Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 180
...Mchawi mpe mtoto akulelee....!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimekuwa napenda sana kusoma misemo mbali mbali katika magari hasa mabasi ya abiria na yale ya mizigo.
Ndipo nilipoamua kuwauliza madereva, nani anayetaka maneno hayo yaandikwe? Majibu yao ni kuwa, wapo matajiri wanataka semi hizo ziandikwe, wakati mwingine ni madereva wenyewe huwa ndiyo wanaandika. Ila semi wanazoandika madereva ni zile zinazokuwa katika bomba au ngao (nyuma chini).
Semi hizi zinabea maana kubwa sana ikiwa ni zaidi ya kufurahisha kwa wakati wake. Mfano,
Ukicheka na nyani utakula mabua.
Hata ukioga, mjini huendi.
Ulifikiri kumwambia baba yako HALLO kwenye simu ndiyo heshima?
Akikua ataacha!
Hata kwetu wapo.
Wanga sasa basi, ukimwi unatosha.
Mimba mnatoa, Ukimwi je ?
Jino moja mswaki wa nini?
Swali kabla hujaswaliwa.
Dume kwenye mfuko wa nyuma?
Usivue viatu kuna mbigiri.
Changanya na zako!!!
Unga robo, usicheze mbali.
Butua uwakomboe wenzako.
Si ulisema tamu, unalia nini?
Naomba utushirikishe semi ulizowahi au unazozisoma toka katika magari hayo.
Ahahahaaaaaaah hapo kwenye ARSENAL wangeweka MAN U.Kushinda washinde CHELSEA wakishinda ARSENAL refa kahongwa!
Kushinda washinde CHELSEA wakishinda ARSENAL refa kahongwa!
Nimeona leo kwenye daladala. Eti POPOTE ULAYA. TATIZO HELA