34 katika mwaka wa pilii wa utawala wa mfalme Juma Nguvu Hovyo wa tano, mfalme wa nchi ya sambaratika, bandari ilikuwa tupu. hakuna mizigo iliyoingia kupitia bandari hii. mfalme na matowashi wale walikuwa katika mfadhaiko mkuu wasijue la kufanya.
35 lakini asubuhi moja katika mwezi wa sita, mlinzi wa lango kuu la bandari aliona vichwa vya treni vikiwa bandarini. moyo wake ukashikwa na hofu kuu. akageuka na kwenda kuwaambia matowashi alichokiona. nao kwa hamaki wakanyanyuka kwenda kuyaona. wakaulizana wao kwa wao "ni nani kati yetu amefanya haya?" hakuna hata mmoja kati yao aliyejua chochote.
36 habari zikamfikia mfalme nguvu hovyo, naye akafika bandarini na kuwakuta matowashi wakiwa wamekusanyika kwa fadhaa. akaviangalia vichwa vile, kisha akawageukia matowashi na kuwauliza "ni nani kati yenu amefanya haya kunijaribu mimi nisiyejaribiwa?". nao wakamjibu "ee bwana usiyejaribiwa, kama wewe uishivyo, hata sisi hatujui"
37 akavigeukia tena vichwa vile vya treni, akaviuliza "enyi mliotoka kusikojulikana, ni nani amewatuma kwangu kuja kunijaribu mimi na watu wangu, watu waliochini ya uvuli wa minyororo yangu?". kichwa kimoja kikafungua kinya chake na kunena "ewe mfalme nguvu hovyo, huoni kuwa bandari yako ilivyo tupu?, huoni watu wako walivyo na fadhaa? je, ni vibaya sisi kuja kurudisha matumaini ya watu yaliyopotea tangu ukalie kiti hicho cha enzi?"
38 maneno yale yalimfadhaisha sana mfalme, akageuka na kurudi kwenye jumba lake jeupe akiwa na gadhabu ya kiwango cha standard gauge akiwaacha matowashi na walinzi wasijue la kufanya.
MENDE MSAFI 24: 34-37