Mishahara mikubwa waliokuwa wanalipana Nyerere na viongozi wenzake kweli ilikuwa ni sahihi

Mishahara mikubwa waliokuwa wanalipana Nyerere na viongozi wenzake kweli ilikuwa ni sahihi

Mkuu Ritz,

Huu ni mwendelezo wako na wenzako wa kujaribu kumchafua Mwalimu Nyerere (Baba wa Taifa) kwa kila namna, kwa mfano, hiyo nukuu yako juu ambayo umedokoa dokoa tu vijineno vya kukusaidia ufikishe ujumbe uliokusudia.

Naomba nikuelekeze kwenye mtazamo na msimamo mwa Mwalimu Nyerere (baba wa taifa) juu ya suala husika kwa kirefu, kwa mujibu wa TANU NA RAIA (1962); Ukisoma kwa makini, utagundua enzi za utawala wake, mambo yalikuwa wazi (transparent) tofauti na sasa ambapo hata mshahara wa waziri haujulikani na wananchi. Pia tofauti na enzi za Mwalimu, viongozi wa sasa hawana huruma kabisa na hali za wananchi walio wengi (maskini), na maneno yafuatayo ya Mwalimu yanawasuta viongozi wa sasa moja kwa moja:

["Tulipokuwa tukitawaliwa na wakoloni tuligawanywa katika makundi matatu. Wazungu walikuwa juu, wahindi walikuwa katikati na waafrika walikuwa chini, kwa hali zao za elimu, mali na vyeo. Yawezekana wachache wa kundi Fulani la chini walipata bahati ya kuwa miongoni mwa kundi la juu, lakini kwa ujumla, hivyo ndivyo tulivyokuwa.

Shabaha ya TANU na serikali ya TANU ni kuondoa makundi haya. Milango ya elimu, mali na vyeo, ambavyo jana ilikuwa imefungwa kwa waafrika leo inafunguliwa. Wazungu na wahindi ambao jana walipita katika milango hiyo kwa urahisi kwa sababu cheti cha kupita kilikuwa ni rangi tu, wanaona kwamba cheti hicho siku hizi hakitoshi kumpitisha mtu asiyestahili kupita. Mambo haya tunayatenda hivi sasa na tunaendelea kuyatenda mpaka mafungu yale tuliyorithi kwa mkoloni yawe yameondoka. Jambo ambalo hatuna budi kujiuliza ni hili:

Je, vitendo hivi vina shabaha gani?

Ni shabaha ya kuinua wanyonge wote wa jana?

Au ni shabaha ya kuwatia waafrika wachache katika nafasi za wazungu na wahindi?

Shabaha yetu ni kuondoa makundi kati ya raia au ni kuunda makundi mapya?

Tutakuwa na kundi la waafrika ambao hawajambo katika mali, elimu na vyeo, na kundi la waafrika ambao ni taabani katika mambo yote hayo.

Tuchukue mfano wa mishahara. Wakoloni walipokuwa hapa walipanga mishahara bila kujali uwezo wa watu wetu kuilipia mishahara hiyo, na bila kuilinganisha mishahara hiyo na mapato ya watu wetu. Lakini wao ilikuwa ni ada yao kufanya hivyo. Serikali ya wageni haiwezi kujali maisha ya raia. Serikali yao ilikuwa ni serikali ya ubwana na ufahari; na walijitimizia ubwana wao na fahari yao, bila kujali uwezo wa watu wetu wa kugharamia ubwana huo na fahari hiyo.

Lakini baadhi yetu tulikuwa hatutambui jambo hilo. Waafrika wengi tulikuwa tumekwisha kusahau kwamba mzigo ule wa ubwana na ufahari ni mzito mno kna watu wetu hawawezi kuubeba. Kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana ule na fahari ile wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia na sisi pia. Baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na fahari, bali tama yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari.Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo hivyo bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, na bila kujali maisha ya watu wetu.

Tulipopunguza mishahara ya Mawaziri, tulisifiwa kwamba tumefanya jambo zuri.
Ni kweli kwamba tulifanya jambo zuri. Mshahara wa waziri wa kikoloni ulikuwa ni zaidi ya Shs. 5,000/- kwa mwezi, Juu ya hiyo kulikuwa na matumizi mengine ya kikazi ambayo hata sisi hatukuondoa. Sisi tulipunguza mshahara huo na kuufanya Shs. 3,000/- kwa mwezi kwa kila waziri pamoja na waziri mkuu pia. Mshahara huu ukiulinganisha na mishahara wanayopata mawaziri katika sehemu nyingine za afrika, au dunia ni mshahara mdogo sana. Lakini kulinganisha mishahara ya mawaziri wetu na mishahara ya mawaziri wa nchi nyingine, ambayo yaweza ikawa tajiri zaidi kuliko Tanganyika, siyo njia safi ya kulinganisha. Njia inayofaa kutumiwa, njia ambayo wana – TANU na wananchi wote hatuna budi tuitumie, ni kulinganisha mshahara huo na pato la ndugu zetu.

Nitajaribu kuwaonyesha na sina shaka natumaini mtastuka. Pato la nchi yetu kama tukiligawa kwa kila mtu sawa sawa, basi kila raia wa Tanganyika atapata Shs.400/- kwa mwaka. Tuseme nyumba ina watu wane – yaani mke, mama na watoto wawili. Basi pato lao lingekuwa Shs. 400/- mara 4 kwa mwaka; yani Shs 1,600/-. Pato hilo ni kiasi cha Shs 133/- kwa mwezi.

Lakini tunalifikiaje pato hili? Tunalifikia pato hili kwa kuchanganya pato la taifa la Tanganyika nzima, na kuligawa sawa sawa. Ukweli wenyewe ni kwamba pato hili la Shs.133/- kwa mwezi ni pato la karatasi tu. Watu wetu hawalipati. Tulipoingia serikalini tulikuta watu wengi wanapata mshahara wa Shs. 1/75 kutwa ambao ni kiasi cha Shs. 45/50 kwa siku 26 za kazi. Tuliongeza mshahara huu ukawa Shs 2/75 kwa siku, ambao ni kiasi cha Shs. 71/50 kwa siku 26 za kazi. Watumishi wa juu ya hao walikuwa wakipata kiasi cha Shs. 107/- kwa mwezi. Ni wakati wa kukubali mishahara iliyotokana na uchunguzu wa Bwana Adu ndio tulipoongeza mshahara wao ukawa Shs 132/- kwa mwezi.

Basi njia safi ya kujua kama mshahara wa Shs.300/- kwa mwezi ni mkubwa au mdogo si ile kuulinganisha na mishahara ambayo mawaziri wa nchi nyingine hupokea. Njia bora ni kulinganisha Shs. 3,000/- kwa mwezi na Shs. 71/50 au Shs. 132/- kwa mwezi. Hapana mtu anayeridhika na fedha. Kwahiyo mawaziri wetu wanazo shida kubwa, na tunazijua. Lakini shida zao ni za aina mbali kabisa na shida ya mtu ambaye anapata Shs. 71/50 kwa mwezi.

Nimewataja mawaziri kama mfano tu. Lakini maneno haya yanawahusu waafrika wote wenye hali nzuri. Leo Permanent Secretary Mwafrika mshahara wake ni Shs. 4,000/- kwa mwezi. Hatujali permanent secretary kupata mshahara mkubwa kuliko waziri wake. Sababu ni kwamba hatutaki mawaziri wetu walinganishe mishahara yao na Ma – Permanent secretary wao, na kusema ni midogo. Tunataka mawaziri wetu walinganishe mishahara yao nay a wale vibarua wanaopata Shs.71/50, na watambue kuwa ni mikubwa. Hatutaki Waziri wetu awe na tama ya kupunguza tofauti ya pengo kati ya mshahara wake wa Shs. 3,000/- kwa mwezi na mshahara wa permanent secretary wake wa Shs.4,000/- kwa mwezi. Tunataka waziri wetu awe na tamaa ya kupunguza tofauti kati ya mshahara wake wa Shs. 3,000/- kwa mwezi na ule wa kibarua wa Shs 71/50 kwa mwezi. Kadhalika mshahara wa permanent secretary mzungu ni Shs.4,800/- au zaidi. Hatutaki permanent secretary mwafrika aseme kuwa huu ni ubaguzi, na adai yeye pia apate mshahara huo. Tunamtaka afikirie njia za kusaidia kupunguza tofauti iliyopo sasa kati ya mshahara wake wa Shs. 4,000/- kila mwezi na ule wa kibarua wa Shs. 71/50 kwa mwezi. Tunataka kila mwafrika ambaye sasa hivi hali yake ni nzuri ailinganishe hali yake na wale walio wengi ambao hali yao ni mbaya."]



SOURCE: J.K NYERERE, TANU NA RAIA, UK 6-8, 1962


Mkuu Ritz, Je:

Kwa suala husika, Viongozi wa leo wa ngazi za juu wa CCM wanatosha kwa Mwalimu - kwa maneno na vitendo?

cc zomba, FaizaFoxy, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, JokaKuu, Pasco, Barubaru, Kimbunga, JingalaFalsafa, ZeMarcopolo, Kobello, chama, Zinedine, jmushi1, Sideeq, gombesugu, EMT, adolay, WildCard
 
Mkuu Mchambuzi.

Nadhani hizo zitakuwa ni fikra zako kusema kuwa namchamfua Mwalimu Nyerere, sijui ni wapi nilipo mchafua nilichokiweka ni maneno yake mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Fanya uchunguzi kisha fungua uzi tuchangie.

Kama wewe umefanya uchunguzi ungekuwa umetoa orodha ya mishahara ya marais wote wanne lakini unajishaua kwa vile mtaumbuka! Nyerere alikuwa muwazi mwambie na kikwete ataje wake ili tuchangie kwa kulinganisha!!
 
Hizo ni fikra zako wapi nimekuambia kuwa natetea mishahara wanayolipana viongozi sasa hivi.

Mimi sina uhusiano wowote na Rais Kikwete, unachofanya ni makosa Name Calling.

Huu ni mjadala huru.

nilidhani we ndo ridhwan
 
Mkuu Ritz kama ulileta uzi huu kwa kutojua maudhui kama alivyofafanua Mchambuzi mada haikuwa balanced and fair.Kuchukua mstari mmoja kunapoteza maana kabisa ya kile kilichokusudiwa.
Wiki hii nimeona nyuzi nyingine ikimlaumu Nyerere.Ni sehemu ya kampeni za kumdhalilisha kwa makusudi.

Nyerere alisema kuhusu mishahara kwa utuhubutu. Hiyo ndio legacy ya yake kuwaeleza wananchi alichokiona kina umuhimu kwao ili wakielewe.

Kusemwa kila siku kwa Nyerere ni dalili njema ana kitu cha kuzungumziwa hata kama hatukubaliani.
Katika jamvi hili kuna watu hawamjui Ngweso ni nani Afrika.
Na wapo wasiojua Mkapa,Mwinyi wamelifanyia nini taifa. Maana yake ni kuwa Nyerere ana kitu cha kuzungumziwa tofauti na diktete Ngweso au akina Mkapa na Mwinyi.

Endaopo tunadhani alilosema Nyerere ilikuwa makosa, nani anajua mshahara wa Mwinyi, Mkapa au JK?
Tumekuwa wajinga wa kusahau bunge la Spika Sitta lilipiga marufuku mishahara ya wabunge kuwekwa wazi!

Wabunge wanalipwa mshahara wa sh milioni 3. Ni mshahara mdogo sana ukilinganisha na wafanyakazi wa taasisi kama TRA na TANROAD. Haya ni mazingaombwe watu wasiyoyaona kwasababu tu wanachuki na Nyerere.

Katika mazingaombwe hayo mshahara wa mbunge wa sh milioni 3 kama ulivyoandikwa ikifika tarehe 30 ya mwezi unaumuka na kufikia milioni 11. Tukiuliza baking soda ipi imetumika jibu ni pesa za mafuta, kujikimu, makazi, mfuko wa mbunge n.k.

Mshahara wa Mbunge ni mara 33 ya kima cha chini katika hesabu za laki 3. Ukinganisha na Nyerere wa mara 20 utaona nani muungwana na nani mumiani!. Hivi wanaopata mara 33 watakuwa wamefanya nini kama si uhalifu.

Yupo kiongozi wa taasisi moja ya umma anapata milioni 25 kwa mwezi kwa kazi zile zile ambazo taasisi yingine zinashughulikia katika uzani wa majukumu.Tumefumba macho tupo bize tunamapka matope Nyerere.

Nyerere yupo katika rekodi ya kuwakatalia wabunge kujiongezea mishahara.
Kikwete yupo katika rekodi ya kuita wazee wa Dar es Salaam wakatae ongezeko la mishahara Diamond Jubilee. Baada ya mkutano Kikwete akarudi Ikulu na kusaini kile alichokikataa Diamond.
Hakuna wa kuhoji hili limefanywa na ''malaika'', tupo bize kumpaka matope'shetani' Nyerere.

Wabunge wapo katika rekodi ya kukataa mafao viongozi ambao walijipelekea mswada wa kuangalia hali za maisha yao baada ya utumishi. Wabunge wapo katika rekodi baada ya kuongezewa wakaridhia ongezeko hilo. Hawakuridhia ongezeko la mtu mwingine bali wenyewe.Tupo bize kumlaumu Nyerere na kufumbia macho wizi unaoendelea hadi dakika hii.

Wabunge si watumishi wa umma ni wawakilishi wa watu. Ni kazi ya heshima na wito.
Leo mbunge anapewa mamilioni ya kustaafu kazi ambayo si ajira bali uwakilishi.
Mafao ya milioni 45 ni pesa ya ndoto kwa mtumishi aliyefanya kazi miaka 30.
Hatuoni haya tupo katika harakati za kumchafua Nyerere kwasababu yeye ndiye tatizo.

Tumeshindwa kulipa bilioni 10 za watumishi wa EAC hadi zaidi ya nusu wamefariki.
Wizi uliobainiwa na CAG kwa mashirika, halmashari na taasisi za umma ni zaidi ya bilioni 20.
Hatuoni haya tumekaza mboni zetu kumpaka Nyerere matope ya fikra.

Mikutano miwili imegharimu biioni 2. Pesa zilizotafunwa mkutano wa teknolojia pale Mlimani city ni bilioni 8.
Kwa mkupuo mmoja wa haraka bilioni 10 zimetoka bila kujua zimeenda wapi. Uongozi wa nchi upo kamili kuanzia juu hadi chini. Yametokea JK yupo madarakani, hilo si tatizo, tatizo ni Nyerere aliyefariki maiaka 15 iliyopita

 
Last edited by a moderator:
Mkuu@nguruvi3 umechambua vyema sana,sijui kama hawa wanasiasa wetu pale jangwani kama wameligusia hili suala la mishahara ya wabunge na mawaziri kuwa siri na hata kwa rais pia,

Na kwanini wanasiasa walipwe mishahara mikubwa kuliko wataalamu kama walimu,madaktari na wengineo hii sio fair kabisa
 
Ritz Nyerere alitasfsiri vitabu vingi sana , ila hakutafsiri kitabu kiitwacho: The Animal Farm; Soma kitabu hicho cha animal farm ambacho kinasimulia jinsi mkomunisti alivyo genious kumtawala mtu mjinga dunniani. mara baada ya kusoma kitabu hicho, Usipolia machozi basi utazimia kwa uchungu.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 Tukiacha , uyanga na usimba, nyerere angefanya kitu kimoja ktk katiba ya nchi, kwa niaba ya wananchi awatwalae hapo angeoneka nabii. angeweka kifungu kisemacho Raisi ashitakiwe kwa makosa au uzembe atakaoobainika kuufanya , wakati yeye yupo madarakani.


matokeo yake kifungu kama hicho cha kuwashitaki watwala wa tanzania kila wafanyapo makosa au kuabuse power, hakiwezekani kuwekwa tena katika katiba.
 
Last edited by a moderator:
Tukijua basi pia tutafahamu Maria nyerere anachukua kiasi gani kwa mwezi (80% mshahara wa rais) kutoka katika pesa za walipa kodi wasio weza kupata milo miwili tu kwa siku.


bhana na wewe shalap, watajijua ktokula milo mitatu kwa siku shauri yao, wasubili watashiba siku ya uchaguz pia kt kampen za ccm watakapo pikiwa pilau na kuuza miaka mitano kwa mafisadi wa ccm.
tnao uku mtaani wajinga hao kibao hutukejeli kila ccm inaposhinda kt uchaguz, let them eat mlo m1 daily
 
nyerere alikuwa muwazi na kutangaza mshahara wake hadharani kwa wale walipa kodi waliokuwa ndio wanaomlipa mshahara wake. Unadhani kwanini mwinyi, mkapa na kikwete waliamua kufanya mishahara yao siri ukilinganisha na mwalimu ambaye aliutangaza mshahara wake hadharani!?
alijua fika kuwa, hata ikikuuma wala kukusikitisha , usingefanya lolote.
 
Mkuu@nguruvi3 umechambua vyema sana,sijui kama hawa wanasiasa wetu pale jangwani kama wameligusia hili suala la mishahara ya wabunge na mawaziri kuwa siri na hata kwa rais pia,

Na kwanini wanasiasa walipwe mishahara mikubwa kuliko wataalamu kama walimu,madaktari na wengineo hii sio fair kabisa
hilo jibu lipo ktk kitabu cha animal farm:
farsi anyelima na kukaza misuli, yeye huishia kusifiwa tuu, ila mbweha ambaye hupiga makelele juu ya mti, alikuwa nakula mishahara miwili miwili!!!
 
Mkuu Mchambuzi.

Nadhani hizo zitakuwa ni fikra zako kusema kuwa namchamfua Mwalimu Nyerere, sijui ni wapi nilipo mchafua nilichokiweka ni maneno yake mwenyewe.
kwa wtu wengine jina la nyerere kwao ni kama vile jina la mungu. kama ilivyokuwa kwa mungu hachambuliwi makosa yake, vile vile iwe kwa nyerere!!!!!!!!!!!!! nawapa pole sana !
 
tukiacha , uyanga na usimba, nyerere angefanya kitu kimoja ktk katiba ya nchi, kwa niaba ya wananchi awatwalae hapo angeoneka nabii. angeweka kifungu kisemacho Raisi ashitakiwe kwa makosa au uzembe atakaoobainika kuufanya , wakati yeye yupo madarakani.
matokeo yake kifungu kama hicho cha kuwashitaki watwala wa tanzania kila wafanyapo makosa au kuabuse power, hakiwezekani kuwekwa tena katika katiba.
Hapana na si kweli.
Rasimu ya katiba iliyopo haizuii mtu kupeleka hoja hiyo.Wananchi WAnapaswa kushinikiza kifungu kiwekwe.

Lakini pia lazima utambue kifungu kizima kinasemaje na si kama usemavyo.
Kinachopaswa kusemwa ni rais kushtakiwa kwa makosa yasiyohusiana na utendaji wake aliyoyatenda akiwa madarakani.Kumshtaki rais kwa makosa aliyoyafanya kirahisi kama unavyomaanisha ni kumuonea.

Yapo majukumu ambayo hayatamfurahisha kila mmoja na yatakuwa makosa hata kama ni sahihi.
Rais akisaini baba yako kunyongwa hilo ni kosa la rais kwako hata kama misingi ya sheria inamruhusu hivyo.
Lakini rais akitumia Ikulu kufanya biashara kama Ben Mkapa hiyo nakubaliana nawe.

Sasa sijui unamhukumu Nyerere kwa lipi kwasababu hayupo madarakani na duniani maika zaidi ya 30 sasa.
Uzembe wetu ndio tatizo letu na si Nyerere.
 
Leo rais Kikwete analipwa mshahara na masurufu yake milioni 47.8, wakati kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa umma ni 180,000,

Mwezi wa saba mwaka huu 2013 kuliibuka mgogoro idara ya uratibu na maslahi ya rais baadhi wakitaka mshahara wa rais na masurufu yake upandishwe hadi milioni 60,

Mwaka 1966 uchumi wa nchi ulikuwa kwenye vipimo vya wastani wa nchi inayokua kistaarabu, na leo mwaka 2013 uchumi wa nchi upo kwenye kasi ya mdororo usioridhisha!
Tafteni tofauti ni asilimia ngapi?

Mwalimu Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache duniani
waliokufa MASIKINI kabisa, hakuwa na hisa kwenye kampuni yoyote ya ndani au nje ya nchi, hakuwa na biashara yoyote zaidi ya utumishi, hakuwa na hata nyumba ya sifa zaidi ya kulazimishwa kujengewa, na zaidi Mwaka 1966 mshahara wake ALIUPUNGUZA kutoka shilingi 5,000/= hadi 3,000/= pesa nyingine alisema iende kwa Walimu na Madaktari,

Leo tunamjadili kwakumlinganisha na wafanyabiasha waliopo ikulu? Wauza madawa ya kulevya waliopo ikulu? Mafisadi waliopo ikulu?


Kuokoteza visababu vya kipuuzi kwaajili ya kuziba udhaifu na ufedhuri wenu havitawaokoa!
 
kwa wtu wengine jina la nyerere kwao ni kama vile jina la mungu. kama ilivyokuwa kwa mungu hachambuliwi makosa yake, vile vile iwe kwa nyerere!!!!!!!!!!!!! nawapa pole sana !
Na kwa watu wengine Nyerere ni 'shetani' ytaundwa makosa akiwa kaburini, atasomewa mashataka na huku akiwa huko huko karibuni.
Kama si Nyerere tusingekuwa na Richmond, EPA, Meremeta, Kagoda n.k.

Njia rahisi na nyepesi ya kukwepa ukweli wa matatizo yetu ni Nyerere aliyeondoka duniani miaka 15 iliyopita.
Hakuna tatizo kumchambua Nyerere lakini ifanyike basi kwa ukweli na vigezo sahihi.
Mchambuzi kachambua kwa kuweka record na facts wazi, sasa sijui nukuu ya mstari mmoja inaweza kuwa uchambuzi!!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom