Misanya Bingi sasa ni Daktari wa Falsafa (PhD)

Misanya Bingi sasa ni Daktari wa Falsafa (PhD)

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Wapi alipo Misanya Bingi?

Alikuwa kati ya watangazaji mahiri ndani ya ITV na Redio One na aliongoza vipindi mbali mbali ikiwemo Kipusa akirithi mikoba ya Abdallah Majura.

Ningependa kujua alipo huyu gwiji wa tasnia ya habari mwishoni mwa miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000.
===========

Misanya.jpg

Mtangazaji Mkongwe wa Radio nchini, DR. Misanya Bingi.

Aliyepata kuwa mtangazaji mahiri wa ITV ambaye sasa ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam jana alitunukiwa cheti chake cha PhD na sasa anajulikana kama Dkt Misanya Bingi.

JamiiForums inakupongeza kwa hatua hiyo na kukuombea wepesi huko kwenye uprofesa unakoelekea, hasa baada ya kutetea vyema andiko lako la "Female Circumcision" kwenye thesis yako.

Ni matumaini yetu wanafunzi wako wote hapo Sociology Dept. wanafurahi.

Hongera mwayego...... When one door is closed many others are open..
 
Hongera zake nakumbuka nilikua sikosi kipindi chake cha chemsha bongo, kilikuwa kina bamba sana
 
Huyu bwana amenitia nguvu sana ya kupambana na elimu kweli hakuna kisichowezekana...chini..ya jua...I believe that one day I will have a pHD....also

Mbona umechelewa sana? Mimi siku niliyomuona Mrema akipita na farasi na matarumbeta City center Dar kuonesha degree yake basi tangu siku ile niliamini i can be anything i want.
 
Mbona umechelewa sana? Mimi siku niliyomuona Mrema akipita na farasi na matarumbeta City center Dar kuonesha degree yake basi tangu siku ile niliamini i can be anything i want.

Hahaaaaaa
Watu mna maneno llloooh!!
 
Nilimsikia kwenye wimbo wa Fid Q
Hongera
 
Nataman hata yule "profeseri" wa kichina nae angepitia shule kama huyu!!!! Safi sana Dr. Misanya umetendea haki elimu!!
 
Iila Misanya bhana akitangaza sauti yake ilikuwa ya kipekee, sijui lafudhi ya wapi
 
Back
Top Bottom