Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

Ndo akafungua kinywa na kunena 'kwa vile umesema wazee tuachwe tupumzike na wala tusihusishwe na mikataba mibovu ya wakati wetu, mkuu wa majeshi, basi ikikupendeza utawale milele' : Kulindana 20:17
Mmmmh
 
Basi mfalme alipoona wadanganyika wamefurahi na kupendezwa baada ya kumweka rumande Ruge na Seth, akamwendea mwenyekiti wa TifuaTifua na Katibu wake nao akawaweka ndani. Hata yule Kanjibhai naye hakuweza kupona mbele ya mkono wenye nguvu wa mfalme Sizonje.
I wish I could be IGP 34: 3-6
Yule nabii mdogo akaonya "msitaje majina katika mahubiri yenu maana yule mwovu atawatia taabuni kwa kutumia nguvu zake na sheria zake za kiuonevu!
Mitandao 20:15
 
Basi nao wafuasi wake wakaanza kumkejeli na kumdhihaki na kutomuelewa nini anachofanya, lkn hakukata tamaa na alisonga mbele kwani alijua yeye aliletwa na bwana kwa ajili ya wanyonge. Viwanda 2:20-20
 
34 katika mwaka wa pilii wa utawala wa mfalme Juma Nguvu Hovyo wa tano, mfalme wa nchi ya sambaratika, bandari ilikuwa tupu. hakuna mizigo iliyoingia kupitia bandari hii. mfalme na matowashi wale walikuwa katika mfadhaiko mkuu wasijue la kufanya.

35 lakini asubuhi moja katika mwezi wa sita, mlinzi wa lango kuu la bandari aliona vichwa vya treni vikiwa bandarini. moyo wake ukashikwa na hofu kuu. akageuka na kwenda kuwaambia matowashi alichokiona. nao kwa hamaki wakanyanyuka kwenda kuyaona. wakaulizana wao kwa wao "ni nani kati yetu amefanya haya?" hakuna hata mmoja kati yao aliyejua chochote.

36 habari zikamfikia mfalme nguvu hovyo, naye akafika bandarini na kuwakuta matowashi wakiwa wamekusanyika kwa fadhaa. akaviangalia vichwa vile, kisha akawageukia matowashi na kuwauliza "ni nani kati yenu amefanya haya kunijaribu mimi nisiyejaribiwa?". nao wakamjibu "ee bwana usiyejaribiwa, kama wewe uishivyo, hata sisi hatujui"

37 akavigeukia tena vichwa vile vya treni, akaviuliza "enyi mliotoka kusikojulikana, ni nani amewatuma kwangu kuja kunijaribu mimi na watu wangu, watu waliochini ya uvuli wa minyororo yangu?". kichwa kimoja kikafungua kinya chake na kunena "ewe mfalme nguvu hovyo, huoni kuwa bandari yako ilivyo tupu?, huoni watu wako walivyo na fadhaa? je, ni vibaya sisi kuja kurudisha matumaini ya watu yaliyopotea tangu ukalie kiti hicho cha enzi?"

38 maneno yale yalimfadhaisha sana mfalme, akageuka na kurudi kwenye jumba lake jeupe akiwa na gadhabu ya kiwango cha standard gauge akiwaacha matowashi na walinzi wasijue la kufanya.
MENDE MSAFI 24: 34-37
 
Mimi nauliza tena? Hapa Tanganyika kuna reli za watu binafsi au? Maana suala la vichwa vyà treni kukosa wenyewe duh, aisee si ndio wangefurahi kuvichukua moja kwa moja!!
 
Mimi nauliza tena? Hapa Tanganyika kuna reli za watu binafsi au? Maana suala la vichwa vyà treni kukosa wenyewe duh, aisee si ndio wangefurahi kuvichukua moja kwa moja!!
Wewe usiulize moja kwa moja wataku tcra quite kifungu cha neno la kuhani mkuu wa wadanganyika
 
Mala nikaona malaika wakipewa maelekezo enendeni kwenye jamii ya frola mkazuie mijadala isiyo nipendeza na mkatangaze ya kwamba mimi sijalibiwi na yeyote nitakaye muona amefanya kazi vizuri nitampatia kondoo sabini
Ufunuo wa twafwa 21:12
 
Ahahahahaaa nimewapenda bure wana jf sio kwa mistari hiyo
 
Kisha akawauliza mchanga huu wa makinikia ni wanani wakajibu wa acacia akawajibu basi wapeni acacia yalio yao acacia na nyie subirini noah kazi kwenu kuchagua rangi.
Kutumwaindia kutibiwa 2017:2020
 
Siku zile za sherehe ya mfalme tazama mwanaye Bashite alimpendeza sana babaye kwa kuwa kila dakika alikuwa anamsifu mfalme ndipo mfalme akamwambia Bashite sema lolote utakalo nitakupatia

Basi bashite kwa vile alichukizwa sana na mange kimambi akamwambia niletee kichwa chake kwenye rambo
Sijaribiwe 7:7
 
"Na ndipo hapo kukakucha, vichwa vile vikashangaza watu wengi, vimekujaje hapo bila kuwa na mmiliki?? Wafuasi wa kule mtoni na wanaoendesha treni wakasema hata sisi hatujui mkuu"
Joseverest andiko lako kitabu gani na mstari wa ngapi
 
Back
Top Bottom