Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Wa NHC USD 13000 kwa mwezi,hapo zamani nafikiri kwa sasa inawezekana kajiboreshea zaidi

13000usd 1usd =1600 times 13000 unapata =20,800,000 ndio mshahara wake na kama kajiboreshea basi ni balaa tupu niyo ukiachia Nyumba ya kuishi usafiri yeye na familia yake tote vocha za simu dharula chai yake na ya wageni kazini na nyumbani yaani upuuzi ni mwingi huwa inazidi hadi mshahara so unaweza kuta jamaa kwa mwezi anaondoka na m80 au m100 kwa Raisi ni kufuru kwa jinsi navyomfahamu tokea pale alipopewa uwaziri wa fedha akaanza makeke yake akilitaka lile Range rover 4.6 akatanue nalo bagamoyo huku akimkataa dereva wa hilo gari wakati sheria zilikuwa haziruhusu
 
Inashangaza...Inasikitisha...Inatia Hasira....Inatia Kichefu chefu....Inaumiza....Kwamba Uzi huu Unaingia Mwaka wa SITA lakini Bado Sijaufahamu Mshahara wa Raisi anaolipwa kutokana na Kodi ninayokatwa. Bado Ni SIRI kubwa kwa Watanzania....!!:tape2: :dizzy
 
kama jibu limekosekana...ni siri...labda kwa kuwa si haki ya kikatiba kujua
sasa tutoe maoni katiba mpya itangaze kuwa mishahara ya viongozi wa nchi sio siri...................ili tuweze kudai kujuzwa/.....
naju wengine mtasema tu......msisahau ni haki yangu kikatiba kutoa maoni yangu...
 
Jamani kuna mtu anayejua mshahara wa raisi wa Tanzania ni kiasi gani? Kuna mtu kaniambia ni $200,000 na kitu kwa mwaka...sikuamini lakini akanihakikishia kuwa taarifa zake ni za uhakika. Bado ninasita kuamini ingawaje sina taarifa zozote na sijawahi kuona mahala popote pale kuhusu mshahara wa raisi.

Na mshahara wa makamu wa raisi..?
Waziri mkuu..?
Spika wa bunge..?
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, polisi,magereza..?
Jaji mkuu..?

Kama kuna mtu anayejua...ni wapi tunaweza kupata taarifa hizi?


$200,000 ndiyo mshahara wa Rais kwa US kwa mwaka mzima.

Rais anayelipwa zaidi Duniani ni wa Cameroun,, zaidi ya USD 1 ml kwa mwaka.

Anaweza kuwa na salary ndogo, lakini marupurupu yakawazidi wote Duniani.
 
nimefurahi kuona hamasa ya watanzania hawa wanaopenda kujua mshahara wa raisi wao. tuulizane! lengo ni kujua tu mshahara au kujua, moja vigezo alivyopewa kuvifikia ili kupata mshahara huo an mbili, kama vigezo hivyo anavifikia. huwezi kulinganisha mshahara wa raisi wa marekani, au wa afrika kusini na raisi wa tz. majukumu tofauti kabisa. hili labda liwekwe kwenye katiba mpya>
 
nia na madhumuni nikwamba waende sawa na uchumi wa marekani..! na wao wanaamini kwamba uchumi wa mareka ni minor case kushuka...! kwahiyo mishaara yao itaendelea kuwa juuu tuu kama wakitumia fedha hiyo ya USD...! WEWE HUJIULIZI KWANINI MUHINDI ANAUZA LAPTOP KWA USD WAKATI YUPO TANZANIA..! BASI SERIKALI WANA NIAMOJA NA MUHINDI..! ULIZA CHUO CHA IMTU NA CHUO CHA KIU...! kilichitokea wakati wakiwalipisha wanafunzi ada kwa USD..! Tena hawa kampala university ni waganda ningewaona wanabusara kutumua hela ya kwao lakini haikutosha wakaenda kutumia hela ya marekani...YOTE HAYO TUNAFANYIWA HUMU NCHINI MWETU:yo:
 
kama jibu limekosekana...ni siri...labda kwa kuwa si haki ya kikatiba kujua
sasa tutoe maoni katiba mpya itangaze kuwa mishahara ya viongozi wa nchi sio siri...................ili tuweze kudai kujuzwa/.....
naju wengine mtasema tu......msisahau ni haki yangu kikatiba kutoa maoni yangu...

Hapo umenena
 
Hi
These bungee must comprehend the problem is not about pay rise; it is about improving efficiency.
 
Damn it,for all those damn years and still uknown,what the secret behind it?
 
Nyerere in one of his speech aliwai sema yeye alikuwa akilipwa 4000 na ikawa haitoshi yeye kulipia mkopo wa nyumba ikabidi nyumba airudishe serikalini
 
Jamani kwa watanzania tunapenda sana kuendekeza siri yaani kila kitu siri hata katika mapenzi tu siri. Huku kutaka kufahamu mishahara ya hawa watu ni kujiongezea hasira ndani ya mioyo na kushindwa kufanya kazi za kutuletea mkate wetu wa kila siku.

Ni vyema kufanya yetu na ikiwezekana tutumie njia mwafaka ikiwemo maandamano ili kulazimisha watawala wetu watueleze hadharani wanagawana kiasi gani katika kodi zetu kila mwezi?
 
kwakweli hata mimi sijui ni sh ngapi
kwa unaefahamu usiogope kukatwa kucha na kung'olewa meno

HILI SHAVU KWAKO TILILIKA
 
Back
Top Bottom