Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimechoshwa na viongozi wa nchi zetu za afrika, nikana kwamba tunaongozwa na watoto wa dogo! Mungu atusaidie turudi tulikoachwa na mzee wetu nyerere kwa amani, vinginevyo hatutafika salama!
Sijui mshahara wa Rais na naamini ni katika vitu ambavyo walipa kodi wanatakiwa kujua. Mshahara wa Rais hautakiwi kuwa siri kwa mtanzania yeyote. Inapaswa kuwa wazi kabisa na kila Raia ajue. TRA watakuwa wanajua kama sio tax exempt. Nadhani tukifatilia kupitia Utumishi tunaweza kupata hizo data. Hebu ngoja nipeleke swali Bungeni kuhusu jambo hili ili lijibiwe Mkutano ujao wa Bunge. Haya ni mambo ambayo tuna overlook sana.
Mwaka 2008 wakati tunapitisha sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly administration act) niliwasilisha ammendment kuwa mishahara ya wabunge na mawaziri iwe wazi na iwekwe online watu waweze ku access. Nikajibiwa ni siri ya mtu. Rais ni mtu ndio, lakini sio mtu kama mtu mwingine. Ni mtu mwenye maamuzi kuhusu mwelekeo wa Taifa. Ni vizuri kujua tunamlipaje. Ngoja na mimi niwaulize, Nani anajua mshahara wa Mbunge wa Jimbo lake hapa?
labda kurahisiha anayejua TGSS J, K ,L na kuendelea. TGSS ndo salary code ya watumishi wa serikali kuu. Akitokea mtu akataw na data hizo TGSS( Tanzania Gov Salary Scale) zinawakilish kiwango gani basi tunaweza kuwa na kadirioa la karibu na ukweli nani anapata kiasi gani.
Hawa wakubwa ngazi zao za mishahara nadhani itakuwa kuanzia TGS J.
Assumption/makadirio yangu ni kuwa
TGS J= wakurugen
Jamani kuna mtu anayejua mshahara wa raisi wa Tanzania ni kiasi gani? Kuna mtu kaniambia ni $200,000 na kitu kwa mwaka...sikuamini lakini akanihakikishia kuwa taarifa zake ni za uhakika. Bado ninasita kuamini ingawaje sina taarifa zozote na sijawahi kuona mahala popote pale kuhusu mshahara wa raisi.
Na mshahara wa makamu wa raisi..?
Waziri mkuu..?
Spika wa bunge..?
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, polisi,magereza..?
Jaji mkuu..?
Kama kuna mtu anayejua...ni wapi tunaweza kupata taarifa hizi?
Wa NHC USD 13000 kwa mwezi,hapo zamani nafikiri kwa sasa inawezekana kajiboreshea zaidiacha noma Dau wa nssf anachukua zaidi ya kumi iweje raisi ndie awe top? Nenda Tanroad ndio utakimbia zaidi ya m35 nakumbuka hadi wabunge walikuja juu baada ya kugundua