LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Makaburi yenyewe ni gharama tupu, wauza majeneza wanatengeneza majeneza ya gharama tofauti kila uchao. Zamani ilikuwa mbao tu zinarandwa linaundwa sanduku mtu anazikwa nalo. Wakaanza kupaka vanishi, wakapandisha bei. Sasa hivi wanaweka hadi vidani na marembo ya kila aina. Ni bajeti yako tu upate la gharama gani. Kwenye misosi nako ni gharama tupu. Ukipika ugali maharage watu hawali wanataka upike vyakula vya kifahari. Angalau wali mweupe watakula kwa shingo upande. Ukubwa wa msiba huendana na gharama za mazishi