JAMANI ULIPAJI KODI NI JUKUMU LA KIZALENDO KWA MAENDELEO YA NCHI YETU' HIVYO RAIS SHARTI AJUMUISHWE KIKAMILIFU KATIKA HILI NA KUJULIKANA TAASISI INAYOMPANGIA MSHAHARA NA MARUPURUPU YOTE
Huo USIRI ndio tunaoupinga vibaya sana.
Maadam umesema rais ni 'Mtumishi' basi atakua na bosi wake ambaye ni 'Mtumikiwa'. Huko nyuma pengine usiri wa mshahara wa rais kuwa siri nchini ulipata kuwa ni fesheni lakini leo hii ambapo tunazungumzia zaidi uwazi na uwajibikaji, KATIBA MPYA ipate kutuongoza katika hili - kote duniani mshahara wa rais haina usiri wowote.
Kama hayo maelezo hayatoshi basi mfano raisi na jirani kwetu zaidi ni kwamba ni majuzi tu tumepata kusoma magazetini kwamba huko nyuma Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, alipata kutajwa kupokea mshahara wa kiasi cha Ksh 2,000,000/- (sawa na 35,000,000/-).
Lakini hivi sasa yasemekana kwamba Tume ya Mishahara kwa Watumishi wa Umma nchini humo hivi majuzi tu wamepata kupiga panga mshahara wa rais hadi sasa Uhuru Kenyatta kupokea Ksh 1,200,000/- (sawa na Tsh 21,000,000/-).
Jamani tusichezeane akili, sisi ndio walipakodi na ndio tunaolipa watumishi wote mishahara hivyo hatuna budi kuanzisha Tume ya Mishahara ya Umma yenye mamlaka na utendaji wa kujitegemea ili itusaidie kupanga mishahara ya kila mtumishi, kupima utendaji wa kila mmoja na kuhakikisha kila mtu analipa kodi.
rais ni mtumishi. Mshahara wa mtumishi ni siri. Mbona mna vichwa vizito?