Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo hii wakati mwingine huwa inaliwaza sana. Siku moja bosi wangu aliniudhi kiasi cha kutamani kumchinja. Nilipofika maeneo ya Mazense, ilipita coasta mbele yangu imeandikwa "Msamehe aliyekuudhi, ni shetani kamtuma ili ugongeshe gari lako" Nilifarijika na kuanza kuwa makini nisije goga magari ya watu.
 
Ntakusema kwa Baba
Siri yako
Waheshimu Wakongwe
Usimwambie Mtu
Watachonga sana
Panda Ukazibe
Tenga halibebi Maji
Utakula Jeuri yako
Mjini Shule
Monica Lewinsky
Ngoma ya Watoto Haikeshi
Mume wa Mama Yako ni Baba Yako
Wowowo
Vuuuuuuu!
 
Aidakishi
Posho kwa mbinde
Kwasababu kazi zinafanana ila mkubwa kwako
Mwaga mboga nimwage ugali
Mwenye dada hakoso shemeji
 
Nimekuwa napenda sana kusoma misemo mbali mbali katika magari hasa mabasi ya abiria na yale ya mizigo.
Ndipo nilipoamua kuwauliza madereva, nani anayetaka maneno hayo yaandikwe? Majibu yao ni kuwa, wapo matajiri wanataka semi hizo ziandikwe, wakati mwingine ni madereva wenyewe huwa ndiyo wanaandika. Ila semi wanazoandika madereva ni zile zinazokuwa katika bomba au ngao (nyuma chini).

Semi hizi zinabea maana kubwa sana ikiwa ni zaidi ya kufurahisha kwa wakati wake. Mfano,
Ukicheka na nyani utakula mabua.
Hata ukioga, mjini huendi.
Ulifikiri kumwambia baba yako HALLO kwenye simu ndiyo heshima?
Akikua ataacha!
Hata kwetu wapo.
Wanga sasa basi, ukimwi unatosha.
Mimba mnatoa, Ukimwi je ?
Jino moja mswaki wa nini?
Swali kabla hujaswaliwa.
Dume kwenye mfuko wa nyuma?
Usivue viatu kuna mbigiri.
Changanya na zako!!!
Unga robo, usicheze mbali.
Butua uwakomboe wenzako.
Si ulisema tamu, unalia nini?

Naomba utushirikishe semi ulizowahi au unazozisoma toka katika magari hayo.

Mbuzi ni mbuzi,ubeberu ni cheo tuuu,
tonge halichagui mboga
njia ya chooni haioti majani
Hatutaki siasa za kale, siku hizi tuna wahi kubalehe
kusoma kuelewa,kukesha mbwembwe
 
Back
Top Bottom