Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Ukijamba kwa hasira utajinyea.
Ukikilazimisha kukohoa utatapika.
Mficha uchi hazai.
Ole wake afuataye nyayo za simba
mchamba wima hatakati.
Nipe sumu yangu ninywe nikafie mbele
mkulu kumwao
kiatu cha kushoto hakivaliwi kulia
 
silaha pesa kisu hatari,uzuri wa nyumba choo,choo chenyewe kicjae,dege la jeshi ktuo popote,stahamili japo unaumia,utamu wa pipi ni mate yako mwenyewe
 
Nimekuwa napenda sana kusoma misemo mbali mbali katika magari hasa mabasi ya abiria na yale ya mizigo.
Ndipo nilipoamua kuwauliza madereva, nani anayetaka maneno hayo yaandikwe? Majibu yao ni kuwa, wapo matajiri wanataka semi hizo ziandikwe, wakati mwingine ni madereva wenyewe huwa ndiyo wanaandika. Ila semi wanazoandika madereva ni zile zinazokuwa katika bomba au ngao (nyuma chini).

Semi hizi zinabea maana kubwa sana ikiwa ni zaidi ya kufurahisha kwa wakati wake. Mfano,
Ukicheka na nyani utakula mabua.
Hata ukioga, mjini huendi.
Ulifikiri kumwambia baba yako HALLO kwenye simu ndiyo heshima?
Akikua ataacha!
Hata kwetu wapo.
Wanga sasa basi, ukimwi unatosha.
Mimba mnatoa, Ukimwi je ?
Jino moja mswaki wa nini?
Swali kabla hujaswaliwa.
Dume kwenye mfuko wa nyuma?
Usivue viatu kuna mbigiri.
Changanya na zako!!!
Unga robo, usicheze mbali.
Butua uwakomboe wenzako.
Si ulisema tamu, unalia nini?

Naomba utushirikishe semi ulizowahi au unazozisoma toka katika magari hayo.


Ukimuna mbwa juu ya mti, jua amewekwa!
 
1. Supprise is better than promise!!
2. Usiulize imetoka wapi!
3. Raha ya kucheka uwe na meno
4. Raha ya dafu ukatiwe kisha uchokonolewe!
 
Yatima hachagui mlezi!!
Gunia tupu halisimami!!
 
1. chuki zenu ni neema kwangu
2. haina fagio
3. 1+1=5
4. mkulu halongwa
 
1.Haiumizi ndo umbile lake
2.usichezee kazi chezea mshahara
3.Nyuki hakumbatiwi
4.Ubaya wa kazi ukiwa nayo
5.Hata ukibanwa nauli utalipa
 
wakati fulani nilikuwa tabora nikaliona basi moja linatoka urambo limeandikwa "shahidi vumbi"
 
Waendesha boda boda nao wanavituko cheki nimeiona wiki hii " KULA KIPANDE, UONE MCHARUKO WA BOSI"
 
Back
Top Bottom