Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Sio tu hatujui mshahara wake,hata kodi halipi wakati obama analipa

HALIPI KODI KWA MUJIBU WA SHERIA ZILIZOTUNGWA NA WABUNGE TULIOWACHAGUA WENYEWE MFANO SHERIA YETU YA KODI YA MWAKA 2010 INASEMA WAZI NA KUANISHA MAPATO YA RAIS KAMA IFUATAVYO;
The following amounts are exempt from income tax (a) amounts derived by the President of the United Republic or the President of the Revolutionary Government of Zanzibar from salary, duty allowance and entertainment allowance paid or payable to the President from public funds in respect of or by virtue of the office as President; please read section 10 of the income tax act 2010 and its third schedule.
 
Laiti ningalikua rais ningalijitolea kulipa kodi bila kuachia raia wenzangu wengine kunibeba beba begani hivi.
 
Jamani kuna mtu anayejua mshahara wa raisi wa Tanzania ni kiasi gani? Kuna mtu kaniambia ni $200,000 na kitu kwa mwaka...sikuamini lakini akanihakikishia kuwa taarifa zake ni za uhakika. Bado ninasita kuamini ingawaje sina taarifa zozote na sijawahi kuona mahala popote pale kuhusu mshahara wa raisi.

Na mshahara wa makamu wa raisi..?
Waziri mkuu..?
Spika wa bunge..?
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, polisi,magereza..?
Jaji mkuu..?

Kama kuna mtu anayejua...ni wapi tunaweza kupata taarifa hizi?

Hizi taarifa kwa Tz kuzipata hata uzitafute mchana na usiku kamwe hutozipata
 
nakumbuka kuna wakati mwalimu alijipunguza mshahara kutoka shilingi 4000 hadi 2000 kwa mwezi! Tukijadili kinadharia hivi kuna ubaya gani hii mishahara (na mingine inayolipwa kwa kodi ya wananchi)ikiwa wazi? Au kuna faida gani ikiwa wazi?



mkapa wakati anastaafu mshahara wake ulikuwa tsh 9,000,000/= kwa mwezi. Sijui jk analipwa ngapi kwa mwezi. Mshahara wa rais haukatwi kodi
 
Tatizo sio mishahara hata wangelipwa buku 5 je wanafanya kazi zao ipasavyo au wanaishia kula posho bure tu bila kuleta results................Wabunge lazima wawajibike.
 
hii ni nchi ya kifisadi zaida na si vinginevyo na haya mabadiliko ya katiba ni lazima yaliangalie hili suala
 
baba yangu ni mwenyekiti wa kitongoji analipwa 3000 kwa mwezi
 
Swali zuri sana na nadhani Ikulu watakapo kamilisha site yao ni vizuri wakiziweka habari hizi wazi kwa wananchi kuziona... Waajiriwa wote wateuliwa na rais ni vizuri tukifahamu mishahara yao!
we unalipwa sh. ngapi??? SAMAHANI KAMA HUTO JALI
 
duh! Kweli suala la kuhoji kuwa rais na watumishi wengine nyeti kuwa wanalipwa mshahara kiasi gani ni swali ambalo linaweza lisipate jibu kirahisi mpaka uwe sehemu nyeti wewe mwenyewe otherwise hakuna. But ninachokiona mimi ni kusimama pale panapotakiwa kuwa na ukweli halafu uongo ume2mika.

Kaza msuli kufanya kazi yako. Mishahara yao itakuumiza kichwa hata uambiwe ni milioni 50 hazitakusaidi atabaki kuwa juu tu.
 
Hizi taarifa kwa Tz kuzipata hata uzitafute mchana na usiku kamwe hutozipata

pia hii mishahara ni geresha tu, hawa jamaa wana access kubwa kwenye fedha za umma. Na wanaweza kuchota watakavyo! Hivyo hata tukipata figure hapa it will reflect nothing!!
 
Ukipata jibu sahihi niPM nami nijue, itakuwa hatua ya kwanza ya kudai tax free kijimshahara changu
 
wadau mnataka nambia wakuru wao wanagonga dolari za obama sisi wanatupa madafu?

Duu! lakini mkuu ww unatafuta salaries za wanene wakati kujuwa tu mishaharar ya wakurugenzi wakuu wa taasisi nyingi za serikali ni issue? kujuwa tu tajiri namba moja tanzania ana kiasi gani hawasemi. Bongo kila kitu siri.
 
Back
Top Bottom