Misiba mingi ya Wakristo ina gharama kubwa kuliko wengine

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Zama za leo ni tofauti kabisa na zama za mababu zetu. Ukisoma vitabu vya dini utagundua kuwa mazishi hayakuhitaji hata majeneza. Mfano Lazaro inaonesha alizikwa tu na sanda pasi na jeneza.

Leo hii watu wanashindana hadi kwenye gharama za majeneza. Hivi kwanini basi majeneza yote yasiwe yenye ubora unaolingana ili kuondoa hii tofauti?

Mtu akipata msiba anawaza namna gani aufanye msiba huo uwe wa kifahari! Na wakati mwingine marehemu alikosa msaada wa tiba bora; na huenda ndio hasa chanzo cha kifo chake!
 
Misiba ya watu kwa interest zao unasema ya kikiristo.

Wapi kwenye biblia wameweka gharama za misiba??
 
Usiniquote vibaya mkuu.
Nimesema ya kikristo kwasababu kwa asilimia kubwa ndiyo huwa na mchakato mrefu! Tofauti na dini nyingine ambao wao mazishi hayahitaji hata jeneza. Samahani kama utakuwa umeelewa tofauti
 
Michakato gani ya kikikristo inataka pesa nyingi.

Mfano, Mimi kwetu misiba ni ya Jamii nzima, kila mfiwa kwa uwezo wake. Kazi ya viongozi wa dini ni kusoma ibada ya mazishi tu na nyimbo za kusindikiza mwili.

Nimekuja Uchaggani, Kuna shida kubwa: MC analipwa, wachimba kaburi wanalipwa, padre analipwa.

Bado hujakodi muziki, viti wapishi na hema.

Sasa hapo utasingizia ukiristo au tamaduni binafsi za watu fulani??
 
Walikuomba mchango wa jeneza ?
Michango ya msiba ni mikubwa na unalazimishwa kutoa.
Watu wengi leo hii wakupatwa na msiba wanawaza namna ya kuufanya uwe wa kifahari. Wanashona sare, wanaandaa ukumbi nk.

Mbaya zaidi usipotoa mchango unatengwa! Sasa swali langu ni je kuna umuhimu wa hayo yote?
 
Wapi huko wana lazimisha kutoa ?
 
Mfano, Mimi kwetu misiba ni ya Jamii nzima, kila mfiwa kwa uwezo wake. Kazi ya viongozi wa dini ni kusoma ibada ya mazishi tu na nyimbo za kusindikiza mwili.

Nimekuja Uchaggani, Kuna shida kubwa: MC analipwa, wachimba kaburi wanalipwa, padre analipwa.
Jitahidi sana kutofautisha kati ya 'mingi' na 'yote!'
 
Roho ya umaskini inakuandama rafiki!

Hii issue imekaa kiutamaduni zaidi kuliko kiimani mfano misiba mingi kule home naonaga watu wanaandaa t-shirt za maombolezo, mziki wa kuwafariji, MC na taratibu za usafir wa wanafamilia kwa kipindi Cha kumpuzisha mpendwa wao plus chakula! Hapo hujapiga gharama za safari kutoka dar mkifika mombo😁mnywe mle

Issue sio Imani ni taratibu za kimila au familia tu wanaamua
 
Kama hutak gharama badili dini uende ambapo hakuna gharama
Ni upumbavu tu watu vichwa hawavifikirishi wanazipa shingo tabu kubeba matikiti maji.

Muone huyu analalamika gharama za jeneza,jeneza si linanunuliwa kutokana na rambirambi za watu?na kama la gharama au siyo la gharama kila mtu atasitiriwa kutokana na mazingira aliyoishi na jamii husika sidhani kama ni kitu cha kulalamikia hiki.
 
We kama huna uwezo wa kuzika jamaa zako Kwa shuka na watumbukize kwa mwana ndani ila ss tunaowapenda wapendwa wetu lazima tuwafanyie sherehe ya mwisho
 
Watu dizain hii unakuta kwao ukoo mzima hakuna anayeweza ku-spell million moja kwa tarakimu.

Shida tupu!

mara nyingi utoaji wa hela za kufanikisha kumpuzisha na kumsitiri mpendwa wenu hua ni hiari sijawahi ona mtu akilazimishwa🤔🤔

Nahis Lengo lake halikua msiba alikua anatafuta namna ya kuattack Imani za watu
 
Na hata hao wanaojisifia kwamba hawana gharama ni umaskini wao tu na roho mbaya.

Misiba ya waarabu wakitoka kuzika wanakula biriani au pilau wa Mndengereko wa Kilwa kwa sababu wameshaamini wao ni maskini wakinywa uji wanaona ndiyo msiba wa bei rahisi hajui ipo misiba ya Kikristo watu wanakula wali maharage.
 
Back
Top Bottom