Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Unaweza kucheza na vyote lakini sio msiba.. Misiba Afrika ni kama mila na desturi.. Ni utamaduni wenye nguvu bado
Kuna muunganiko wa ajabu na wenye nguvu sana kwenye mila na desturi za Kiafrika na wageni wanautamani lakini hawawezi tena maana walishaharibu
Nadhani ndio chimbuko la Ubhuntu kwamba sisi ni wamoja langu lako na lako langu!
Matunda ya huu muunganiko ni haya (japo sasa unakufa kwa baadhi ya vipengele)
1. Kikipikwa chakula mpishi ataambiwa aongeze kidogo kunaweza kuwa na mgeni
2. Mgeni akifika bila taarifa na chakula kilishapikwa atakaribishwa hicho hicho
Kusaidiana na kushiriana kazi za kijamii kama ujenzi, kilimo, harusi , jando nk...
Kwenye ujenzi na kilimo mhusika halipi hela mbali huandaa chakula na vinywaji kwa washiriki Kwenye sherehe mbali mbali waalikwa kila mtu huleta alichonacho kwa hiari na bila kupangiwa
Usithubutu kwa namna yoyote ile kukosa shughuli mbali tatu mfululizo. Utatengwa na Jamii yote Kuna baadhi ya matukio unaweza kuyaruka lakini makinika sana kwenye ugonjwa na misiba..
Wana msemo wao kama tulifurahi pamoja bali hata kwenye kulia tulie pamoja
Wagonjwa was Afrika walikuwa hawana shida .. Maana Jamii inayomzunguka itampa support ya kila kitu
Matukio ya misiba ndio sensitive zaidi.. Utakavyofanya kwenye misiba ya wengine ndivyo watakavyofanya kwenye misiba inayokuhusu
Kama Kazi yako ilikuwa kutoka rambirambi tuu nao watafanya hivyo hivyo kwako
Kama ulikuwa huli kwenye misiba yao, siku likikufika watafanya kila kitu ila hawatakula hata kama umeandaa biriani na nyama choma Kama hukuwepo siku ya msiba mpaka mazishi ukirudi nenda kahani.. Huo ndio upendo..LAKINI kamwe usiondoke siku msiba umeshatokea.. Ahirisha mambo yako nenda kaonekane, kaa kidogo kisha omba udhuru ondoka
Kuna wachache watakaokusema vibaya lakini wengi kwenye hao wachache watakutetea na kukusema vizuri
Bado utamaduni wa kuzikana una nguvu sana Africa!
Usiende mpirani kisha urudi kutoa pole.. Kwa kuona haya wanaweza kukupokea lakini moyoni wana kisasi nawe!
Hicho kisasi kitatungwa mimba
Hiyo mimba italelewa na kuzaliwa mtoto
Mtoto kisasi akikua na kukomaa kifuatacho ni malipizi..!
Good morning Tanganyika❤❤❤