Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
miss Manyara
...elimu kwanza
....utaisoma
....how am I driving?
...if you can read this you are too close
...wide load/vrag cargo
...asha ngedere
...Joni Sinna
...mwanamalundi
...twanga kotekote
...dege la jeshi
...ikiuma sema
...cheza na mke wangu usicheze na kazi yangu.
...mke nitakuazima,gari sitakuazima
...chaja ya kobe
...ya karim
...umebipu? Sasa unapigiwa.
...mteja ni ****
...imetoka hiyo..ikirudi pancha.
...punguza shida
...waweja kulumba
...kumbe chipsi ni viazi...
...usikanyage hapa
...a.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.k.a
...wrong number
...pesa mbele kama mimba.
...hiloooooooo! Nimelipita
Hii nimeipenda "Msafara wa simba hauitaji escort"Usiogope haiumiz ni umbile lake,talaka ya hawara makonde,kama weupe ni mali ubuyu usingepakwa rangi,
Nimekuwa napenda sana kusoma misemo mbali mbali katika magari hasa mabasi ya abiria na yale ya mizigo.
Ndipo nilipoamua kuwauliza madereva, nani anayetaka maneno hayo yaandikwe? Majibu yao ni kuwa, wapo matajiri wanataka semi hizo ziandikwe, wakati mwingine ni madereva wenyewe huwa ndiyo wanaandika. Ila semi wanazoandika madereva ni zile zinazokuwa katika bomba au ngao (nyuma chini).
Semi hizi zinabea maana kubwa sana ikiwa ni zaidi ya kufurahisha kwa wakati wake. Mfano,
Ukicheka na nyani utakula mabua.
Hata ukioga, mjini huendi.
Ulifikiri kumwambia baba yako HALLO kwenye simu ndiyo heshima?
Akikua ataacha!
Hata kwetu wapo.
Wanga sasa basi, ukimwi unatosha.
Mimba mnatoa, Ukimwi je ?
Jino moja mswaki wa nini?
Swali kabla hujaswaliwa.
Dume kwenye mfuko wa nyuma?
Usivue viatu kuna mbigiri.
Changanya na zako!!!
Unga robo, usicheze mbali.
Butua uwakomboe wenzako.
Si ulisema tamu, unalia nini?
Samaki mkubwa usiogope kuuliza bei
Naomba utushirikishe semi ulizowahi au unazozisoma toka katika magari hayo.
Chezea Mshahara... Usichezee Kazi..!Utamu wa kazi, pesa..!
Si uliingia mwenyewe, uwii ya nini?
Tatizo pesa.
Una beep....Ntakupigia!!
Salio dogo.
Panda juu kazibe.
Usizame chubwiii
Kamba fupi
Yeboyebo haimalizi mwaka
Mmmh! nani kasema sitaki?
Hata paka mzee hutamani maziwa.
Shemeji ananitega
Usinichumm...wanaona.
Wapambe nuksi.
Usiogope haiumiz ni umbile lake
Hii kwenye Red inaleta maana sana.imekaa vizuri...........Kamweleze, nitajieleza, ni mwelewa, atanielewa..............
..........njaa haina ubaunsa........................................................
Zafanana