Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Kujua Mishahara haitusaidii sana inatakiwa tujue walificha mabilioni uswisi na tuweze kuyarejesha nchini
 
kwani itasaidia nini ukijuwa mishahara yao, wenzetu ulaya na marekani wanajuwa ya viongozi wao lakini wao hawategemei mishahara wanategemea network yao ya biashara, hawa wa kwetu wanategemea mishahara, sasa wewe itakusaidia nini kujuwa japokuwa inatokana na kodi zetu, mimi ningependa kwanza kujuwa mshahara wako
 
kwani itasaidia nini ukijuwa mishahara yao, wenzetu ulaya na marekani wanajuwa ya viongozi wao lakini wao hawategemei mishahara wanategemea network yao ya biashara, hawa wa kwetu wanategemea mishahara, sasa wewe itakusaidia nini kujuwa japokuwa inatokana na kodi zetu, mimi ningependa kwanza kujuwa mshahara wako

Mshahara wangu hautokani na kodi yako kwa hiyo huna haki ya kuujua. Kwa upande mwingine, kimsingi, sisi wananchi ndiyo waajiri wa hao viongozi. Ni pesa zetu za kodi tunazolipa ambazo zinatumika kuwalipa mishahara pamoja na marupurupu yao.

Hivyo, sisi kama waajiri wao tuna haki zote za kujua hao waajiriwa wetu tunawalipa kiasi gani kwa kazi ambazo tumewaajiri watufanyie. Jiulize swali jepesi tu, ni mwajiri gani asiyejua mshahara anaomlipa mwajiriwa wake? Kama yupo naomba nitajie.

Vilevile, kuna suala la uwazi. Walipa kodi tuna haki zote za kujua pesa zetu zinatumiwaje, mishahara ikiwemo. Kujua ni haki yetu halali na ya msingi kabisa. Usiri wa nini kwenye matumizi ya pesa zetu? Tukijua kitaharibika nini? Uwazi wa watumishi wetu wa umma pamoja taasisi wanazozitumikia ni jambo la muhimu sana katika kujenga imani baina ya wananchi na serikali yao.

Mimi nataka kujua na kuna wengine pia nao wangependa kujua. Wewe kama hutaki shauri yako. Kama kwako kujua siyo muhimu basi fumba macho na/au ziba masikio. Sisi tunataka kujua.
 
kiukweli mimi ningependa sana kujua kiasi ambacho hawa viongozi wetu wanavyochukua,kama yupo anaejua Afunguke..!
 
Jamani kuna mtu anayejua mshahara wa raisi wa Tanzania ni kiasi gani? Kuna mtu kaniambia ni $200,000 na kitu kwa mwaka...sikuamini lakini akanihakikishia kuwa taarifa zake ni za uhakika. Bado ninasita kuamini ingawaje sina taarifa zozote na sijawahi kuona mahala popote pale kuhusu mshahara wa raisi.

Na mshahara wa makamu wa raisi..?
Waziri mkuu..?
Spika wa bunge..?
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, polisi,magereza..?
Jaji mkuu..?

Kama kuna mtu anayejua...ni wapi tunaweza kupata taarifa hizi?

haya ndio mambo muhimu.watuambie
 
ukijaji mishahara utakufa kwa presha bure!! acha wale yupo jaji mkuu "Yesu" atawahukumu ck ya mwisho n her upate tabu dunian kulko mbinguni.
 
Kwa nilivyo angalia mshahara wa OBAMA kwa mwaka ni $500,000, but png inawezekana au la kwa JK kupata hapo TZ pesa zipo but ndo ivyo zimekaliwa
 
Niliona hapa, kama sikosei kwenye topic moja kuhusu mkapa, mdau moja alisema mshahara wa rais ni $12,000 kwa mwezi.

Kama nimekosea naomba nirekebishwe

Mpaka raisi wa Tanzania analipwa kwa currency ya nje au ni makadirio?
 
mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa ova.

Mwajiri wa hawa viongozi wafuatao ni nani?

Makamu wa raisi.
Waziri mkuu.
Spika wa bunge.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, polisi,magereza.
Jaji mkuu.

Kama ni wananchi, kuna ubaya gani kujua mishahara yao tukizingatia kauli yako mshahara ni kati ya mwajiri na mwajiriwa...

cc Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Nenda Kaulize Mishahara ya Directors na Managers wa Executive Agencies za Serikali kama vile TCRA, TCCA, SUMATRA, TRA, na TPA.
ndugu yangu utakufa kwa PRESSURE. Dereva anapata Basic Salary 900,000/= Wasomi wanapata basic 420,000/ = kwingineko.
 
Kuna mkuu wa idara ya ndege ya rais anavuta ki2 cha TZSH18mil kwa mwez.
Chief officer.
 
Nakumbuka kuna wakati Mwalimu alijipunguza mshahara kutoka shilingi 4000 hadi 2000 kwa mwezi! Tukijadili kinadharia hivi kuna ubaya gani hii mishahara (na mingine inayolipwa kwa kodi ya wananchi)ikiwa wazi? Au kuna faida gani ikiwa wazi?

Na kuna hasara gani isipokua wazi?
 
Jamani kuna mtu anayejua mshahara wa raisi wa Tanzania ni kiasi gani? Kuna mtu kaniambia ni $200,000 na kitu kwa mwaka...sikuamini lakini akanihakikishia kuwa taarifa zake ni za uhakika. Bado ninasita kuamini ingawaje sina taarifa zozote na sijawahi kuona mahala popote pale kuhusu mshahara wa raisi.
Kama kuna mtu anayejua...ni wapi tunaweza kupata taarifa hizi?

Haya nyingine hizi hapa

Leo rais Kikwete analipwa mshahara na masurufu yake milioni 47.8, wakati kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa umma ni 180,000,

Mwezi wa saba mwaka huu 2013 kuliibuka mgogoro idara ya uratibu na maslahi ya rais baadhi wakitaka mshahara wa rais na masurufu yake upandishwe hadi milioni 60,
 
Back
Top Bottom