Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Mishahara ya viongozi wa Tanzania

HIvi mshahara wa mwenyekiti wa kijiji ni bei gani? Ninachojua mimi mwenyekiti wa kijiji ni rais wa kijiji sasa kwanini yeye halipwi mshahara halafu Rais wa nchi alipwe mshahara? Uwekwe utaratibu mishahara igawanywe kulingana na level ya utendaji.

Halafu wakuu wa mikoa na wilaya tufanye kuwachagua. Kwanini tuwe na uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji na Rais, halafu wenyeviti wa kata, tarafa wilaya na mikoa hatuchagui?
 
naskia umeongezeka hadi 68.1

eeeh!?
Nimeshangaa nusu ya kuzimia.
Mbona haimtoshi?
Ukichanganya na safari zake 356 kila moja =250mil
250 x356=89,000mil
Ongeza 47millxmiaka 5=237mil.
Ongeza 68.1millx5miaka ijayo.=340.5mil.

Total=89,577.5mil
hadi nimeshindwa kuhesabu.

Kujumlisha tembo wa kinana+epa+dowans+rich-monduli+kiwila coal mine scandal+meremeta+buzwagi+....

Haki ya Mungu hii nchi tusinge kuwa masiki kamwe endapo viongozi wetu wangekuwa wazalendo.
 
Kwenye katiba mpya, mwajiriwa namba moja katika ofisi za umma ambaye nni Rais wa nchi sharti awe ni MLIPAKODI namba moja.

Chini ya wazo hili hapa ni lazima rais atajwe mshahara wake wazi, majukumu yake ya kazi na jinsi gani ya kupima utendaji wake kama mfanyakazi yeyote yule.

Sababu yangu ya kusema hivo ni kwa kuwa ni mtu huyu huyu ndiye tunayemhudumia kwa gharama kubwa zaidi kwa kutumia kodi zetu kuliko afisa yeyote yule.

wewe ni great thinker, umeweka wazo hili kwa tume ya katiba. Usikute umeliweka humu tu!!
 
HIvi mshahara wa mwenyekiti wa kijiji ni bei gani? Ninachojua mimi mwenyekiti wa kijiji ni rais wa kijiji sasa kwanini yeye halipwi mshahara halafu Rais wa nchi alipwe mshahara? Uwekwe utaratibu mishahara igawanywe kulingana na level ya utendaji. Halafu wakuu wa mikoa na wilaya tufanye kuwachagua. Kwanini tuwe na uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji na Rais, halafu wenyeviti wa kata, tarafa wilaya na mikoa hatuchagui?

sasa Babu kawatoeni kwenye Mchakato wa Katiba mtaisoma namba, hayo mapendekezo mbona hukuyatoa kwa Mzee Warioba
 
sasa Babu kawatoeni kwenye Mchakato wa Katiba mtaisoma namba, hayo mapendekezo mbona hukuyatoa kwa Mzee Warioba
Nilishayapeleka. Lakini sina uhakika kama watayaingiza, kwa kuwa process ya kupata katiba imetekwa na CCM. Maana CCM hawana muda na maoni yenye maslahi kwa taifa, isipokuwa yenye maslahi kwa chama chao.
 
kwakweli hata mimi sijui ni sh ngapi
kwa unaefahamu usiogope kukatwa kucha na kung'olewa meno

HILI SHAVU KWAKO TILILIKA

Daaaah umenkata steam kinoma mi nkajua una figa halisi, yaani wanaojua ni usalama wa taifa tu lakini naomba msininotoe kunja naombeni msamaha
 
Kulingana na mpango ambao umekuwepo tokea serikali ya awamu ya kwanza hadi kufikia serikali hii ya awamu ya nne Rais halipwagi mshahara anapewa posho na marupu rupu tu. Hakuna mshaara wa rais na kama unabisha, taja mshaara wake hapa acha kuzuga.
 
JAMANI ULIPAJI KODI NI JUKUMU LA KIZALENDO KWA MAENDELEO YA NCHI YETU' HIVYO RAIS SHARTI AJUMUISHWE KIKAMILIFU KATIKA HILI NA KUJULIKANA TAASISI INAYOMPANGIA MSHAHARA NA MARUPURUPU YOTE

Huo USIRI ndio tunaoupinga vibaya sana.

Maadam umesema rais ni 'Mtumishi' basi atakua na bosi wake ambaye ni 'Mtumikiwa'. Huko nyuma pengine usiri wa mshahara wa rais kuwa siri nchini ulipata kuwa ni fesheni lakini leo hii ambapo tunazungumzia zaidi uwazi na uwajibikaji, KATIBA MPYA ipate kutuongoza katika hili - kote duniani mshahara wa rais haina usiri wowote.

Kama hayo maelezo hayatoshi basi mfano raisi na jirani kwetu zaidi ni kwamba ni majuzi tu tumepata kusoma magazetini kwamba huko nyuma Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, alipata kutajwa kupokea mshahara wa kiasi cha Ksh 2,000,000/- (sawa na 35,000,000/-).

Lakini hivi sasa yasemekana kwamba Tume ya Mishahara kwa Watumishi wa Umma nchini humo hivi majuzi tu wamepata kupiga panga mshahara wa rais hadi sasa Uhuru Kenyatta kupokea Ksh 1,200,000/- (sawa na Tsh 21,000,000/-).

Jamani tusichezeane akili, sisi ndio walipakodi na ndio tunaolipa watumishi wote mishahara hivyo hatuna budi kuanzisha Tume ya Mishahara ya Umma yenye mamlaka na utendaji wa kujitegemea ili itusaidie kupanga mishahara ya kila mtumishi, kupima utendaji wa kila mmoja na kuhakikisha kila mtu analipa kodi.


rais ni mtumishi. Mshahara wa mtumishi ni siri. Mbona mna vichwa vizito?
 
Wakati mwingine ni busara kubaki kimya badala ya kuleta mzaha katika mjadala mzito wenye maslahi makubwa kwa Waheshimiwa Walipakodi wa vyama vyote vya siasa nchini kikiwemo hicho chama chako pendwa - CCM.

Mshahara wa Padri Slaa ni kiasi gani?
 
RAIS WA NCHI KUTOKULIPA KODI NA BADALA YAKE KURUHUSIWA KIKATIBA KUWA 'MCHWA WA KODI ZA RAIA WENZAKE WENGINE' NI KASHFA KUBWA NA KUKOSESHWA UWANJA WA KUONYESHA UZALENDO WAKE WA DHATI

Rais yeyote yule ANAPOKOSA KUTEKELEZA JUKUMU LA MSINGI MNO KIASI KUKOSA KULIPA KODI kwa maendeleo ya taifa analoliongoza ni kashfa ya kikatiba na fedheha katika nafsi husika kujigeuza MCHWA WA KODI ZA RAIA WENZAKE tena kwa kujilipa sirini.

Naam, katika swala hili nyeti ya kufanya mishahara ya watumishi wetu KUTOKUJULIKANA KWETU SISI MABOSI WAO katu siwezi kuiunga mkono hata kama Dokta wa ukweli, ambaye hadi sasa ana uhakika na kura yangu kumpeleka Magogoni, au rais aje awe ni rafiki yangu Zitto Kabwe baada ya miaka 10, bado napenda kuwahakikishia kwamba endapo watakosa kulipa kodi wao wenyewe, kuturidhisha kimaandishi juu ya tija katika utendaji wao na kutokuingilia utendaji wa Tume ya Mishahara ya umma katika kumpangia mshahara basi nitakua wa kwanza kwenda kusimama katika kuwapinga juu ya hili jambo.

Kati ya sifa muhimu kuangaliwa pindi mtu anapotaka kushika wadhifa wowote ule katika ofisi za umma ni katika kuturidhisha pasipo shaka kwamba unatekeleza viklivyo jukumu lako la uraia KULIPA KODI KIKAMILIFU.
 
Back
Top Bottom