga saa ngapi kuhutubia hao wananchi na kueleza changamoto zao kama sio smepangwa na wananchi wameandaliwa?
TUACHE KUDANGANYANA
 
Ndg Pasco wewe umekuwa na bahati umesimamishwa 30 minutes tu, juzikati wakati mheshimiwa anaenda mapumzikoni nyumbani, akiwa bado Singida kama sijakosea, tayari Nzega magari yalishasimamishwa. Yaani karibia masaa 4 bila kujali kama msafara umesimamishwa na wananchi wanaompenda mheshimiwa na kufunga barabara ili walau wampongeze. Hii hali imekuwa shida sana kwakweli japo ulinzi wa viongozi wetu pia ni muhimu sana ili walau magari yasimamishwe pale wanapokuwa wanakaribia.

Kuna siku nilikuwa nakaribia kuingia Shinyanga nikakutana na dhahama hiyo ya kusimamishwa kwa ajili ya msafara lakini raia wema wakanionyesha njia ya kuingia mjini bila tatizo nikaitumia na wakati huo huo gari nyingine ya mwenzangu ilikuwa nyuma yeye hakupata bahati ya kuelekezwa njia niliyotumia mimi, basi pale mjini napo nilipokaribia Chuo cha Veta nikaambiwa niweke kushoto lakini napo nikapata uchochoro kushoto kwa barabara ndani ndani baadae kwa mbele nikarudi barabarani nikaendelea na safari yangu hadi nilipokaribia Nzega ndio nikasimamishwa na ndipo msafara ukapita wakati huo namuuliza mwenzangu yupo wapi yeye anasema bado yupo Shinyanga kazuiliwa na Askari..Kuna kitu tunakosa akilini mwetu?
 
Wanabodi,

Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"
Ukiondoa thamani ya uhai, hakuna kitu kingine duniani chenye thamani kama muda, time is money, kupotezeana muda ni kuzorotesha maendeleo.

Niko njia ya Bagamoyo eneo la Mbezi Tangi Bovu, tumesimamishwa karibu dakika 30 kupisha msafara wa Kiongozi fulani anatokea njia ya Bagamoyo.

Huku kusimamishana babarani nusu saa nzima, kisa anapita kiongozi, ilikuwa ni zile enzi za ujima, kwenye dunia ya sasa ya the age of information science, unamsimamisha mtu dakika 30 kupisha msafara wa kiongozi ni kupotezaana muda. Wengine kazi zetu zina very tight deadlines, kama zilivyo tender deadlines, umechelewa hata dakika moja, imekula kwako.

Ndio maana sisi tunawasisitiza viongozi wetu, wasiopenda kusafiri nchi za watu kwa lengo la kubana matumizi, mara moja moja wasafiri tuu kwenda nchi za Ulaya na Amerika, sio kwa ajili ya kwenda kuponda raha, au kubembea hewani kwa kukwea pipa bali kusafiri ili kwenda kupata tuu exposure, wenzetu wakoje na wanafanyaje mambo yao.

Msafara wa magari zaidi ya 15, ulipopita, umepita kwa mwendokasi wa speed 150 kph, na umbali wa Bagamoyo Mbezi Beach, ni appx 50km, hivyo kwa mwendokasi huo, msafara unatumia just 20 minutes, hivyo akina sisi tumesimamishwa huku majiani, kabla hata msafara haujafika Bagamoyo!.

Nimeelezwa kinachochelewesha misafara ya viongozi ni wananchi kujitokeza kwa wingi kufunga barabara kuzuia msafara ili wamsalimie kiongozi. Yaani msafara wa kiongozi at 140kph mbele una escorts 3 as advance, then kuna sweeper, halafu wananchi wanajotokezea tuu kuusimamisha msafara ili wamsalimie kiongozi, na kweli msafara at 140kpm unasimama ghafla kiongozi asalimiwe, huku sisi tukisubirishwa!. Siulizi if its true true msafara unasimamishwa ghafla na wananchi wenye upendo na viongozi wao, bali nauliza tuu is this fair?.

Kwa hili la misafara ya viongozi ya kupotezeana muda, namshauri Afande IGP, Kamanda Sirro, amchukue Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akafanye ziara ya kimafunzo nchini Sweden aone misafara ya viongozi wa wenzetu wanaojali muda, wanafanya nini?.

Kule Sweden hakuna kusimamishwa kwa kupotezeana muda, hata ukija ugeni wa rais, magari yanasimamishwa for less than 3 minutes. Misafara ya wenzetu inatumia precise timings kwa kutumia GPS, msafara ukifika Bagamoyo, wanaona time calculations msafara utafika Mbezi saa ngapi, then kabla ya just 5 minutes before ndipo barabara zinafungwa. Hizo GPS kwenye hizo SUV zenu za nini?.

Misafara ya wenzetu kwa long trips kama Dar -Bagamoyo, kunakuwa na pikipiki 5 kwenye msafara, piki piki moja mbele, pikipiki 2 kulia na mbili kushoto. Zile pikipiki zinakwenda fasta kuziba barabara ya mbele just two minutes kabla msafara haujapita, msafara ukiishapita, zile mbili nyingine zinatangulia mbele kwa interchangeable paces. Yale mapikipiki makubwa ya polisi wa wenzetu kwenye misafara ya viongozi sio ya kurembeshea tuu msafara, bali pia kutumika kufunga njia na kufunga, sisi kutokana na umasikini, just imagine the labour cost ya kutandaza traffic barabara nzima toka Bagamoyo hadi Dar, tunatumia Traffic wangapi?!. Japo ukubwa raha, wengine wote wanasimamishwa mkubwa apite, lakini kusimamishwa huku kusiwe kero kwa wengine. Tena wajemeni hii misafara ya wakubwa pia ni mateso kwa Traffic wetu japo ndio wameajiriwa kwa kazi hiyo, sidhani kama ni matumizi mazuri ya askari wetu kutandazwa njia nzima Dar-Bagamoyo kwa kazi ya kusimamisha magari nusu saa nzima kabla mkubwa hajapita,
Tukiufuata utaratibu kama huu wa Sweden, we can save a lot of time and put our askaris to a better use.

Tena huku Sweden, wako cost conscious, misafara ya viongozi wanapotembelea regions za mbali wanatumia special trums, huna haja ya kutumia msafara wa magari 20!. Trums 3 tuu zinatosha!.

Maendeleo ya kweli ni pamoja na kuwa na developmental attitudes kwenye kila kitu, tufanye kama wenzetu walioendelea, sio tunahumbiri tuu maendeleo ya kisasa na mbinu za mwaka 1947.

Alhamisi Njema.
Paskali
Kweli muda mwingine ni kero...lakini kwa hili viongozi wetu wa mikoani wa kisiasa wakishirikiana na wa kitaifa ndo wametufanya wananchi kuwa hivi ...unakuta kero za kutatuliwa na level ya ngazi ya chini hadi isubiri msafara wa Rais ...halafu wanaanza kuhamasisha WATU Rais atapita wananchi mjitokeze kumlaki ilihali msafara huo unaenda mkoa Mwingine tofauti na aliposimama kwangu kiongozi kama Rais akienda mkoa kama wa Mwanza akitoa Dodoma haina haja ya kusimama simama mikoa ambayo hana ratiba ya kiziara pale, kama anapita barabani bora apitilize na apange ratiba ya kufika eneo hilo lenye tatizo siku nyingine ..

Kupangana barabara ni utumwa pia ..dunia ya sasa tunaheshimu sana muda (time values) muda ni rasimali ambayo ni haiguswi..
Tujitafakari Rais akipita ahakikishiwe usalama wake lakini pia ahakikishe wengine wanapata haki zao ...yaliyotokea barabara ya MWANZA akiwa Kahama inatia hasira, Rais yupo Kahama gari zinasimamishiwa Singida...takriban masaa 5 haijalishi mpo sehemu ya por wala wapi, haijalishi hali za watu kama ni wagonjwa ,wajawazito watoto wazee...
Jeshi la polisi na vyombo vingine vya kiitelejensia tafuteni mbinu mbadala ya kutatua kero hii .
 
Nilikuwa mdogo, shule ya msingi. Tulikuwa tukimsubiri Nyerere apite toka Mwanza kwenda Musoma tangu saa 4 asubuhi mpaka saa 10. Akipita nilichokuwa nakiona ni mkono akitupungia, gari mbili mbele, yake kati na mbili nyuma. Hapakuwa na pikipiki, nahisi kwa umbali wa mwendo. Msururu wa magari leo ni utukufu wa viongozi miungu watu, wanao simama barabarani kuongea na watu waliopangwa na wachumia tumbo, barabara zikiwa zimefungwa.
 
Mbwa za kiafrika haziwezi kufanya haya. Wao ukuu ndiyo first priority kwao.
Miafrika abadani haitakuja kuwa developed kuendana na kasi za wenzetu hata ikisoma kiasi gani. Uafrika ni laana tu mi naona.
 
Uku kwetu sisi ukisikia waziri furani anakuja idara zote zinawasha magari yani anakuja waziri wa michezo unashangaa kwenye msafara yupo mkuu wa idara ya kilimo, elimu, mipango 😀😀😀 wanafunga ofisi uko siku nzima kisa kuna ugeni
 
Nilitoka tunduma saa mbili asubuhi nilikuwa nasafiri na air tz songwe to dar,nilifika songwe airport saa tatu na nusu tayari kuanza hatua za ukaguzi ili tuingie kwenye ndege,basi nakaribia kuingia lounge ikaja taarifa kuwa ndege tunayotarajia kutumia ndio mh anatarajia kutoka nayo Malawi basi tumekaa pale songwe huku naona hotuba yake Malawi live tbc,amekujakuingia mbeya kama sijakosea saa kumi au zaidi basi tukaanza kupanga folen ili tuingie kwenye ndege Mara ndege ikaondoka tukataarifiwa tusubiri bombadear inatoka mwanza ilipokuja ikabeba baadhi ya watu sisi tukasubiri trip ya pili ambayo nadhani ilikuwa zaidi ya saa 12,watu walichoka sana na mipango mingi ilivurugika

Maana yangu kuandika haya nikuwataka wenye mamlaka wakati mwingine kujaribu kuheshimu muda wa watu wengine mfano rais anatoka Malawi saa kumi jioni kuna haja gani yakuweka watu uwanjani toka asubuhi?kwanini tusingepewa taarifa kabla kuwa nitakuwa na mabadikiko ya muda wa safari?hili kwetu sisi linaweza lisiwe na madhara makubwa ila kumbuka pale kuna wasafiri wamataifa mbali mbali wanachukuliaje hili
 
Sidhani kama in sawa kumlaumu Mkuu wa Polisi na kumtaka kupeleka Polisi Sweden kujifunza zingatia hili labda unapotaka kulinganisha;

Sweden per capital income > 50 000 USD.
TZ yetu per capital < 2 000 USD

Sasa unawezaje kulinganisha hizo nchi mbili, Uchumi wa Sweden > 500 Billions USD idadi ya watu 10 million vs TZ yetu ukubwa wa uchumi < 80 Billions Idadi ya watu > 45 million.

Hivyo majibu yote yako hapo na hakuna kitu IGP atafanya usifikiri hawajui cha kufanya, wanajua ila wana limitations wakati huo huo ni jukumu lao pia kuhakikisha Usalama wa Viongozi, wanaweza hata wakawasafirisha kwa helikopta lkn who pays? Unaongelea nchi ambayo hata magari ya Polisi tunapewa msaada na hata kuweka mafuta tu wakati mwingine ni ishu, ...
Visingizio
 
Kila nchi inalinda Viongozi wake asikudanganye mtu hata huko Sweden sema hauoni kwa sababu wana options nyingi, wana pesa ya kuweza kufanya mengi.
Wana public transportation imara unaweza kupanda treni, subways, tramway system, n.k.

Bajeti ya Jeshi la Polisi peke yake huenda ikawa sawa na Bajeti ya JMTZ ya kuhudumua > milioni 45, isitoshe ni jukumu lao kuhakikisha Viongozi wa nchi wako salama sasa huo Usalama unafanikishwa vipi inategemeana na rasilimali zilizopo.
Another stupid excuse
 
Hii ni kero sana kuwasubirisha watu zaidi ya masaa matano. Wangejiwekea standard ya walau dk 15. Kwa jinsi ulivyosema hapo mbona inawezekana kabisa sio teknolojia kubwa sana ni ya kawaida tu. Tunaweza kusimamisha magari kwa muda usiozidi dk 15 kiongozi akawa ameshapita watu wakaendelea na shughuli zao.

Alafu kibaya zaidi siku hizi kila kiongozi ana motorcade yaani mpaka naibu waziri anasimamishiwa magari hii ni hatari sana kwa maendeleo yetu. Muda ni mali jamani.
 
Wanabodi,

Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"
Ukiondoa thamani ya uhai, hakuna kitu kingine duniani chenye thamani kama muda, time is money, kupotezeana muda ni kuzorotesha maendeleo.

Niko njia ya Bagamoyo eneo la Mbezi Tangi Bovu, tumesimamishwa karibu dakika 30 kupisha msafara wa Kiongozi fulani anatokea njia ya Bagamoyo.

Huku kusimamishana babarani nusu saa nzima, kisa anapita kiongozi, ilikuwa ni zile enzi za ujima, kwenye dunia ya sasa ya the age of information science, unamsimamisha mtu dakika 30 kupisha msafara wa kiongozi ni kupotezaana muda. Wengine kazi zetu zina very tight deadlines, kama zilivyo tender deadlines, umechelewa hata dakika moja, imekula kwako.

Ndio maana sisi tunawasisitiza viongozi wetu, wasiopenda kusafiri nchi za watu kwa lengo la kubana matumizi, mara moja moja wasafiri tuu kwenda nchi za Ulaya na Amerika, sio kwa ajili ya kwenda kuponda raha, au kubembea hewani kwa kukwea pipa bali kusafiri ili kwenda kupata tuu exposure, wenzetu wakoje na wanafanyaje mambo yao.

Msafara wa magari zaidi ya 15, ulipopita, umepita kwa mwendokasi wa speed 150 kph, na umbali wa Bagamoyo Mbezi Beach, ni appx 50km, hivyo kwa mwendokasi huo, msafara unatumia just 20 minutes, hivyo akina sisi tumesimamishwa huku majiani, kabla hata msafara haujafika Bagamoyo!.

Nimeelezwa kinachochelewesha misafara ya viongozi ni wananchi kujitokeza kwa wingi kufunga barabara kuzuia msafara ili wamlaki na wamsalimie na kumpa kero zao kiongozi. Ma kwa vile viongozi wetu ni watu wa watu, watu wakikusanyika kumlaki kiongozi kwenye msafara unaokwenda speed 140kph mbele una escorts 3 as advance, then kuna sweeper, halafu wananchi wanajotokezea tuu kuusimamisha msafara ili wamlaki na wamsalimie kiongozi, na kweli msafara at 140kpm unasimama ghafla kiongozi asalimiwe, huku sisi tukisubirishwa!. Siulizi if its true true msafara unasimamishwa ghafla na wananchi wenye upendo na viongozi wao ili wamlaki, bali nauliza tuu is this fair?.

Kwa hili la misafara ya viongozi ya kupotezeana muda, namshauri Afande IGP, Kamanda Sirro, amchukue Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akafanye ziara ya kimafunzo nchini Sweden aone misafara ya viongozi wa wenzetu wanaojali muda, wanafanya nini?.

Kule Sweden hakuna kusimamishwa kwa kupotezeana muda, hata ukija ugeni wa rais, magari yanasimamishwa for less than 3 minutes. Misafara ya wenzetu inatumia precise timings kwa kutumia GPS, msafara ukifika Bagamoyo, wanaona time calculations msafara utafika Mbezi saa ngapi, then kabla ya just 5 minutes before ndipo barabara zinafungwa. Hizo GPS kwenye hizo SUV zenu za nini?.

Misafara ya wenzetu kwa long trips kama Dar -Bagamoyo, kunakuwa na pikipiki 5 kwenye msafara, piki piki moja mbele, pikipiki 2 kulia na mbili kushoto. Zile pikipiki zinakwenda fasta kuziba barabara ya mbele just two minutes kabla msafara haujapita, msafara ukiishapita, zile mbili nyingine zinatangulia mbele kwa interchangeable paces. Yale mapikipiki makubwa ya polisi wa wenzetu kwenye misafara ya viongozi sio ya kurembeshea tuu msafara, bali pia kutumika kufunga njia na kufunga, sisi kutokana na umasikini, just imagine the labour cost ya kutandaza traffic barabara nzima toka Bagamoyo hadi Dar, tunatumia Traffic wangapi?!. Japo ukubwa raha, wengine wote wanasimamishwa mkubwa apite, lakini kusimamishwa huku kusiwe kero kwa wengine. Tena wajemeni hii misafara ya wakubwa pia ni mateso kwa Traffic wetu japo ndio wameajiriwa kwa kazi hiyo, sidhani kama ni matumizi mazuri ya askari wetu kutandazwa njia nzima Dar-Bagamoyo kwa kazi ya kusimamisha magari nusu saa nzima kabla mkubwa hajapita,
Tukiufuata utaratibu kama huu wa Sweden, we can save a lot of time and put our askaris to a better use.

Tena huku Sweden, wako cost conscious, misafara ya viongozi wanapotembelea regions za mbali wanatumia special trums, huna haja ya kutumia msafara wa magari 20!. Trums 3 tuu zinatosha!.

Maendeleo ya kweli ni pamoja na kuwa na developmental attitudes kwenye kila kitu, tufanye kama wenzetu walioendelea, sio tunahumbiri tuu maendeleo ya kisasa na mbinu za mwaka 1947.

Alhamisi Njema.
Paskali
Ndugu Mayalla ungekuwa kweli uko objective na mwandishi ambaye yuko impartial ungekuwa pia unaandika kukemea kauli na matendo yanayotoka upande wa watawala. Unatumia taaluma yako kwa maslahi yako binafsi. Katika mazingira ya sasa kukaa kimya ni bora zaidi kuliko na utaonekana impartial kuliko kuendelea kutoaka maandiko ambayo biased huku ukitengeneza njia ya malengo yako binafsi. Uwe na siki njema.
Mdomo Mwepesi, karibu, shuhudia jinsi ninavyosifu
P.
 
Wanabodi,

Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"
Ukiondoa thamani ya uhai, hakuna kitu kingine duniani chenye thamani kama muda, time is money, kupotezeana muda ni kuzorotesha maendeleo.

Niko njia ya Bagamoyo eneo la Mbezi Tangi Bovu, tumesimamishwa karibu dakika 30 kupisha msafara wa Kiongozi fulani anatokea njia ya Bagamoyo.

Huku kusimamishana babarani nusu saa nzima, kisa anapita kiongozi, ilikuwa ni zile enzi za ujima, kwenye dunia ya sasa ya the age of information science, unamsimamisha mtu dakika 30 kupisha msafara wa kiongozi ni kupotezaana muda. Wengine kazi zetu zina very tight deadlines, kama zilivyo tender deadlines, umechelewa hata dakika moja, imekula kwako.

Ndio maana sisi tunawasisitiza viongozi wetu, wasiopenda kusafiri nchi za watu kwa lengo la kubana matumizi, mara moja moja wasafiri tuu kwenda nchi za Ulaya na Amerika, sio kwa ajili ya kwenda kuponda raha, au kubembea hewani kwa kukwea pipa bali kusafiri ili kwenda kupata tuu exposure, wenzetu wakoje na wanafanyaje mambo yao.

Msafara wa magari zaidi ya 15, ulipopita, umepita kwa mwendokasi wa speed 150 kph, na umbali wa Bagamoyo Mbezi Beach, ni appx 50km, hivyo kwa mwendokasi huo, msafara unatumia just 20 minutes, hivyo akina sisi tumesimamishwa huku majiani, kabla hata msafara haujafika Bagamoyo!.

Nimeelezwa kinachochelewesha misafara ya viongozi ni wananchi kujitokeza kwa wingi kufunga barabara kuzuia msafara ili wamlaki na wamsalimie na kumpa kero zao kiongozi. Ma kwa vile viongozi wetu ni watu wa watu, watu wakikusanyika kumlaki kiongozi kwenye msafara unaokwenda speed 140kph mbele una escorts 3 as advance, then kuna sweeper, halafu wananchi wanajotokezea tuu kuusimamisha msafara ili wamlaki na wamsalimie kiongozi, na kweli msafara at 140kpm unasimama ghafla kiongozi asalimiwe, huku sisi tukisubirishwa!. Siulizi if its true true msafara unasimamishwa ghafla na wananchi wenye upendo na viongozi wao ili wamlaki, bali nauliza tuu is this fair?.

Kwa hili la misafara ya viongozi ya kupotezeana muda, namshauri Afande IGP, Kamanda Sirro, amchukue Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akafanye ziara ya kimafunzo nchini Sweden aone misafara ya viongozi wa wenzetu wanaojali muda, wanafanya nini?.

Kule Sweden hakuna kusimamishwa kwa kupotezeana muda, hata ukija ugeni wa rais, magari yanasimamishwa for less than 3 minutes. Misafara ya wenzetu inatumia precise timings kwa kutumia GPS, msafara ukifika Bagamoyo, wanaona time calculations msafara utafika Mbezi saa ngapi, then kabla ya just 5 minutes before ndipo barabara zinafungwa. Hizo GPS kwenye hizo SUV zenu za nini?.

Misafara ya wenzetu kwa long trips kama Dar -Bagamoyo, kunakuwa na pikipiki 5 kwenye msafara, piki piki moja mbele, pikipiki 2 kulia na mbili kushoto. Zile pikipiki zinakwenda fasta kuziba barabara ya mbele just two minutes kabla msafara haujapita, msafara ukiishapita, zile mbili nyingine zinatangulia mbele kwa interchangeable paces. Yale mapikipiki makubwa ya polisi wa wenzetu kwenye misafara ya viongozi sio ya kurembeshea tuu msafara, bali pia kutumika kufunga njia na kufunga, sisi kutokana na umasikini, just imagine the labour cost ya kutandaza traffic barabara nzima toka Bagamoyo hadi Dar, tunatumia Traffic wangapi?!. Japo ukubwa raha, wengine wote wanasimamishwa mkubwa apite, lakini kusimamishwa huku kusiwe kero kwa wengine. Tena wajemeni hii misafara ya wakubwa pia ni mateso kwa Traffic wetu japo ndio wameajiriwa kwa kazi hiyo, sidhani kama ni matumizi mazuri ya askari wetu kutandazwa njia nzima Dar-Bagamoyo kwa kazi ya kusimamisha magari nusu saa nzima kabla mkubwa hajapita,
Tukiufuata utaratibu kama huu wa Sweden, we can save a lot of time and put our askaris to a better use.

Tena huku Sweden, wako cost conscious, misafara ya viongozi wanapotembelea regions za mbali wanatumia special trums, huna haja ya kutumia msafara wa magari 20!. Trums 3 tuu zinatosha!.

Maendeleo ya kweli ni pamoja na kuwa na developmental attitudes kwenye kila kitu, tufanye kama wenzetu walioendelea, sio tunahumbiri tuu maendeleo ya kisasa na mbinu za mwaka 1947.

Alhamisi Njema.
Paskali
Inchi hii ya visasi na vinyongo hilo litaleta balaa,na msingi mama wa haya yote ni kupuuzwa kwa demokrasi hivyo kusababisha viongozi kujiona hawapo kihalali hivyo kuhitaji ulinzi mkali kila wakati.(
 
Huyu Bwana Pascal Mayalla ni Janga kweli, bado anaamini kuwa Rais atamfikiria
Jamii ya Kujipendekeza na Kusifu tu! Hovyo kabisa.
Hapa ni juzi tuu nasifu msafara wa kiongozi fulani ili niteuliwe.
P
 
Back
Top Bottom